Kuna tatizo lolote chato ikiwa mkoa?
Tatizo sio Chato kama Chato tatizo lipo wanasiasa wanapo endelea kuigawa nchi na kutengeneza mikoa,majimbo,wilaya,harafu wakituaminisha kwamba hicho kitendo kinaleta maendeleo,
Mwananchi wa kawaida anataka Maji,shule,afya,Usalama,ajira,chakula,badala ya kufikiria kuigawa nchi na kuongeza maeneo ya kiutawala,bora wangesema tutajenga mradi wa kilimo Cha umwagiliaji mkubwa kuliko yote Afrika,wa miwa,Mpunga,au kiwanda Cha nyama,maziwa,au kuweka plant ya kua assemble magari,wao wanataka kuifanya Chato iwe mkoa,tupate RC,RAC,RPC,na mavyeo meeengi yasio na tija,hapa hatuleti maendeleo,tunaongeza Wage bill kwa serikali,Mkoa sio kiwanda,hatuzalishi,ni utawala tu,hauongezi panadol Wala asprini,
Kama ni huduma za ardhi,jenga ofisi ya kanda,weka maofisa kwenye ofisi ya DC,
Badala ya kuleta RC,na kumjengea Ofisi,bora kijengwe chuo kikuu Cha sayansi na tekinolojia,silicon valley iwe Chato,au kuna ubaya gani kukawa na Kariakoo nyingine Chato,lakini sio limkoa,
Hakukuwa na Tija kuigawa Arusha,kutengeneza Manyara,hakuna tija kuwa na Katavi,simiyu,Dar ilikuwa na wilaya tatu tu,Kinondoni,Ilala,Temeke,leo zipo tano,hata kama watu wameongezeka,ukubwa wa Dar upo pale pale kijiografia,kama ni huduma huitaji watumishi wengi,ni vitendea kazi tu,ongeza mashule,hospitari,vituo vya polisi.
Madakitari.sio huu upuuzi wa kuongeza watawala.