Rais Samia Suluhu Hassan kulihutubia taifa leo Desemba 31, 2021

Rais Samia Suluhu Hassan kulihutubia taifa leo Desemba 31, 2021

Akitaka hotuna yake iwe na maana kwa watanzania aguse mambo ya msingi yanayolihusu taifa kwa sasa.

1. Katiba Mpya.

2. Uhuru wa vyombo vya habari.

3. Kubambikia wapinzani kesi za uongo.

4. Ajira.

Mambo mengine kama;

- SGR

- Ujenzi wa vyumba vya madarasa.

- Vituo vya afya na barabara nayo ni muhimu lakini tumeshazoea kuyasikia.
Na upatikanaji wa crane kule Rufiji,huu mradi bi mkubwa kapigwa pini kuuongelea kama haupo nchini mwake vile.
 
Tatizo hotuba zake ziko juu hazizungumzii changamoto za wananchi. Kama ile hotuba yake ya miaka 60 ya uhuru sijui hata alikuwa anazungumzia nini
 
Akitaka hotuna yake iwe na maana kwa watanzania aguse mambo ya msingi yanayolihusu taifa kwa sasa.

1. Katiba Mpya.

2. Uhuru wa vyombo vya habari.

3. Kubambikia wapinzani kesi za uongo.

4. Ajira.

Mambo mengine kama;

- SGR

- Ujenzi wa vyumba vya madarasa.

- Vituo vya afya na barabara nayo ni muhimu lakini tumeshazoea kuyasikia.
5.bei mbaya ya mahitaji muhimu

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Za dikteta msukuma mwenzenu hotuba zake zilijaa matusi,kejeli na pumba tupu, kichwani alikuwa mweupe
Basi labda umeamua kujitoa akili mkuu...enzi za Magu akisema leo anahutubia mpaka vibanda umiza vilikuwa vinajaa,maduka ya mangi alikuwa anaacha kuuza kwanza jinsi watu wanavyojaa kuangalia hotuba za mzee JPM.
Yani hivi leo watu vibanda umiza wangetoka kucheki game ya Yanga wangeunganisha kusikiliza hotuba ya JPM.

Na hotuba ikiisha watu wanarudi majumbani na matumaini makubwa juu ya Taifa lao.

Rip JPM
 
Tatizo hotuba zake ziko juu hazizungumzii changamoto za wananchi. Kama ile hotuba yake ya miaka 60 ya uhuru sijui hata alikuwa anazungumzia nini
Leo atasema tu tusinywe Sana, tuendeshe magari taratibu na tumuombe Mungu atupe nguvu na afya .

Kawaida Sana!
 


Dedication by Shyne.

Kwa wapambe ninauzoefu wa kunyofoa kucha.

The woman has to go
 
HOTUBA YA MAMA LAZIMA IGUSE MAMBO MUHIMU YA JAMII LAKINILISSU LAZIMA AANZE KUSIMULIA ALIPONEKAJE KWENYE SHAMBULIO NA WATU KWA NINI HAWAJAKAMATWA SASA ANATAKIWA ATANGAZE SERTA TUMUELEWE YALIYOPITA YAMEPITA
Yatapita siku wale waliompiga risasi watakamatwa na kupelekwa mbele ya mahakama.
 
Kiongozi muoga hatufai!
Wewe ndio muoga, Lissu alichofanyiwa ingekuwa Ni wewe ungefanyaje?. Umepigwa risasi , ukafukuzwa ubunge na bado ukaibiwa kura. Saa zingine kabla ya kusema Jambo tufikiri Kwanza. Kina mtu alimiattack Magufuri face to face Kama Lissu?. Unaona kilichomtokea mbowe mpaka kapewa ugaidi na hali ilivyo mpango Ni kumfunga moja kwa moja gerzani.
 
Tunasubiri kwa hamu tupate roadmap ya uchumi,siasa,jamii n.k toka kwa Mh. SSH.

Ila wasaidizi mumkumbushe mama aanze kutumbua majipu utendaji umekuwa wa kisanii sana. Watu kila ukiwafuata ofisini wanadai wako field kumbe wako kwenye shughuli binafsi ofisi za umma.

Upandaji holela wa bei za vitu

Ukatikaji hovyo wa umeme na maji

Tunapenda kujua hawa Tarura au Tanroads mbona mishe za barabara kujengwa ni kama zimeishia na JPM.
 
TUTAKUWA KANISANI TUKIMUOMBA MUNGU NA KUSUBIRI MWAKA UPINDUKE KUELEKEA 2022.
 
Aliweza mkapa kutuzungumzia kero za watanzania na kuzitatua
MH MKAPA likuwa Rais bwana acha tu.... nadhani angeongoza 20 years Tanzania ingekuwa bora sana.

Binafsi namuonaga he was the most genius President ever happen in Tanzania.
 
Hakuna jipya hapo,atume PDF mitandaoni wenye mda wasome,itakuwa haina tofauti na hotuba ya send off,Tunasubiri ya Lissu
 
Back
Top Bottom