#COVID19 Rais Samia Suluhu: Tutalichukulia kwa uzito suala la COVID-19

#COVID19 Rais Samia Suluhu: Tutalichukulia kwa uzito suala la COVID-19

mimi sitachanja hata ikija. hata wazungu wengi tu huko kwao wamekataa kuchanjwa. sitaki.
 
Swala la chanjo liwe optional isiwe lazima.
 
Mama amegundua kuwa ni lazima science iheshimiwe, aachane na upuuzi.

Na Mungu aonewe haya tuende kwa Jina la JMT. Hata JPM akiwa kalala kaburini na wengine walio kufa iwe ni corona, uchawi ama sababu nyengine yeyote iwayo ile. Mungu wa Mbinguni atabaki kuwa Mungu. Nguvu na Uweza wake Mkuu havilinganishwi, havifananishwi wala kushindanishwa wala kushindwa na chochote kile kiwacho. Ikiwemo hiyo sayansi inayotakiwa ichukue mkondo wake.

Mrithi wa JPM awe macho na achukue tahadhari zote kwa kauli zake na matendo yake. Asifikie pahala akataka kutuonesha na kuangana na wanao taka kuonesha kwamba uamuzi wa Marehemu JPM wa kumtegemea Mungu kwanza kwa kila jambo la taifa hili ikiwemo na corona ulikuwa wa kijinga. Atajikuta yeye na wa aina yake wamemkufuru Mungu wa Mbinguni. Hakika watakuja kujutia kosa hili.

Kama hawana agenda nyingine za kutafutia umaarufu wa kisiasa na kushawishi kukubalika na kuungwa mkono ndani na nje ya Tanzania waombe wasaidiwe mawazo. Waachane na hii habari ya kutaka kuwaona Watanzania walioungana baada ya kuhimizwa maombi na kufunga na almaruhumu JPM kwamba walishawishiwa kuchukua hatua za kijinga badala ya kufata sayansi. Hawamdhika yeye JPM na Watanzania wenzao tu, bali wanamdhihaki Mungu wa mbinguni.
 
Shalom "Bwana Mungu akasema nami juu ya ujio wa chanjo ya Corona kwa kasi sana barani Africa ikiwemo Tanzania ingawa baadhi ya nchi za Africa zinaendelea na udungaji wa chanjo hizo pia Bwana akanionyesha Contena saba ziko kwenye kama behewa kubwa ila ndani ya maji na ndani yake kuna sindano kama ndogo ndogo hivi nyingi na gloves nyingi na madwa mengi kisha Bwana akanionyesha watu wengi humo ndani ya behewa wazungu na watu weusi wengi lakini cha ajabu watu hawa walikuwa wakisheherekea hivi wengine wakisema tumeshinda na haya ni maono ya wazi wazi kisha Bwana akaniambia niwaambie watanzania wenzangu niwaambie watumishi wa Mungu wote tuombe sana juu ya taifa letu ila rehema na toba ya ndani kwa kanisa lote na taifa,Tuziombee familia zetu na tuwaombee bila kuchoka viongozi wa taifa letu la Tanzania maana Lucifer ameandaa uharibifu mkubwa kupitia wakala zake ambao ni baadhi ya watu katikati ya wanadamu Mungu atupe kutii amen.
Amina
 
Huu ndio utakuwa unabii wa kwanza kupingwa na Chadema, natabiri tu!
 
mimi sitachanja hata ikija. hata wazungu wengi tu huko kwao wamekataa kuchanjwa. sitaki.
Ndugu yangu omba Mungu atusaidie. Kama wewe ni mwajiriwa,hivi bosi akisema wafanyakazi wote wachanjwe utakataa?
au umeishajiandaa kuacha kazi? Kama wewe ni mfanya biashara,sehemu unakonunua bidhaa wakisema huingii kununua mpaka uoneshe cheti cha chanjo utapata wapi bidhaa? n.k ndo maana tusisubiri wakati ufike,tuombe Mungu atunusuru.

Sishangai wanaoshadadia chanjo,huenda ni wadau wa hiyo biashara,maisha ya watanzania si kitu kwao.
ikumbukwe kulitokea kashfa ya dawa feki za kufubaza makali ya ukimwi,na huyo mfanya biashara alijipatia fedha nyingi
bila kujali kwamba anapukutisha maisha ya watanzania wenzake,sitashangaa watu kushadadia chanjo.
Tuwaombee wataalam watakaoifanyia utafiti na kuwashauri viongozi wa nchi nini kifanyike wawe na moyo wa kizalendo.
 
Kenya tu hapo yamewakuta inaelezwa Kuna watu zaidi ya 200 hali sio nzuri baada ya chanjo, Mungu awape maono mema viongozi wetu
Unajiita mlokole ila unaongea uongo. Thibitisha hili.

Kama wewe hutaki chanjo sisi tunataka.

Hata ARVs mlisema hivi hivi ila sasa mnabugia kama pipi.
 
Chanjo zitasaidia kupunguza vifo haswa kwa Wazee na wenye magonjwa sugu
Wao Waingereza wanasema hivyo kwa sababu wana Winter ambayo hata Flu huwa inawasumbua sisi hatuna Winter

Winter watu kukohoa kohoa na kupiga chafya sana

Sisi tukipata chanjo itatusaidia sana
Mara marufuku kwa walio chini ya 30 mara kwa walio chini ya 60, zungukeni mrudi kwa Magu[emoji38][emoji38]
JamiiForums-959571117.jpg


Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Toka mwendazake atutoke hatujasikia vifo vya corona wala vinavyotokana na changamoto ya kupumua, je kwa nini sasa mnataka kuunda kamati na kwa maslahi ya nani?
unataka watangaze ili iweje? kwasababu hajasikia haimaanish watu hawafi.
kamati itakayoundwa ni ku asses impact ya corona nchini ktk nyanja zote. then watatoa suggestion nn kifanyike
 
unataka watangaze ili iweje? kwasababu hajasikia haimaanish watu hawafi.
kamati itakayoundwa ni ku asses impact ya corona nchini ktk nyanja zote. then watatoa suggestion nn kifanyike
Mbona hatusikii hata mtaani achilia mbali huko kutangazwa!! Yaani corona unaweza kuficha kishindo chale kweli mpaka iyo kamati ndo ije itupige sound?
 
Lengo ni kurudisha mahusiano mazuri na wazungu hivyo tutalazimika kufuata yale wanayotaka tufanye kuhusiana na corona hasa kuagiza chanjo za corona,kwahiyo hayo ndio masilahi na ndio ikabidi atolewe pale Kabudi.
 
Back
Top Bottom