Rais Samia Suluhu: Mkikidhi vigezo, Chato tutaifanya kuwa Mkoa

Rais Samia Suluhu: Mkikidhi vigezo, Chato tutaifanya kuwa Mkoa

Angekuwa fulani angejibu hivi
"Kuanzia leo Chato ni Mkoa tayari"
 
Mama amekubali, amesema hata kama wataona vigezo havijakidhi basi watawaelekeza ili vigezo vikidhi

Ndio nimeanza kumuona huyu mama hamna kitu

Basi Butiama, Mkuranga, Bagamoyo, Masasi nazo zingefanywa mkoa basi kwa kuwa nazo zimetoa viongozi waliofanya makubwa tu

Unaipa chato kuwa mkoa wakati kuna mikoa mikubwa kama Morogoro haijagawanywa
Kwenye msiba kunakua na ahadi nyingi sana suhiri watu watawanyike sasa. Danadana kibao..

Mama atakua na vipaombele vyake so sidhan kama hicho kitakua kimojawapo
 
Hapo Kagera tunamegwa tena ....
Mkuu, ndio ulikuwa mpago wenyewe - kumega sehemu ya Mkoa wa Kagera specifically Ngara may be part ya Karagwe na Kasulu - usifikiri Burigi ilikuwa inapigiwa debe as if it belongs to Chato bila sababu. Mpango huo nilikuwa siuingi mkono hata kidogo, hasa uporaji wa Ziwa Burigi na kulibatiza Chato /Burigi wakati ukweli ni kwamba Ziwa hilo lipo Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera.
 
Mama amekubali, amesema hata kama wataona vigezo havijakidhi basi watawaelekeza ili vigezo vikidhi

Ndio nimeanza kumuona huyu mama hamna kitu

Basi Butiama, Mkuranga, Bagamoyo, Masasi nazo zingefanywa mkoa basi kwa kuwa nazo zimetoa viongozi waliofanya makubwa tu

Unaipa chato kuwa mkoa wakati kuna mikoa mikubwa kama Morogoro haijagawanywa
Umemsikia au umehadithiwa?? Kwa Kauli ya Rais Chato haiwezi kuwa Mkoa kwa maana haiwezi kidhi vigezo vya kuwa mkoa.
 
Ikiwa mkoa,itasaidia nini?itaongeza kipato kwa wananchi?itaongeza ajira?zaidi itaongeza gharama na watumishi tu,RC,DC,RAC ambao hawazalishi kitu zaidi ya kula mishahara tu,
Bora wangesema tujenge kiwanda,Mi Afrika bwana shida sana.inataka mkoa,mie kijana wa bodaboda itanisaidia kwa lipi?
Mtu mmoja aniambie Mara ya mwisho kusikia USA,au UK imeongeza mkoa au wilaya,au jimbo,lini?
Watawala wetu huwa wanafurahia sana ujinga wetu.
Panaitwa mkoa hakuna vitega uchumi, bora tu na wao wapo mkoani.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Kaondoka na uwanja wa ndege unaenda kuwa pori la kulishia mifugo
Haya mawazo ya kijinga tu mnadhani dhahabu na mbuga za wanyama vinavyochangia mikoa mingine isiyo na chocote nayo ameondoka navyo ukiachia akili na nguvu ya wana Chato? Wivu mwingine wa kipumbavu.
 
Kwenye kuomboleza ndo kauli zake...subiri msiba uishe tunarudi kwenye vipaombele vya nchi..

Unafikiri hosptal ya Rufaa chato itapata bajet kama zilivyo hosptal za Rufaa?
 
Ila chato ni kuzuri
Mkazi wa Chato anavuta Oxygen nzuri kuliko mkazi wa Masaki
 
Kumekuwa na tetesi za muda mrefu tangu Mh. Magufuli aingie madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 2015 kwamba alikuwa na mpango kabambe wa kuifanya wilaya ya Chato kuwa mkoa. Habari hiyo imekuwa ikikanushwa kwa hisia kali na wafuasi wa CCM ndani ya JF kuonesha kwamba wanaosema hivyo ni wazushi na wana nia mbaya ya kuonesha labda MH. Magufuli alikuwa anajipendelea ukizingatia udogo wa mji na uchanga wa wilaya ya Chato.
Lakini mtu aliyeandaliwa kuwasilisha salaam za Wanachato siku ya mazishe, Mzee maarufu pale Chato aitwaye Magambo ameweka wazi kwamba marehemu katika uhai wake aliwaahidi kuigeuza Chato kuwa mkoa kabla ya 2025.
Akijibu hoja hiyo Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kulifanyia kazi kama litakidhi vigezo vilivyowekwa. Lakini facial expression yake imeonesha mshitumko juu ya jambo hili kwa kuliona kama jipya. Baadhi ya maneno aliyotumia ni "Nasikia mmeshaanza mchakato". Jambo jema Kama hili la kuliongezea thamani eneo mojawapo katika nchi hii halikupaswa kuwa siri hata kwa watu muhimu na wawezeshaji. Tulifichwa mchakato huu ili iweje? Yaani walitegemea siku moja tuamke na kukuta Chato ni mkoa ghafla?
Tabia hii ya kuweka siri vitu vinavyopaswa kuwa wazi haileti Afya kwa Utangamano wa nchi yetu. Mh. Samia asikubali kuendelea na utaratibu wa usiri usio wa lazima unaiweza kuibua fikra za upendeleo.
Kuna tatizo lolote chato ikiwa mkoa?
 
Wilaya tajwa hapo juu zinaunganishwa na mbuga ya Burigi-Chato. Kwa ukubwa wake, zinatosha kuwa mkoa. Mkoa huu utakuwa na kila vigezo vya kuwa mkoa kwa vile una idadi ya kutosha ya watu, eneo, na kila sababu ya kuwa mkoa hata pasina kuwa ndiko alikozaliwa Magufuli.n Rais Samia amesema ataufanya mkoa kama utakidhi vigezo. Hapo nimetaja vichache. Je, wewe unashaurije?
 
Wilaya tajwa hapo juu zinaunganishwa na mbuga ya Burigi-Chato. Kwa ukubwa wake, zinatosha kuwa mkoa. Mkoa huu utakuwa na kila vigezo vya kuwa mkoa kwa vile una idadi ya kutosha ya watu, eneo, na kila sababu ya kuwa mkoa hata pasina kuwa ndiko alikozaliwa Magufuli.n Rais Samia amesema ataufanya mkoa kama utakidhi vigezo. Hapo nimetaja vichache. Je wewe unashaurije?
Na kama hautakidhi atawapa muongozo jinsi gani wataweza lupata vigezo.
 
Umemsikia au umehadithiwa?? Kwa Kauli ya Rais Chato haiwezi kuwa Mkoa kwa maana haiwezi kidhi vigezo vya kuwa mkoa.
Duh...aisee...kazi mnayo...wapotoshaji mko wengi aisee..duh...Yaani hata aibu huna....Rais hajasema hivyo...amesema mchakato umeanza na Kama vigezo havitoshi wataelekeza namna ya kufanya kukamilisha vigezo ili Chato iwe mkoa kumuenzi JPM...umesikia wewe .mpotoshaji?
 
Back
Top Bottom