Rais Samia Suluhu piga chini daraja la Kigongo - Busisi haijalishi lilipofikia

Rais Samia Suluhu piga chini daraja la Kigongo - Busisi haijalishi lilipofikia

Ndio maana wengine mlilazimika kukimbia nchi kipindi mzee wetu bado yuko hai,hivi hujui mamilioni ya watu na tani za mizigo zitakazopita juu ya daraja hill,kati ya miradi ya maana kabisa kutekelezwa na hayati Magufuli ni mradi wa hili daraja
 
Kiuchumi hilo Daraja ni muhimu sana maana linaunganisha barabara kuu ya kitaifa tena lilichelewa kujengwa hapo.
Lingekuwa linaunganisha wilaya kwa wilaya tungesema tusubiri kidogo lakini hilo ni Kitaifa acha liendelee tu kujengwa..!
 
Ungeelezea umuhimu wake kwani wengi hawajafika huko ili wajue. Ni suala la mjadala tu. Otherwise na wewe utakuwa unafikiri kwa kutumia hicho hicho kiungo ulichosema.
Hilo daraja ni kiungo katika mikoa ya magharibi na kanda ya ziwa,na nchi Rwanda, Burundi, Uganda hata Kenya
 
death sio punishment, ufanye mema ufanye mabaya utakufa tu dogo
Rejea vitabu vitakatifu, kuna nyakati kifo kinaletwa kwa watu fulani fulani kama adhabu. Na pia adhabu hiyo inakuwa endelevu huko walipofikia kwenye maziwa ya moto.
 
Bora limaliziwe tu, kuachia katikati ni hasara

Baada ya hapo kanda ya ziwa wasipewe mradi mwingine utakao gharimu pesa nyingi
Hilo daraja haliwasaidii watu wa kanda ya ziwa tu, wanaovuka hapo wanaenda hadi Rwanda, Burundi, Uganda hata Congo, lakini pia ufanyaji wa biashara utakuwa wa haraka na rahisi badala ya mtu kukaa pale masaa kadhaa anasubiri ferry imvushe watu watakuwa wanapita tu bila kikwazo
 
Jibu kimantiki, yaani ungeelezea umuhimu mkubwa wa kujengwa kwa daraja hilo na sio kusema sijui ndio daraja kubwa sijui la kwanza iyo sio mantiki,, elezea kimanufaa.
 
Watanzania ni wapumbavu sana sometimes. Hivi kuna faida gani ya kupinga aliokuwa anafanya hayati,for the welfare of the society?

Hivi mtu anayebana pesa kwa ajili ya maendeleo ya jamii kwa ujumla na yule anaehujumu pesa kwa ajili ya kujilimbikizia maghorofa na mali kila kona ya jiji kwa maslahi yake binafsi yupi ni mshenzi?
Unafikiri watakuelewa..waafrika akili zetu fupi kama nywele...wanataka ufisadi urudi..pesa ziwe za kijanja janja..maisha holela as if hao wazungu waliendelea hivyo..hawataki visionary leaders...wanataka viongozi wa kukwapua pesa BOT kwenye sandarusi na kupeleka nje ya nchi wafaidi wao na vizazi vyao.
 
Hapa ndio nami aliponiumiza huyu mzee wetu, wasukuma wote niliosoma nao wameajiriwa wakati Mimi naendelea kuzulura tu na baasha ya kaki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe ndio chuki yako inapoanzia, kwahiyo daraja lisiendelezwe kwa sababu wewe unazulura na bahasha?
Halafu Eng. ulishawahi hata kupita hapo kigongo ukajua baada ya kuvuka hiyo barabara inaenda hadi wapi? Acheni chuki zisizokuwa na maana
 
Daraja la Kigogo Busisi ni halina maana yoyote ile. Matumizi mabovu mno ya fedha ambayo yangeelekezwa pengine.

Nakusihi Rais Samia Suluhu. Piga chini huu mzigo. Hakuna fedha zinazotolewa kama takrima. Eti kisa sijui kina fulani wanatokea hapo ndiyo iwe kigezo. Piga chini mama.

Lingine kwenye taasisi karibu zote za umma angalia sana viongozi wake. Kuna kigezo kimetumika kuwaweka pale. Kwa sasa nikupe muda ufanye kazi huku nikikuangalia kwa umakini mkubwa.
Eti nikikuangalia kwa umakini mkubwa........pumbavu sana, wewe kama nani? Unaongea kama una mamlaka wakati we kidampa tu.
 
Kumbe ndio chuki yako inapoanzia, kwahiyo daraja lisiendelezwe kwa sababu wewe unazulura na bahasha?
Halafu Eng. ulishawahi hata kupita hapo kigongo ukajua baada ya kuvuka hiyo barabara inaenda hadi wapi? Acheni chuki zisizokuwa na maana
Tunahitaji equal distribution of our resources bila kuangalia dini, kabila, kanda au ukanda gani una natural resources nyingi, hii nchi ni ya wote.
Unaweza fanya mambo mengi mazuri lakini jambo moja tu linaweza alibu taswira yako katika umma wa watu wengine.
Hii sio chuki ndugu tunarekebishana tulipokosea. Huu ubaguzi wa wazi haifai.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada ameleta maoni yake bila kuyafanyia utafiti wa kutosha.
Mana miradi mikubwa ya Madaraja ,barabara , viwanja vya ndege ,umeme, bandari na maji ni miradi ya kitaifa.

Ni kweli kuwa kuna maeneo yamesahauliwa tangu awamu ya kwanza ya mkoloni mpaka sasa.
Sijajua ni kwa nini mikoa ya Pwani imesahauliwa sana.
NILIFIKA Tanga nikashangaa sana kua ule mji ni JIJI , hata barabara zake ni zile za mkoloni. Viwanda vimekufa yamebaki magofu.Jiji lenye bandari linapotea. Tanga ni mkoa wenye utajiri mkubwa wa ardhi yenye madini, rutuba, misitu,maji, gesi ,wanyama, fukwe n.k lakini hakuna mikakati ya kitaifa ya kupaendeleza.
Tatizo hilo linaonekana Lindi,Mtwara, Ruvuma, Rukwa ,Katavi ,Singida,Arusha wilaya za vijijini, Mara, Manyara. Huko pote kunahitaji maendeleo ya barabara na majengo ya shule yenye ubora.
Mfano ilihitajika jambo la kwanza kwa mikoa yote kuwa na Barabara za lami kufika Dodoma makao makuu ya serikali ya Tanganyika. Yaani iwe ni uhakika wa mtu kutoka Tanga ,kufika Dodoma ndani ya masaa matano tu, kutoka Kilimanjaro ama kupitia Arusha au Kiteto au Handeni na kufika Dodoma kwa muda mfupi, Barabara nzuri kutola Songea mpaka Dodoma bila kuzunguka sana mpaka Dsm au mbeya na kufika Dodoma, kutoka Rukwa kuunganishwa na Mbeya na hatomaye Dodoma, Kutoka Mara kupita serengeti Loliondo Arusha na kuingia Dodoma. Hii ilitakiwa ifanyike kwa haraka zaidi na ionekane ikifangika usiku na mchana . Reli ni muhimu pia ikajengwa lakini haina watumiaji wengi kama barabara.
Kwa hiyo miradi mikubwa kupelekwa Ukanda mmoja ni jambo mahususi lakini kama lengo halikuwa kuigawa nchi vipande viwili au kujenga himaya fulani ili kutawala himaya nyingine kimabavu basi nadhani miradi yote nchini ni muhimu alimradi iwe inapata baraka za Bunge huru linalochambua mambo kwa kina.
 
Rejea vitabu vitakatifu, kuna nyakati kifo kinaletwa kwa watu fulani fulani kama adhabu. Na pia adhabu hiyo inakuwa endelevu huko walipofikia kwenye maziwa ya moto.

the fact that everyone will die doesn't categorize death, its unfortunate that you see death from a human perspective because all you carry is hate and violence, i have to tell you that you will also die, your childrens will also and everyone else will, either from natural causes, diseases, wars you must die!
 
We mletauzi hebungoja nikuulize kwa msisitizo.

Are you Crazy???.

Kama hujui kingereza nakuuliza, Wewe ni Kichaa???.

Yani huoni umuhimu wa daraja la busisi ama unataka kutukanwa tu.
 
Back
Top Bottom