Rais Samia Suluhu: Kusanyeni kodi kwa kutumia akili, sio nguvu

Rais Samia Suluhu: Kusanyeni kodi kwa kutumia akili, sio nguvu

Kule masasi wafanyabiashara waliokodi mabanda ya ccm kufanyia biashara wamewafungia mabanda yao yapata wiki sasa kisa eti hawajalipia kodi. Sasa ukifunga hayo mabanda hizo pesa za kodi zitapatikanaje
Jpm fufuka
 
Huyo sidhani kama ni mfanyabiashara.
Kweli Mkuu, angekuwa ndio marehemu Magufuli ameongea maneno aliyoongea Mh. Rais Samia S. Hassan hata huyu anayepinga angeshangilia na kusema kasema kweli. TRA kuna tatizo kubwa sana, hii nchi haikuwa ya kukusanya kodi ya trillion 1 halafu unajisifu. Nchi hii ni kubwa na ina vyanzo vingi vya mapato. TRA waende kwenye nchi zingine wakajifunze namna ya kukusanya kodi bila kelele na nguvu.
 
Kweli Mkuu, angekuwa ndio marehemu Magufuli ameongea maneno aliyoongea Mh. Rais Samia S. Hassan hata huyu anayepinga angeshangilia na kusema kasema kweli. TRA kuna tatizo kubwa sana, hii nchi haikuwa ya kukusanya kodi ya trillion 1 halafu unajisifu. Nchi hii ni kubwa na ina vyanzo vingi vya mapato. TRA waende kwenye nchi zingine wakajifunze namna ya kukusanya kodi bila kelele na nguvu.
Kabisa mkuu.
 
Weee mdanganye tuu,
nchi hii ni nani aliye tayari kulipa kodi stahili kwa biashara/ shuguli anayo ifanya labda mfanyakazi tuu through PAYE, Kila mfanya biashara ana wazo la kukwepa kodi ili maximize mapato yake., mwacheni rais akusanye kodi
Sio kweli, umewahi kufanya biashara wewe? Nenda TRA ukawaone wananchi wanavyojitokeza kwa wingi kulipa kodi kwa hiyari. Halafu waangalie ndugu zako wa TRA wanavyowafokea walipa kodi waliojitokeza bila shuti.
 
Sio kweli, umewahi kufanya biashara wewe? Nenda TRA ukawaone wananchi wanavyojitokeza kwa wingi kulipa kodi kwa hiyari. Halafu waangalie ndugu zako wa TRA wanavyowafokea walipa kodi waliojitokeza bila shuti.
Watendaji Wajinga.
 
Bora kasema maana huyo waziri wa feza anaweza kuagiza wafanyabiashara wanaodaiwa kodi wamwagiwe tindikali.
Hats kina Zakayo walikuwa na ujuzi na elimu ya kukusanya kodi.sasa tz waalimu tu ndio hawakusanyi kodi,ushuru na madhuhuri mengine ya serikali,utakuta afisa afya badala kuelimisha jamii mambo usafi mwaka mzima yuko busy kukusanya ushuru was taka taka na faini za uchafuzi was mazingira,afisa biashara busy anakusanya ada ya leseni za biashara,ushuru wa huduma,mabango.

Afisa mifugo bussy na ushuru was minada,machinjio,ukaguzi was nyama.afisa kilimo bussy na ushuru was mazao,afisa uvuvi bussy na ushuru was samaki,mitumbwi na kodi zingine zinakusanywa na madalali ambao wanaangalia makusanyo zaidi kuliko welfare ya mlipa kodi.

TRA wawe wanafanya assessment na makadirio halisi ya kodi badala ya kukaa ofisini wakitumia nadharia ya majeduali kukadiria kodi,kweli tuwe na watumishi was kukusanya kodi waliosomea mambo ya kodi.
 
natamani hii mentality iwe induced kwetu.
sijui wazungu wamewezaji kuzishawish jamii zao zilipe kodi.
imefika mahali wanaona aibu hata wasipo lipa kodi. yaani kwao wanasikia msukumo toka moyoni kabisa.

lini tutafika huko?
Tutaendelea kutamani kufika huko tu always, shida ya bongo kila kitu ni kukiingizia siasa tu. Wenzetu hiko kitu wamefunzwa toka utotoni ni kama utamaduni wa mtu aliyestaarabika ila japokuwa wapo vichwa ngumu hawapendi kulipa kodi ila imewekwa kama geti kwenye kila unalofanya lazma upitie kwwenye kodi incase litahusisha mapato na mwisho wa mwaka wanafanyaga Tax filing. Ukiwa mlipa kodi mzuri kuna sehemu ya hela unarudishiwa.

Ila ulaya kila kitu kiko kwenye mfumo, kodi inaelekezwa kuboresha huduma za kijamii, watoto wanasoma bure, afya iko safi! Huku kodi zinakusanywa ma Trillion ya shilingi, cha ajabu utasikia eti raisi kaiba hela! Mara sijui waziri flani kapiga billion kadhaa! Mbali na yote hamna unafuu wa maisha kwa wananchi wa hali ya chini, ni udhalimu tu. Hio motivation ya ulipaji kodi unategemea nani atakuwa nayo!
 
Huyu mama ameisha anza kujichanganya tena, akicheza kidogo tuu, nchi inarudi kwenye enzi za JK, yaani inakua full la manyani mwendo wa kujiachia tuu, milunzi imekuwa mingi sana na yeye ameanza kuusikiliza mlunzi wa kutoka kwa flanii badala ya kuwa na mlunzi wake......
 
Huyu waziri wa Fedha ana elements za ugaidi. Hafai kuwa kiongozi. Najua hata aliyemteua anafahamu hilo ila kwa sababu hakutaka kumwacha hata waziri mmoja toka baraza la zamani, kulikuwa hakuna namna.

Kabudi alitakiwa kuondolewa haraka mbo ya nje hakukuwa na mahali pa kumpeleka zaidi ya Katiba na Sheria.
 
Tutaendelea kutamani kufika huko tu always, shida ya bongo kila kitu ni kukiingizia siasa tu. Wenzetu hiko kitu wamefunzwa toka utotoni ni kama utamaduni wa mtu aliyestaarabika ila japokuwa wapo vichwa ngumu hawapendi kulipa kodi ila imewekwa kama geti kwenye kila unalofanya lazma upitie kwwenye kodi incase litahusisha mapato na mwisho wa mwaka wanafanyaga Tax filing...
hii sentensi ya mwisho ina reflect how mich mamlaka zimeshindwa kuswashawish wananchi kuona jukumu la kulipa kodi ni lao.
intead wamekuwa wakitumia nguvu zaidi kuliko akili.

itachukua muda sana kubadilisha hili
 
Sisi wananchi wenyewe kulipa kodi bila kusukumwa ni mtihani!! Ukisema leo waje kwa kulemba kwenye kodi aaah hawapati ata bilion 1 kwa mwezi. Wakwepa kodi wengi wanajua kama wanakwepa kodi na wanafanya hivo ili faida ipige maradufu.
Elewa humu kwenye bara letu la giza Africa hakuna mfanyabiashara anayelipa kodi halali,I mean ile halali kabisa kwamba mfano 1000/= kwa 370/= hata hao unaosikia wamepewa tuzo wanakuwa wameunga unga tu hesabu ila kuna sehemu wanapiga.

Kama kodi ikawa rafiki,italipwa serikalini kile kinachohisiwa kinaibwa kitaingizwa mtaani kuzungusha uchumi kwa njia nyengine kama ni kujenga nitaenda kununua materials serikali itapata tena kodi yake wapo watakaopata ajira nao wataenda kuzungusha pesa mtaani tukisema tuende straight hapa hakuna kitakachoenda.

Ukweli ni toka enzi za mitume hakuna mfanyabiashara anayependa kitu kinachoitwa kodi ila apewe elimu na apewe uhuru na makadirio mazuri mambo yataenda vizuri.
 
Hii ni kauli ya kutokujua,,watu wanakwepa kodi kila siku K'koo,vitu vya laki mbili unapewa risiti ya 65000..usipotumia nguvu,tutakula nyasi humu ndani.
Kwani wewe unalishwa na serikali au kula unatafuta mwenyewe?

Kama serikali inakulisha sawa ila kama unajilisha mwenyewe shusha pressure tafuta hela hakuna siku utakula nyasi.
 
hotuba za maza zinathibitisha maneno ya kitaa kuwa jiwe alikuwa anafanya haya mambo yeye peke yake au na washkaji zake wengine anaowajua bila kumshirikisha huyu mama.
 
Bora kasema maana huyo waziri wa feza anaweza kuagiza wafanyabiashara wanaodaiwa kodi wamwagiwe tindikali.
Rais Samia Hassan hasiishie kuwaonya Wizara ya fedha tu, hata Wizara ya mawasiliano imeanza vibaya kwa kukumbatia makampuni ya simu Nchini na kuwasahau raia wanyonge,mashule na vyuo,wizara ya afya nk yaani kundi linalo tumia internet kwa wingi katika masuala kujifunza mambo mengi online pamoja na mawasiliano yanayo simamiwa/endeshwa kwa kupitia apps za whatsapp, Skype etc.

Wanataka tubaki nyuma kimaendeleo kwa kubeba makampuni ya simu yanayo zalisha matrillion ya TSh. kwa mwezi, lakini hapa wanajitia kupoteza revenue wakati wateja wanapo tumia whatssap kuwasiliana kwa njia ya simu,wanacho sahau ni kwamba uwezi kutumia apps hizo bila ya kupitia kwenye internet na internet inakuwa accessed through ununuzi wa vifurushi vya internet hivyo madai ya Makampuni ya simu kwamba wanapata hasara madai hayo ni ulaghai mtupu hazina ukweli wowote, wanapata fahida nyingi wakati wateja wanapo nunua bundles kutoka kwao, hilo Rais aliangalie kwa umakini sana - inaelekea Wizara ya mawasiliano inawajali zaidi makampuni kuliko wanyonge.
 
Naona hoja kubwa ya watu waliokua wananufaika na udhalimu uliokua unafanyiwa wafanyabiashara wamekua wakali baada ya milija yao haramu ya kupata pesa kuzibwa sasa wanaanza na propaganda kua mama atafanya watu wasikusamye kodi, wapi mama kasema hivyo ? Mama anachotaka ni utawala wa sheria, kingine mataga mjue kutesa kwa zamu, mlipokula panatosha,
 
Back
Top Bottom