Rais Samia Suluhu: Mkikidhi vigezo, Chato tutaifanya kuwa Mkoa

Rais Samia Suluhu: Mkikidhi vigezo, Chato tutaifanya kuwa Mkoa

Mama amekubali, amesema hata kama wataona vigezo havijakidhi basi watawaelekeza ili vigezo vikidhi

Ndio nimeanza kumuona huyu mama hamna kitu

Basi Butiama, Mkuranga, Bagamoyo, Masasi nazo zingefanywa mkoa basi kwa kuwa nazo zimetoa viongozi waliofanya makubwa tu

Unaipa chato kuwa mkoa wakati kuna mikoa mikubwa kama Morogoro haijagawanywa
Dah ikiwa hivyo kufikia 2050 Tz itakuwa na mikoa 75!
 
Kukataa sio lazima useme hapana.... Wala kukubali si lazima useme ndio....

Kuelekezwa kama hamna vigezo ni kupewa sababu za kukataliwa

Kupewa sababu inamaana hamna vigezo.
 
Zingekuwa Enzi hizo... Hapo hapo chato ingetangazwa mkoa na kutangazwa mkuu wa mkoa
 
Itakua unasikiliza Lisu Redio Fm ila kama umemsikiliza rais, mipango ya chato iko pale pale.
Hamna cha chato wewe ulitaka asemeje wakati mwili wa bos wake bado haujazikwa ngojea azikwe akalie kiti aone cha moto ndo utajua hujui, yaan huku wanalia ajira, huku wanalia maafa huku korona akumbuke kujenga uwanja wa mpira chato mh nicheke kidogo hiiiiiiiiiii
 
Wilaya tajwa hapo juu zinaunganishwa na mbuga ya Burigi-Chato. Kwa ukubwa wake, zinatosha kuwa mkoa. Mkoa huu utakuwa na kila vigezo vya kuwa mkoa kwa vile una idadi ya kutosha ya watu, eneo, na kila sababu ya kuwa mkoa hata pasina kuwa ndiko alikozaliwa Magufuli.n Rais Samia amesema ataufanya mkoa kama utakidhi vigezo. Hapo nimetaja vichache. Je wewe unashaurije?
Mkuu, kama kuna wilaya zinahitajika kuifanya Chato kukidhi vigezo vya kuwa mkoa, kwa nini isiwe kwamba Chato ndiyo iende iunganishwe na hizo wilaya halafu moja ya hizo wilaya zingine ndiyo iwe mkoa?

Kwanza inatoa picha gani mzee wa Chato anajua mipango mikubwa ya nchi kama hiyo huku aliyekuwa Makamu wa Rais hakuwa na habari nayo? Kuna uzi nauandaa, embu ngoja wazike kwanza.
 
Ukikidhi vigezo alisikika raisi. Shida ni vigezo si jambo lingine. Ukishakidhi vigezo kwann usiwe mkoa?
Na hivyo vigezo ndio ngumu kufikiwa! Mwanza iligawanywa ukapatikana mkoa wa Geita, sasa Geita nayo igawanywe upatikane mkoa wa Chato! Kipi cha zaidi huku? Kule Moro kuna wilaya ili uifikie unatumia masaa karibu 16 kwa nini wasifikirie kuugawa mkoa kama huo!?
 
Na hivyo vigezo ndio ngumu kufikiwa! Mwanza iligawanywa ukapatikana mkoa wa Geita, sasa Geita nayo igawanywe upatikane mkoa wa Chato! Kipi cha zaidi huku? Kule Moro kuna wilaya ili uifikie unatumia masaa karibu 16 kwa nini wasifikirie kuugawa mkoa kama huo!?
Kazi ipo
 
Tatizo sio Chato kama Chato tatizo lipo wanasiasa wanapo endelea kuigawa nchi na kutengeneza mikoa,majimbo,wilaya,harafu wakituaminisha kwamba hicho kitendo kinaleta maendeleo,
Mwananchi wa kawaida anataka Maji,shule,afya,Usalama,ajira,chakula,badala ya kufikiria kuigawa nchi na kuongeza maeneo ya kiutawala,bora wangesema tutajenga mradi wa kilimo Cha umwagiliaji mkubwa kuliko yote Afrika,wa miwa,Mpunga,au kiwanda Cha nyama,maziwa,au kuweka plant ya kua assemble magari,wao wanataka kuifanya Chato iwe mkoa,tupate RC,RAC,RPC,na mavyeo meeengi yasio na tija,hapa hatuleti maendeleo,tunaongeza Wage bill kwa serikali,Mkoa sio kiwanda,hatuzalishi,ni utawala tu,hauongezi panadol Wala asprini,
Kama ni huduma za ardhi,jenga ofisi ya kanda,weka maofisa kwenye ofisi ya DC,
Badala ya kuleta RC,na kumjengea Ofisi,bora kijengwe chuo kikuu Cha sayansi na tekinolojia,silicon valley iwe Chato,au kuna ubaya gani kukawa na Kariakoo nyingine Chato,lakini sio limkoa,
Hakukuwa na Tija kuigawa Arusha,kutengeneza Manyara,hakuna tija kuwa na Katavi,simiyu,Dar ilikuwa na wilaya tatu tu,Kinondoni,Ilala,Temeke,leo zipo tano,hata kama watu wameongezeka,ukubwa wa Dar upo pale pale kijiografia,kama ni huduma huitaji watumishi wengi,ni vitendea kazi tu,ongeza mashule,hospitari,vituo vya polisi.
Madakitari.sio huu upuuzi wa kuongeza watawala.
We jamaa una point sana kwenye hili. Mimi mwenyewe sielewagi sababu za kugawa mikoa.

Wanachohitaji ni kuboresha huduma za jamii, kugawa mikoa hakuleti ufanisi wowote zaidi ya kuongeza gharama za serikali. Tena ukizingatia hatuna majimbo, haya maamuzi hayana maana.
 
Mama amekubali, amesema hata kama wataona vigezo havijakidhi basi watawaelekeza ili vigezo vikidhi

Ndio nimeanza kumuona huyu mama hamna kitu

Basi Butiama, Mkuranga, Bagamoyo, Masasi nazo zingefanywa mkoa basi kwa kuwa nazo zimetoa viongozi waliofanya makubwa tu

Unaipa chato kuwa mkoa wakati kuna mikoa mikubwa kama Morogoro haijagawanywa
Andamana Mkuu
 
Mama amekubali, amesema hata kama wataona vigezo havijakidhi basi watawaelekeza ili vigezo vikidhi....
Kuna wimbo wa twanga pepeta unaimba, "Chuki binafsi haifai yooo... Tuiacheni jamani italeta tafrani"
 
Back
Top Bottom