bucho
JF-Expert Member
- Jul 13, 2010
- 5,149
- 3,209
Wewe kama ni mzima huna shida yoyote mshukuru Mungu....ila usiwe msemaji wa watu wengine kuhusu maisha yaoKwahiyo ukiwa na "magonjwa sugu" unakimbilia kudungwa chanjo ya corona?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe kama ni mzima huna shida yoyote mshukuru Mungu....ila usiwe msemaji wa watu wengine kuhusu maisha yaoKwahiyo ukiwa na "magonjwa sugu" unakimbilia kudungwa chanjo ya corona?
Mkuu
Unauliza wakati shehena ilishatinga mlangoni? Ushoga tayari njia nyeupe ila hatatangaza hadgarani!!!
Timu iliyoundwa tayari imekuwa 'compromised' majibu yatakayotoka yataendana na kileambacho tayari kinaonekana hadharani wanakifanya
Utahama wewe kwanza mimi nipo mpaka mwisho wa dunia.Wee ni pro mwendazake hatushangai 🤣🤣🤣, na sio lazima unaweza hama hata nchi kama vp hamia Madagascar. OVER!!
Hizi drama za corona zinasisimua na kuchekesha sana.
Miezi michache nyuma, kulizuka wimbi kubwa la vifo vya viongozi wakubwa na watu mashuhuri — Tukaambiwa wamefariki kwa corona.
Muendelezo wa vifo ulichachamaa mpaka ukamkumba Rais John Magufuli. Naye "tukaaminishwa" amefariki kwa corona kinyume na taarifa rasmi ya daktari.
Tangu alipofariki Rais Magufuli, hatusikia tena kuhusu vifo vya vigogo wa serikali.
Tukaambiwa corona imeenda likizo (annual leave) na kwamba itarejea kwa makali hapo baadaye.
Pamoja na drama zote hizi za kuigiza, sisi wakazi wa Kariakoo siku zote tunasongamana na hakuna hata mmoja aliyeugua japo mafua ya bahati mbaya.
Hata yale mabarakoa sijayaona. Watu wanadunda tu.
Hakuna cha wimbi wala mawimbi. Kila siku watu wapo tu na wanaendelea na maisha yao wakiwa na afya zile zile.
Tukaambiwa linakuja wimbi sijui la pili. Wenyewe wanaita ati "second wave".
Hilo wimbi nalo likaja likatukuta vile vile na likaondoka likatuacha vile vile.
Hivi sasa tunaambiwa kuwa hilo wimbi limekimbilia India. Likipiga "rivasi" linarudi tena Tanganyika likiwa na maguvu mengi.
Bibi samia anatueleza habari za chanjo. Bila shaka ziko mbioni kuja.
Najiuliza, hizo chanjo anamdunga nani?
Sisi wakazi wa Kariakoo na kwingineko, wala hatuna ugonjwa wowote ule.
Tunapoelezwa kuhusu chanjo, tunahamaki!
Wale wajuzi wa corona hebu mtueleze, hizo chanjo mnamdunga nani?
Mnawadunga hawa hawa watu ninawaona wakiwa na afya tele kila siku?
Ama kuna wagonjwa mahali ambao hatujaambiwa kuhusu taarifa zao?
Magu kaondoka na Corona,sasa wewe na familia msivae barakoa kama Magu.ni suala la muda tu, nilijua tu tunapoelekea sooner or later Chanjo itakuja maana mwenye misimamo yake alishaenda, Kweli Magu tunakukumbuka sana mzee
Kwahiyo na wewe unasubiri kudungwa chanjo?
Ohh sawa!Chanjo ni kwa wale wanauhitaji
Hii ni kauli ya Mh Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania Madam President Samia Suluhu Hassan. leo.
"Nataka kuwahakikishia kwamba tahadhari zote mlizotoa hapa juu ya chanjo na mengine zitafuatwa, kikamilifu na Serikali yenu, hata hivyo hii haina maana kwamba tutapokea kila kitu tutakacholetewa au kuambiwa la hasha lazima na sisi tukiridhishe.
Hata suala la chanjo tutajiridhisha kwanza kabla ya kuamua kutumia au kuacha kutumia.hivyo nawaasa watanzania kutokuwa na hofu yoyote Serikali iko makini sana katika kushughulikia suala hilo"......Rais Samia Suluhu Hassan 14/mei /2021.
MY TAKE ON COVID 19 VACCINE
Tanzania haina historia ya kugomea wala kukimbilia chanjo.
nikitolea mfano wa chanjo dhidi ya kansa ya shingo ya kizazi ambayo duniani ilianza kutumika mwaka 2006 ilichukua miaka 12 kuanza kutumika rasmi nchini Tanzania.Mwaka 2018 Serikali ilianza kueneza matumizi ya chanjo hii kwa awamu katika mikoa ya Tanzania.baada ya majaribio kadhaa miaka michache kabla.
Kenya walianza kuitumia mwaka mmoja au miwili kabla.
Ikumbukwe kansa ya shingo ya kizazi imeumiza na kuua kina mama wengi pengine kuliko covid 19.do we have clear reasons why should the nation fast track and accept covid 19 vaccines?
Wazo la kufanya uchambuzi wa kina juu ya chanjo za corona ni wazo la kisayansi.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
View attachment 1784954
Mimi sitachanjwa!
Nenda ukachanjwe kama mboweChanjo haidungwi bali ina chanjwa. Ukweli mchungu - suala la chanjo ni hiari. Wanaoihitaji chanjo tupo wengi sana.
Kwamba kuna wanaotaka na wasiotaka chanjo mbona jambo la kheri tu?
Heko Mufti kwa kutambua mtaani kuna wataalamu na wataalamu pori:
View attachment 1784968
Tutasimama na wataalamu lakini si mamburula!
Na wewe utapotea karibuni nakuona corona unayokichwani mwako.Naona unasema ikatuacha vilevile !! unaweka ushabiki kwasababu hujafiwa kaongee na wale Watanzania waliopeteza ndugu zao kuanzia mwezi wa kwanza 2020!. Chanjo ni kwa wale wanauhitaji kama hauko kwenye wahitaji basi usifanye lakini huna haki za kuweka siasa zako kwa wananchi wote kwasababu ya fikra binafsi. Hakuna mtu analazimishwa kufanya chanjo wanacho omba wengi ni upatikanaji tu maana hizi chanjo haziuzwi kwa watu binafsi kwa sasa. Chanjo zingekuwa zinapatikana wala watu wasingeongelea serikali. Mimi nimepoteza marafiki wawili Tanzania kwa Corona najua uchungu wake
IrrelevantMbowe alichanjwa haraka sana
Nenda hapo Kenya kwa Manyang'ao ipo.Hongera sana kwa uchaguzi wako. Kuchanjwa au kuacha ni optional. Tatizo hamna.
Ila mimi na washirika zangu tutachanjwa mapema kabisa. Hapa tulipo tunalaani kwani mwendazake alituchelewesha mno!
Nenda ukachanjwe kama mbowe
Nenda Kenya au Dubai ukachanjweNaona unasema ikatuacha vilevile !! unaweka ushabiki kwasababu hujafiwa kaongee na wale Watanzania waliopeteza ndugu zao kuanzia mwezi wa kwanza 2020!. Chanjo ni kwa wale wanauhitaji kama hauko kwenye wahitaji basi usifanye lakini huna haki za kuweka siasa zako kwa wananchi wote kwasababu ya fikra binafsi. Hakuna mtu analazimishwa kufanya chanjo wanacho omba wengi ni upatikanaji tu maana hizi chanjo haziuzwi kwa watu binafsi kwa sasa. Chanjo zingekuwa zinapatikana wala watu wasingeongelea serikali. Mimi nimepoteza marafiki wawili Tanzania kwa Corona najua uchungu wake
Nenda hapo Kenya kwa Manyang'ao ipo.
Ushauri tu maana unapigika sana na awamu sita 🤣🤣, na ndo kwanza ni miez miwil tu. Shubaaamiiit!!Utahama wewe kwanza mimi nipo mpaka mwisho wa dunia.