Tuna mfumo wa kodi ambao ulibuniwa kipindi Taifa linajenga uchumi wa Kijamaa. Kutumia mfumo huo huo kipindi hiki tukiwa katika mfumo wa Soko huria, ni kama kuingiza "a square peg in a round hole". Tunahitaji kufumua mfumo huu wa kodi na kubuni ambao unafanana na malengo yetu ya kiuchumi kwa sasa.