Kipindi cha Rais samia cha sasa kuna mambo mengi yamekua hayaendi sawa Kupanda kwa vitu bei ila kwenye suala la kuruhusu maandamano ameonyesha busara na hekima ya hali ya juu sana kitu ambacho marais waliotangulia walikosa
Kipindi cha magufuli kuna dada wa kitanzania mpare sahivi ni billionaire kwa habari za umbeya alitishia maandamano nguvu ambazo magufuli alizitumia zilikua ni kubwa sana mixer ndege za kivita zilikua zinapita kwenye makazi ya watu alionyesha kutokua mstaarabu, kukosa busara na hekima kwa kiwango cha juu sana
Maandamano ya 2002 kulikua na matumizi ya nguvu makubwa mpaka lipumba amavunjwa mkono na watu kadhaa kuuliwa baadae mkapa alisema lile tukio analijutia sana ila anasema alishauriwa vibaya
Mnyonge mnyongeni ila kwenye hili Rais samia anahitaji pongezi sana