Rais Samia Suluhu: Kusanyeni kodi kwa kutumia akili, sio nguvu

Rais Samia Suluhu: Kusanyeni kodi kwa kutumia akili, sio nguvu

Anaweza hata kuwabambikia kesi za ugaidi yule!! Hana maana kabisa yule jamaa! Namkumbuka sana namna alivyo husishwa kwenye ile kesi ya ugaidi ya kutengeneza iliyomhusu Wlifred Lwakatare.
Hivi kesi iliishaje Mkuu!? Nilihama Tz nikaenda kusiko na network.Ila nimecheka na nilicheka mno kipindi kile.
 
Sisi wananchi wenyewe kulipa kodi bila kusukumwa ni mtihani!! Ukisema leo waje kwa kulemba kwenye kodi aaah hawapati ata bilion 1 kwa mwezi. Wakwepa kodi wengi wanajua kama wanakwepa kodi na wanafanya hivo ili faida ipige maradufu.
Kwahiyo wewe una akili na maono makubwa ya ukusanyaji wa kodi kuliko Mh. SSH?
 
Sisi wananchi wenyewe kulipa kodi bila kusukumwa ni mtihani!! Ukisema leo waje kwa kulemba kwenye kodi aaah hawapati ata bilion 1 kwa mwezi. Wakwepa kodi wengi wanajua kama wanakwepa kodi na wanafanya hivo ili faida ipige maradufu.
Umeona hilo tu?
  • Ujajiuliza kwann kulipa kodi ni had tusukumwe?
  • je umejiuliza hio kodi inaendana na hali halisi ya mapato mtu anayo ingiza?
  • umejiuliza mazingira ya ukusanyaji kodi ni rafiki kwa huyo mlipa kodi?
  • Umejiuliza kuhusu usawa katika kulipa kodi?
 
Mama kasema ana macho malegevu lakini yanaona mbali! Huyu mzenji atawaua jamaa wa kanda ile! Hivi ile ajenda ya kuongeza muda wa kutawala bado ipo?
 
...kweli kabisa hili kodi amenena vema.naona PEPSI wanatoa mabango yote ya kutangaza biashara nchi zima sababu kodi ipo juu
 
Mheshimiwa Rais Mama Samia amemuonya Waziri wa wizara ya Fedha kuacha kutumia nguvu kwenye kukusanya kodi badala yake watumie akili.

Mama Samia ameonya tabia ya Watendaji wa Serikali kutumia nguvu kukusanya kodi, kufungia biashara zao, kunyang'anya fedha kwenye akaunti kisa Sheria inawaruhusu.

Ameongeza kuwa Kitendo hicho kinasababisha wafanyabiashara kufunga biashara zao na kukimbilia nchi Jirani na hatimaye Serikali kukosa mapato.

Safi sana mama naona unaanza kuiga iga mienendo ya yule wa zanzibar kwa sasa hali shwari
 
Mama amenikosha sana.

Kumbe walikuwa wanatumia mabavu hadi kukwapua hela za watu kwenye account zao za benki.

Kama analoongea ndo alilokusudia kulisimamia basi sekta hii ya biashara na uwekezaji itaanza kustawi tena.
Ulishaanza kuwa utaratibu wa watu kuzulumiana. Wengine wakatumia huo upenyo kama unamdai anakwambia TRA wamefunga Account zangu..

Hapa Mama kafanya jema sana
 
Kwakweli rais awaambie tuu...... TRA, BRELA, TIC, HALMASHAURI ni majipu, watumie akili na waache kuhujumu juhudi za serikali na wawekezaji
 
Weee mdanganye tuu,
nchi hii ni nani aliye tayari kulipa kodi stahili kwa biashara/ shuguli anayo ifanya labda mfanyakazi tuu through PAYE, Kila mfanya biashara ana wazo la kukwepa kodi ili maximize mapato yake., mwacheni rais akusanye kodi
Wewe unafanya biashara gani.?unataka kusema Rais anachoongea ni uongo ila wewe Koti la chawa ndy unajua Ukweli? Wengi wenye kuishi kwa vikazi vya wajomba huona mfanyabiashara kama adui...
 
Sisi wananchi wenyewe kulipa kodi bila kusukumwa ni mtihani!! Ukisema leo waje kwa kulemba kwenye kodi aaah hawapati ata bilion 1 kwa mwezi. Wakwepa kodi wengi wanajua kama wanakwepa kodi na wanafanya hivo ili faida ipige maradufu.
Mkuu
Kwa technology ilivyo advance , huwezi kufikiria kukwepa kodi na ukafaulu , wakiamua wanakudaka fast tu,
Tunacholilia watu ni fairness kwenye baadhi ya sheria za kodi , zipo harsh na haziangaliii hali halisi .
 
Mama Samaia Hassan Suluhu anazidi kuthibitisha kuwa, Kwenye uumbaji Mwenyezi Mungu alituumba Wanaume wa Kwanza lakini AKAWAPA WANAWAKE HEKIMA, UPENDO NA NIDHAMU KAMA UPENDELEO KWAO NA KUTUTOFAUTISHA NA SISI (wanaume)..
wanaume sisi tukipata madaraka tunakuwa jeuri na kusababisha Mabalaa na mitafaruku
ndio maana wakasema hakuna kama MAMA
 
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Sasa Hivi Atatuvusha
 
Sisi wananchi wenyewe kulipa kodi bila kusukumwa ni mtihani!! Ukisema leo waje kwa kulemba kwenye kodi aaah hawapati ata bilion 1 kwa mwezi. Wakwepa kodi wengi wanajua kama wanakwepa kodi na wanafanya hivo ili faida ipige maradufu.
Umeongea vizuri, nimeshtuka kidogo alivyosema hatakama sheria inaruhusu.
sababu kama kunawanao kwepa nasheria inaruhusu kuchukua fedha kwaajili ya malipo ya kodi then it's very confuzd.
 
Mkuu unamaanisha kutumia nguvu ni bora zaid ili tulipe kodi? Kikubwa ni kujenga taasisi imara na mfumo thabiti na wananchi wapewe elimu na uwajibikaji wa kulipa kodi. Akili 75% nguvu 25%
Uliza kodi ya nyumba km inalipwa kwa wakati
 
Back
Top Bottom