Automata
JF-Expert Member
- Mar 3, 2015
- 3,414
- 4,794
Zile ni chai za yule mzee na wenzake wanapokaa vijiweniKumekuwa na tetesi za muda mrefu tangu Mh. Magufuli aingie madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 2015 kwamba alikuwa na mpango kabambe wa kuifanya wilaya ya Chato kuwa mkoa. Habari hiyo imekuwa ikikanushwa kwa hisia kali na wafuasi wa CCM ndani ya JF kuonesha kwamba wanaosema hivyo ni wazushi na wana nia mbaya ya kuonesha labda MH. Magufuli alikuwa anajipendelea ukizingatia udogo wa mji na uchanga wa wilaya ya Chato.
Lakini mtu aliyeandaliwa kuwasilisha salaam za Wanachato siku ya mazishe, Mzee maarufu pale Chato aitwaye Magambo ameweka wazi kwamba marehemu katika uhai wake aliwaahidi kuigeuza Chato kuwa mkoa kabla ya 2025.
Akijibu hoja hiyo Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kulifanyia kazi kama litakidhi vigezo vilivyowekwa. Lakini facial expression yake imeonesha mshitumko juu ya jambo hili kwa kuliona kama jipya. Baadhi ya maneno aliyotumia ni "Nasikia mmeshaanza mchakato". Jambo jema Kama hili la kuliongezea thamani eneo mojawapo katika nchi hii halikupaswa kuwa siri hata kwa watu muhimu na wawezeshaji. Tulifichwa mchakato huu ili iweje? Yaani walitegemea siku moja tuamke na kukuta Chato ni mkoa ghafla?
Tabia hii ya kuweka siri vitu vinavyopaswa kuwa wazi haileti Afya kwa Utangamano wa nchi yetu. Mh. Samia asikubali kuendelea na utaratibu wa usiri usio wa lazima unaiweza kuibua fikra za upendeleo.