Rais Samia Suluhu: Kusanyeni kodi kwa kutumia akili, sio nguvu

Rais Samia Suluhu: Kusanyeni kodi kwa kutumia akili, sio nguvu

Nchi imepata raisi
Wakiongoza waislam hali huwa shwari kabisa
 
Naunga mkono hoja binti kiziwi lakini ukweli ni kwamba ukiwaomdoa wafanyakazi wa Umma wengi wote walio baki hakuna anayependa kulipa kodi hapa tanzania!

Hata yakiwekwa mazingira gani hakuna mfanyabishara mkubwa au mdogo atakuwa tayari kuleta haki ya TRA au Halmashauri bila kusukumwa na hilo sio africa pekee ni tatizo pengine la dunia!

Nina kuhakikishia bila nguvu na akili hakuna kodi wala ushuru TRA wataweza kusanya kamwe na hizi ni hadithi!

Wafanya biashara wote target yao ni kutengeneza faida kubwa hata maradufu huku wakitafuta mwanya wa kukwepa kodi!


“CCM mbele kwa mbele”
Hata mimi ilo la kodi Mama naona kachemka.

Target trillion 2 kwa kubembelezana sioni kama itawezekana.
 
Hii ni kauli ya kutokujua,,watu wanakwepa kodi kila siku K'koo,vitu vya laki mbili unapewa risiti ya 65000..usipotumia nguvu,tutakula nyasi humu ndani.
Unachotakiwa kuelewa ni kwamba kwanza watu wapewe elimu ya kudai risiti halali kwa malipo halali. Pia kodi zipunguzwe ili kutanua wigo wa walipaji wengi. Lakini pia tuimarishe exportation sana ila kupata pesa (vyanzo vingine vya mapato kama madini, makaa ya mawe, Mazao nk) lakini pia kuboresha bandari zetu DAR, MTWARA, TANGA ili nchi jirani kama ZAMBIA, MALAWI, CONGO RWANDA NK kupitishia bidhaa zao. UTALII uwe katika malipo ya CHINI sana kwa WATANZANIA ili kuongeza watalii wa ndani. Mfano kuingia mbugani ni BUKU 10 tu au Buku 5 kwa native lkn kwa natives na wageni unasogeza Kidogo. Huku ukiwapa conditions za kutumia bidhaa za ndani kama bia na sigara ili kukuza soko la ndani. YAAN KWA KIFUPI TUNA NJIA NYINGI MNO ZA KUAKILI KULIKO NGUVU.
 
Ulishaanza kuwa utaratibu wa watu kuzulumiana. Wengine wakatumia huo upenyo kama unamdai anakwambia TRA wamefunga Account zangu..

Hapa Mama kafanya jema sana
Mtu asiyetaka kukulipa hakulipi tu. Leo TRA wamefunga kesho atakupa sababu mpya.
 
Mama amenikosha sana.

Kumbe walikuwa wanatumia mabavu hadi kukwapua hela za watu kwenye account zao za benki.

Kama analoongea ndo alilokusudia kulisimamia basi sekta hii ya biashara na uwekezaji itaanza kustawi tena.
Hongera sana Mama.Nafungua tena maduka yangu.
 
Huyu mama nampa miezi 6 tu tunarudi kulekule enzi za JK
Kwa JK ni Makusanyo m700/800, halmashauri zinakusanya pesa zake hazichukuliwi na serkali kuu, miundombinu inajengwa, ajira, kupanda madaraja n.k

Alijitahidi kudhibiti madawa ya kulevya maana ile awamu hili tatizo lilikuwepo, JPM kajitahidi kuliondoa.
Ufisadi awamu zote upo hakuna wa kumcheka mwenzie.
 
Mimi sikubaliani na wewe Mkuu. Wananchi wenye utashi wa kulipa kodi bila kusukumwa ni wengi. Bali kinachokera ni namna TRA wanavyoshughulikia zoezi la kulipa kodi. Hii ikiwa ni pamoja na makadirio ya kodi, maswali wanayoulizwa walipa kodi ni kama wapo kituo cha polisi. Ukimaliza makadirio, Kuna milolongo kibao isiyokuwa na msingi. Unazungushwa kwenye vyumba utadhani uko Hospital. Hivyo, Wananchi wengi kuepuka adha hiyo wanaacha kulipa kodi. Kwa ujumla TRA sio wabunifu wa kupunguza kero za walipa kodi.
Huyo sidhani kama ni mfanyabiashara.
 
Aliyekuwa kinara wa kupora watu ndio huyo kapewa umakamu.

Na kuonyesha kwamba bado ana uchu ameagiza zikusanywe trilioni mbili....hivi zinakusanywa vipi hizo pesa?. kama sio sisi Wanyonge wa huku chini kukamuliwa mapaka tone la mwisho?.

Kati ya mbinu alizokuwa anatumia yeye ndio hayo mabavu na kupora akina Ramadhani Ntuzwe pesa zao zipelekwe HAZINA.

Kuna usemi "Shona Koti kulingana na kitambaa ulichonacho"

Serikali ifanye utafiti kujiridhisha kama Wananchi wake wana huo uwezo wa kulipa Serikalini hizo Trilioni mbili kabla tu ya kutamani zikusanywe.
Wakikuza mzunguko wa fedha ukawa mzuri sana, wakaongeza wigo wa kodi si kubana watu wale wale, wakatengeneza wafanyabiashara wapya, wakabuni mfumo bora wa ukusanyaji kodi mpaka kwa mfagia ofisi, wakatoza kodi kidogo ila kwa kila mtu. Inafika hata T3. Tanzania ina mazingira mazuri sana ya upambanaji.
 
Pia siyo muende kukwapua pesa za watu kwenye A/C kwa nguvu
Mama kawapasulia wote mpaka makamu wake. Katafuteni bilioni 2 lakini msitumie nguvu wala kuwabambikia watu makodi tangia enzi za mababu zao. Kwa utaratibu huu, baada ya mwaka tu watapata mara 2 ya hizo. Hongera Mama, Ila Makamu naye azingatie Mambo ya Mazingira na climate change etc.
 
Lakini huyu msaidizi wake anaongea bila kuelewa muelekeo wa Mh. Rais, yeye ana mwagiza Mwigulu wakusanye trilion mbili kwa mwezi wakati yeye zilimshinda na kuanza kuibia watu.
Mpango bado sana kwenye utendaji.
Alisema mpaka wakifika Desemba wafikie lengo la 2 th
Kwa jinsi nilivyomuelewa ni kama ameagiza waanze kujiwekea malengo.
 
''Kwa upande wa mapato naomba mkaongeze walipa kodi, hii 'trend' mnayoenda nayo si nzuri, mnatumia nguvu sana kuliko akili katika kukusanya mapato, mnaowachukulia vifaa vyao na kufunga akaunti wakitoka hapo wanaenda kufunga biashara wanahamia Nchi ya pili'' - Rais Samia Suluhu

Mama anaongea vizuri huyu.
Anajua shida tulizopitia kutokana nguvu kubwa iliyotumika kutoka kwa mtangulizi wake.
Mwenyezi Mungu amsimamie ili aendelee kututetea
 
Hatukusema haya enzi za ibilisi tukaonekana wachochezi , sio wazalendo , wasaliti , tunatumiwa na mabeberu .View attachment 1740521
Usisahau pia hapa Jf kuna vizabizabina waliokuwa wanaunga mkono kila kitu kilichoagizwa na malaika mkuu, bila kujali athari zake kwa wafanyabiashara.

Usishangae waliounga mkono maagizo ya malaika watakuja kumsapoti mama na kudai ana huruma na watanzania.
 
Back
Top Bottom