butron
JF-Expert Member
- Jun 3, 2013
- 5,640
- 7,943
Anzia dakika ya 9:25 mpaka 9:40.
View: https://www.youtube.com/live/PEzgcxu_A50?si=AFWVhAKOGy8b_VG7
Akiwa kwenye ikulu ya Rashtrapati Bhavan huko New Delhi, India, baada ya kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake kwenye ziara yake nchini humo, Rais Samia alipewa wasaa wa kusema machache.
Katika machache hayo aliyoyasema, Rais Samia kasema kuwa eti mahusiano katika ya Tanzania na India yaliasisiwa na Mahatma Gandhi na Julius Nyerere!
Sidhani kama hilo ni kweli.
Gandhi alikufa mwaka 1948. Mwaka huo huo Nyerere alikuwa bado ni mwalimu huko Tabora.
Sasa Gandhi na Nyerere walianzishaje hayo mahusiano baina ya hizi nchi mbili?
Huenda labda alimaanisha kusema Jawaharlal Nehru na Julius Nyerere? Kama alimaanisha hivyo, sawa.
Hii ni constructive criticism.
Awe anafanya ‘homework’ yake vizuri maana hii si mara ya kwanza yeye kusema vitu visivyo sahihi kwenye medani za kimataifa.
Kuna wakati aliwahi kusema kuwa Kamala Harris ndo mwanamke wa kwanza Marekani kugombea moja ya nafasi za juu kabisa nchini humo, kana kwamba hajui chochote kuhusu Geraldine Ferraro.
Aache uvivu. Awe anajiandaa vizuri kwa kusoma kabla hajafungua mdomo wake na kuanza kusema mambo yasiyo sahihi.
Kuna yule fala mwingine Mulugo alisema kuwa Tanzania ilipatikana baada ya Tanganyika kuungana na Zimbabwe!🤣🤣