Pre GE2025 Rais Samia Suluhu kwenye hili la kuruhusu maandamano anahitaji sana pongezi

Pre GE2025 Rais Samia Suluhu kwenye hili la kuruhusu maandamano anahitaji sana pongezi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
B42BE557-540E-4E64-A9C5-265628D486A2.jpeg


Huyo raisi mwenyewe hata ana habari
basi nini kinaendelea Tanzania, muda huu yupo zake Indonesia huko.
 
Sema ameshindwa kuzuia maandamano baada ya Mbowe kumzidi ujanja Kwa kushirikisha UN na mabalozi wa USA na Uingereza.

Ikiwa alikuwa na Nia njema kuruhusu maandamano, why wanajeshi hawakujitikeza yalipotokea mafuriko, waje kufanya usafi siku ya maandamano ya CHADEMA?

Huna HOJA.
Mkuu Rais wa nchi hii hashindwi kitu. Mm nadhani rangi kamili itaonekana siku si nyingi
 
Rais Samia tayari ameingia katika Kitabu Cha KUMBUKUMBU, Marais wa kiume wote waliogopa maandamano, mama ameonyesha moyo wa mama mlezi. Aliyepita alisema uchaguzi ukiisha basi hakuna mikutano mpaka miaka 5 ipite, mama mlezi ameruhusu. Aliyepita alisema mwanafunzi anayezaa akiwa shule asirudi shuleni, Mama mlezi ameruhusu
Aliyepita alisema mkurugenzi ambaye eneo lake atachaguliwa mpinzani Hana kazi, hili Sasa mama mlezi aruhusu sanduku la kura lichague aliyechaguliwa na Wananchi. HONGERA sana mama mlezi umeingia katika Kitabu Cha KUMBUKUMBU.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
He was a sadist.
 
Kipindi cha Rais samia cha sasa kuna mambo mengi yamekua hayaendi sawa Kupanda kwa vitu bei ila kwenye suala la kuruhusu maandamano ameonyesha busara na hekima ya hali ya juu sana kitu ambacho marais waliotangulia walikosa

Kipindi cha magufuli kuna dada wa kitanzania mpare sahivi ni billionaire kwa habari za umbeya alitishia maandamano nguvu ambazo magufuli alizitumia zilikua ni kubwa sana mixer ndege za kivita zilikua zinapita kwenye makazi ya watu alionyesha kutokua mstaarabu, kukosa busara na hekima kwa kiwango cha juu sana

Maandamano ya 2002 kulikua na matumizi ya nguvu makubwa mpaka lipumba amavunjwa mkono na watu kadhaa kuuliwa baadae mkapa alisema lile tukio analijutia sana ila anasema alishauriwa vibaya

Mnyonge mnyongeni ila kwenye hili Rais samia anahitaji pongezi sana

..Nadhani pongezi ziende kwa walioandaa maandamano ambao hawakutishwa na yaliyowapata wenzao huko nyuma, na hawakusikiliza kejeli na vitisho ilivyokuwa vikitolewa na magenge yanayomuunga mkono Rais Samia.
 
Piga picha ingekua kipindi cha magufuli au mkapa alafu ndo kuna haya maandamano nakuhakikishia sahivi ingekua damu imeshamwagika

..Mbowe na wenzake wanastahili pongezi kubwa sana.

..Pamoja na historia ya serikali za Ccm kumwaga damu kunapotokea maandamano wao walishikilia msimamo wao wa kudai HAKI ya kikatiba ya kuandamana.
 
Tanzania rais yupo juu ya katiba kama ulikua hujui
Ndo maana anaweza akazuia maandamano na hakuna wa kumfanya chochote

Rais ana hiari aifuate katiba au asipoifuate sababu hata asipoifuata huna cha kumfanya katiba ya Tanzania inategemea sana busara za aliyeko madarakani
Vijana hawa elimu ndo maana hata hili nalo watakataa.
 
..Mbowe na wenzake wanastahili pongezi kubwa sana.

..Pamoja na historia ya serikali za Ccm kumwaga damu kunapotokea maandamano wao walishikilia msimamo wao wa kudai HAKI ya kikatiba ya kuandamana.
Mimi nadhani pongezi wangepewa Jeshi la polisi kwa kumhakikishia raisi na wasaidizi wake kwamba watayadhibiti maandamano.

Kamanda Murilo amesoma na safari hii ametumia elimu yake ipasavyo na si kuiweka kapuni.
 
Vipi kuhusu jua Kuchomoza tumpongeze nani ?

Badala ya kutumia muda wetu ku-criticize vitu ambavyo haviendi sawa kutokana na sera na utendaji mbovu (mgao wa giza, mfumuko wa bei, kukosekana ujira wa kutosha kwa watu n.k.) tunapoteza muda kupoteza vitu ambavyo hata wala hana Haki kuvizuia.., vitu ambavyo vipo kisheria..., Kwahio mtu apongezwe kwa kufuata Sheria ?!!! Kweli !!!!

Na wewe tukupongeze kwa kupongeza ?!!!!
 
Hivi nyie mnakili ndio maana hatuwezi kuendelea hivi raisi aruhusu maandamano kama Nani katiba ndio inaruhusu sio rais
 
Mkuu Rais wa nchi hii hashindwi kitu. Mm nadhani rangi kamili itaonekana siku si nyingi
Mbona ameshindwa kudhibiti wizi wa raslimali za nchi?

Mbona kushindwa kuhakikisha Bei ya sukari isizidi 2500 per kg?

Kushindwa ni kushindwa tu!!
 
Issue ya wanajeshi ni RC tu alikurupuka, unadhani SSH angeamua kukaza asingeweza ?
Sisi chadema hatuna jema
Tumemaliza maandamano ingawa hayakunoga kama tulivyotarajia sasa tumeacha tumegeukia kwanin mama karuhusu
Narudisha kadi mim ohoo shar lennu
 
Katika jambo lililomwinua mama samia ni hili la kuruhusu maandamano big up mama samia kiuhalisia amezidi maraisi wote waliopita namuona mama samia ni mwema tatizo ni wanaomzunguka huko ccm sio watu wema mama Leo umeonyesha Kwa jamii ya watanzania anaweza kuleta mabadiliko ukiacha doa la Dp world kura zingepigwa Leo ungeshinda uraisi umeonyesha Utu mama Mungu akulinde na azidi kukupigania
 
Back
Top Bottom