Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Mheshimiwa Rais anaposema TRA watumie akili ni kwamba wapaswa kubuni njia rafiki za kukusanya kodi ikiwemo njia ya kumruhusu mfanyabiashara alipe kwa awamu endapo atagundulika alikwepa kulipa kodi.
Sheria ya uhujumu uchumi ni kweli yahitaji mabadiliko lakini sheria hii ni dawa ya wahujumu uchumi.
Mtu hawezi kuingiza nchini bidhaa zilokwisha muda wake kisha atake kuuza na kupata faida kubwa.
Kama mteja amegundulika alikuwa akiepa kulipa kodi TRA wapaswa kuandaa utaratibu wa kulipa kwa awamu au "Instalments" mpaka amalize.
Hii ya TRA kuingia kuchungulia akaunti ipo katika nchi nyingi tu na imeruhusiwa kisheria ila pale wanapogundua una fedha za kutosha kwenye akaunti hawachukui bali wanakujulisha halafu mnaandaa utaratibu wa kulipa kwa awamu.
Suala la raisi kusema wizara ya fedha na TRA watumie akili katika kuhakikisha wanakusanya kodi ni pamoja na kuhakikisha kila raia ambae apaswa kulipa kodi yumo kwenye mfumo na analipa kodi.
Pia ukusanyaji kodi kwenye halmashauri zote nchini wapaswa kuwa ni wa kuhakikisha kodi ya maendeleo yalipwa na kila mlipakodi na hakuna wizi unaofanywa ama kupitia mashine za OPS au maofisa wa halmashauri ambao hukusanya kodi na kukimbia na fedha.
Hivyo kila mlipa kodi ni lazima atumie njia rasmi ya muamala kulipa kodi nikimaanisha kwamba lazima TRA iendeshwe kisasa kwa kuwa na mifumo ya kielektroniki yaani automated system ambapo hata wawekezaji wa nje wataridhika na njia hizo rahisi na rafiki za ulipaji kodi.
Mwisho, Wizara ya fedha na TRA wawekeze zaidi kwenye mifumo ya kisasa ya kieletroniki ambapo mashine kama za EFD ni kwa ajili ya utoaji stakabadhi na kuwekeza katika mfumo wa EDS yaani Electronic Data System ambapo shughuli hizi zinakuwa "outsourced" kwa makandarasi wa nje.
Shughuli hizi zikiwa outsourced inakuwa rahisi kwa vijana kupata ajira kupitia makampuni hayo ambayo mengi ni ya nje na pia huweza kuleta teknolojia mpya khasa kampuni kama MphasIS ya Bangarole India ni mojawapo.
Hivyo basi, utozaji kodi aina zote ni lazima uwe ni rafiki ambapo kila mlipa kodi atawajibika bilashuruti na pia elimu zaidi kupitia vipeperushi na matangazo redioni na njia zingine vitasaidia kupanua mfuko wa trillioni 2 na zaidi.