Rais Samia Suluhu: Kusanyeni kodi kwa kutumia akili, sio nguvu

Mama amenikosha sana.

Kumbe walikuwa wanatumia mabavu hadi kukwapua hela za watu kwenye account zao za benki.

Kama analoongea ndo alilokusudia kulisimamia basi sekta hii ya biashara na uwekezaji itaanza kustawi tena.
Bila shaka atakuwa amefanya vyema kabisa.
 
Bi mkubwa hawataki wenye HILI NA LILE....ingawa bado anao wenye walikuwa na HILI NA LILE...
 
Weee mdanganye tuu,
nchi hii ni nani aliye tayari kulipa kodi stahili kwa biashara/ shuguli anayo ifanya labda mfanyakazi tuu through PAYE, Kila mfanya biashara ana wazo la kukwepa kodi ili maximize mapato yake., mwacheni rais akusanye kodi
 
Lakini huyu msaidizi wake anaongea bila kuelewa muelekeo wa Mh. Rais, yeye ana mwagiza Mwigulu wakusanye trilion mbili kwa mwezi wakati yeye zilimshinda na kuanza kuibia watu.
Mpango bado sana kwenye utendaji.
Mpango itabidi abadilike....naona hajamuelewa mama. Anataka kuendelea na utaratibu wa kukusanya kodi bila weledi ambao umeua biashara.

Bahati nzuri mama ni very intelligent,ameliweka vizuri suala hili mapema.
 
Lakini huyu msaidizi wake anaongea bila kuelewa muelekeo wa Mh. Rais, yeye ana mwagiza Mwigulu wakusanye trilion mbili kwa mwezi wakati yeye zilimshinda na kuanza kuibia watu.
Mpango bado sana kwenye utendaji.
Naona ule Uwaziri bado haujamtoka tumpe muda.
 
Ila mama unawachanganya sana Mataga, walitudanganya hakuna mfanyabiashara aliyekimbilia nje??
 
Mpango itabidi abadilike....naona hajamuelewa mama. Anataka kuendelea na utaratibu wa kukusanya kodi bila weledi ambao umeua biashara.

Bahati nzuri mama ni very intelligent,ameliweka vizuri suala hili mapema.
Bado anajiona Waziri, tumpe muda kwanza azoee kiti kipya na majukumu mapya.
 
Mtu anaambiwa eti hii kodi ilitakiwa uwe umekadiriwa na kuilipa mwaka 2016, hivyo lipa sasa!
 
Ukipunguza kodi kwa wazalishaji mfano viwandani au kwenye kampuni za simu wengi watajirusha means wengi watalipa kodi
 

Naunga mkono hoja lakini kwa tanzania hii walipa kodi kwa hiari ni wafanyakazi wa Umma pekee! Walio baki ni lazima nguvu na akili zitumike lasivyo hakuna kodi wanatoa!

Swala la kufunga biashara limeshasemwa sana na kila mtu na kila Rais!
Pia TRA wanabebeshwa lawama za bure bali wao wanafata sheria zilizo wekwa na ndizo zinawapa nguvu!


CCM mbele mbele
 
Naona Mpango anajaribu kutoa matamko kama vile yeye ndo rais.
Anaongelea makusanyo kama kumwambia Mwigullu kuwa mimi niliweza sasa wewe kafanye kama mimi.
Kweli huyu jamaa ni kimeo bado ana matoxin moyoni mwake.
Lakini mama Samia amemcounter kihekima- Nendeni mkatanue wigo wa walipa kodi"
Naamini mh.Mwigullu ameelewa kuwa achukue maelezo ya nani.
 
Mtu anaambiwa eti hii kodi ilitakiwa uwe umekadiriwa na kuilipa mwaka 2016, hivyo lipa sasa!

Ni ajabu sana na unakuta kuna muda au miaka yote walikuwa wanakupa na ‘Tax Clearance’ kwamba upo sawa hesabu zako na malipo yao kwao, lkn wanakuletea mambo ya nyuma sijui penalty hii imetokana na hivi na hivi na ‘Tax Clearance’ walikupa wao basi si wangesubiria umalizane na hilo tatizo muda huo why sasa hivi ndo wanalileta kama penalty na ukiangalia ni hao jamaa pia maalum wa hiyo ‘task force’ ni kuvunjilia mbali hao wabaki wataalam wa kodi huko kwenye ofisi zao siyo kuwa na kundi maalum la kuhakiki mwishoe ni kuua watu kwa pressure tu

Yaani watu hawa hawana uhalisia kabisa wa hali ya biashara zilivyo ktk ground level as long wanapata mishahara yao na njia zao wanazojua kukuza vipato vyao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…