Rais Samia Suluhu: Mkikidhi vigezo, Chato tutaifanya kuwa Mkoa

Rais Samia Suluhu: Mkikidhi vigezo, Chato tutaifanya kuwa Mkoa

Kushabikia chato kuwa lazima iwe mkoa wakati kwako hakujatengamaa huo ni umama.Sisi tusubiri watakachotangaza inshallah
 
Hakika Rais Mama Samia kaonesha kuheshimu Mamlaka.

Ombi la wana Chato kuomba kuwa Mkoa kalikabidhi kwa mamlaka husika.

"Mkikidhi vigezo tutaipa Chato kuwa Mkoa" Rais Mama Samia Suluhu
Si mlikuwa mnamchukulia poa!!!.
 
Uko sahihi...kwa mujibu wa Rais Chato itakuwa mkoa ....Kama vigezo havitoshelezi kwa Sasa wataelekezwa namna ya kufanya kukamilisha vigezo hivyo...na tayari vigezo vingi tayari...hospitali ya rufaa inakamilishwa, uwanja wa Ndege inakamilishwa ambao hata Boeing zitatua, vyuo, viwanda, miundo mbinu Yaani barabara tayari ni za lami, hoteli nyita tatu inajengwa...na kadhalika na kadhalika...miaka mitatu ijayo Chato itakuwa mkoa...
Wilaya zake ni zipi ?
 
Kaondoka na uwanja wa ndege unaenda kuwa pori la kulishia mifugo,
Wabongo bana. Utazani hawataki maendeleo.

Aliondoka pinda wakasema kama wewe.

Sasa hivi kule mpanda ndege zinatua.

Hapo chato airport patanoga na hautaamini macho yako
 
Angekuepo mwenyewe angesema leo natangaza Chato kua mkoa na viongozi nitawateua.
Ndio sifa ya Hayati,alikua si mpenda kuchelewesha mambo,Chato lazima iwe mkoa

kwani mfano ikatangazwa kuwa mkoa sasa hivi na hivyo vigezo "vikafata nyuma" shida iko wapi?

tatizo katika process za kutimiza vigezo (ndipo wapigaji hutumia huo mwanya kula pesa) ndio maana

Hayati Dr.JPM alitambua hilo na akawaa analikwepa, Akawa anatoa solution Papo kwa Hapo yanapotokea

mambo ambayo yapo katika uwezo wake (RAIS) Rais n mtu wa ORDER sio REQUEST dear,ndio maana ktk utendaji

IDEA za RAIS ni MAAGIZO KAMILI, Chato inaenda kuwa mkoa,mama hajatamka ila inakuwa tena very soon,kwanini?

kwasababu RAIS si mtu wa kuomba omba kuuliza ilikuaje itafanyikaje,Jambo kama linawezekana ni Anatamka na LIWE,short n clear.
 
Back
Top Bottom