DOKEZO Rais Samia tafadhali chunguza BRELA kwani ni kikwazo kwa wafanyabiashara, bila hongo hufungui kampuni

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
BRELA wamekuwa sababu ya wafanyabiashara wengi kushindwa kurasimisha biashara zao kwani ukitaka kufungua kampuni utapitia machungu na mwisho utaacha kabisa.

Brela wamekuwa wanafanya masahihisho ya maombi kwa mtindo wa kuchelewesha ili mwombaji atoe rushwa.

Brela wanasahihisha neno moja moja na kufanya zoezi kuwa refu na lisiloisha ili wapate mwanya wa rushwa. Tafadhali Rais Samia tusaidie kuondokana na watendaji hawa wabovu pale Brela.
 
#BrelaMwanza unakwenda ofisini na hukuti mhusika pale jengo la mkuu wa mkoa.

Yule mtu utaishia kuambiwa "alikujacasubuhi na kuondoka"
Ukimpigia simu kwa namba iliyoko mlango wa Ofisi pia mara nyingi hapokei.

Na ikitikea akapokea simu.Atakupa maelekezo ya kwenda kwa wakala wao.

Na ukimpata ofisini, anaongea kama vile umemkera kwenda pale!
Hiyo ndio Tanzania ya Samia!
 
BRELA wamekuwa sababu ya wafanyabiashara wengi kushindwa kurasimisha biashara zao kwani ukitaka kufungua kampuni utapitia machungu na mwisho utaacha kabisa.

Brela wamekuwa wanafanya masahihisho ya maombi kwa mtindo wa kuchelewesha ili mwombaji atoe rushwa.

Brela wanasahihisha neno moja moja na kufanya zoezi kuwa refu na lisiloisha ili wapate mwanya wa rushwa. Tafadhali Rais Samia tusaidie kuondokana na watendaji hawa wabovu pale Brela.
Nilihangaika kusajili business name kwa ile takataka yao ya online mpaka nikachemsha na hela yangu walishakula...nimeamua kupuyanga kienyeji years later ntatafuta kishoka nimpe hela akafanye manually!
 
BRELA wamekuwa sababu ya wafanyabiashara wengi kushindwa kurasimisha biashara zao kwani ukitaka kufungua kampuni utapitia machungu na mwisho utaacha kabisa.

Brela wamekuwa wanafanya masahihisho ya maombi kwa mtindo wa kuchelewesha ili mwombaji atoe rushwa.

Brela wanasahihisha neno moja moja na kufanya zoezi kuwa refu na lisiloisha ili wapate mwanya wa rushwa. Tafadhali Rais Samia tusaidie kuondokana na watendaji hawa wabovu pale Brela.
Takukuru Wana kazi gani? Waziri wa Viwanda na Biashara ana kazi gani?
 
KIZIMKAZI kwenye suala la rushwa kashindwa kabisa kutetea watanganyika.pole yetu
 
Siyo kwa mateso haya ya brela nimejaribu kuhuisha kampuni yangu kwa njia mtandao ORS yangu mwaka 2017 Hadi Leo na hela yangu walishakula nikiri kuwa nimechemsha Hadi leo,kila ukifanya unajibiwa system imefeli,Hadi Leo hii kampuni yangu imesajiliwa manually tu,ORS nilishashindwa yaani ni ukiritimba kwa kwenda mbele Hadi nimeomba poooo! Wajuzi wa hizo issue mnisaidie,hivi brela wanaishi dunia ya wapi iliyotopea kwenye dimbwi la rushes namna hii,yaani hakuna huduma kabisa,labda ukikubali kuliwa.
 
Bila kuwafurusha BRELA sidhani kama patatulia Mhe.Waziri mkuu tunaomba utupie macho pale wale vijana hawafai kabsaa, kusajiri kampuni sio chini ya miezi 6, ujinga gani huu, hao vijana wafunguliwe kesi ya uhujumu uchumi.Ukipiga simu yaweza kupokelewa baada ya siku 4 hapo ujipange kutofanya kitu chochote kile kazi yako iwe ya kupiga simu tuu BRELA bila hivyo hata mwezi utaisha bila kupokea simu.
 
Kwani Shida ya Brela huwa ni kitu gani yaani????

Status "Make final decision" mwezi mzima imeng'ang'ania hapo kila kitu kina simama kwa ajili ya hawa wapumbavu.

Simu hawapokei email hazijibiwa sasa hawa wanalipwa mshahara kwa kazi gani?
 
BRELA wamekuwa sababu ya wafanyabiashara wengi kushindwa kurasimisha biashara zao kwani ukitaka kufungua kampuni utapitia machungu na mwisho utaacha kabisa.

Brela wamekuwa wanafanya masahihisho ya maombi kwa mtindo wa kuchelewesha ili mwombaji atoe rushwa.

Brela wanasahihisha neno moja moja na kufanya zoezi kuwa refu na lisiloisha ili wapate mwanya wa rushwa. Tafadhali Rais Samia tusaidie kuondokana na watendaji hawa wabovu pale Brela.
Mkuu,Kuna tatizo Brela ila nafikiri Tatizo sio watendaji bali ni Brela yenyewe kutokuwa na Standard Operating Procedures matokeo yake unakuta kila mara kunakuwa na marekebisho ambayo yanategemea ni nani anapitia nyaraka zako kwa wakti huo.

Kwa mfano Bado Brela wanahitajika kufanya namna kuwe na clear SOPs na Taratibu za utoaji wa feedback na iwapo kuna changamoto basi wanapaswa kutoa taarifa kwa wakati kwa mteja
 
Back
Top Bottom