#COVID19 Rais Samia: Tanzania kuna wagonjwa zaidi ya 100 wa Corona. Chanjo itakuwa ya hiyari

#COVID19 Rais Samia: Tanzania kuna wagonjwa zaidi ya 100 wa Corona. Chanjo itakuwa ya hiyari

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Rais Samia amesema wafanyabiashara wengi wa Kitanzania wameshachanja chanjo ya Corona wengine Dubai, SA na Nairobi.

Rais amesema baraza la mawaziri limekaa na kuamua tukubaliane na chanjo na iwe ni hiyari.

Serikali imeshatenga usd 470 milioni kukabiliana na covid 19.

Nawasalimu kwa jina la JMT.

---
Kuna wanaoona hatuko serious ktk mapambano dhidi ya #COVID19. Nilipoingia madarakani nilitamani tupambane na ugonjwa huu kama wanavyofanya mataifa mengine. Tanzania tuna wagonjwa zaidi ya 100 wenye #coronavirus #wave3, kati yao Wagonjwa 70 naa, wapo kwenye mitungi na wengine matibabu ya kawaida.

Tumeamua tukubali chanjo kwa walio tayari.

Tanzania tumeingia kwenye #COVAX community. Wataalamu wetu wanafanyia kazi Chanjo ipi inafaa kwa Watanzania. Kuna mashirika mengi wamejitokeza kutaka kusaidia Watanzania lakini lazima wataalamu wetu ndio watoe ushauri kitaalamu.

Sisi kama Serikali tunahimiza yale yanayoshauriwa na wataalamu; kama unaamini kwenye kupiga nyungu - wewe piga. Kila mmoja atekeleze wajibu wake. Jikingeni sana na wakingeni watoto.

Samia Corona.jpg
 
Hizo takwimu za wagonjwa kwanini zisiwe zinatolewa kwa public?

Rais anajitahidi sana kuendana na kile WHO wanataka, ningependa atuambie hao wagonjwa wamelazwa hospitali zipi? familia zao wameziweka karantini? na mikoa ipi inaongoza kwa maambukizi.

This is a wake up call, tuamke, ile likizo ya Corona imeisha, now kirusi kipo mjini.
 
Wameweka ndoano ya hela hatimaye kanasa!

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ukiwa masikini ni sawa na [emoji205][emoji205][emoji205][emoji205]
Magufuli hela yoote alimalizia kujijenga kule Chato, na kwa vile haukuwa mpango wa Mungu akafa huku hajakamilisha azma yake.

Wacha tu mama atembeze bakuli afufue uchumi, hakuna namna!
 
Hizo takwimu za wagonjwa kwanini zisiwe zinatolewa kwa public?

Rais anajitahidi sana kuendana na kile WHO wanataka, ningependa atuambie hao wagonjwa wamelazwa hospitali zipi na mikoa ipi inaongoza kwa maambukizi.

This is a wake up call, tuamke, ile likizo ya Corona imeisha, now kirusi kipo mjini.
Si ndio ameanza hivyo
 
Hizo takwimu za wagonjwa kwanini zisiwe zinatolewa kwa public?

Rais anajitahidi sana kuendana na kile WHO wanataka, ningependa atuambie hao wagonjwa wamelazwa hospitali zipi? familia zao wameziweka karantini? na mikoa ipi inaongoza kwa maambukizi.

This is a wake up call, tuamke, ile likizo ya Corona imeisha, now kirusi kipo mjini.
Kirusi lini kiliondoka?

Takwimu zinasaidia nini?

Huko Ulaya kwenyewe walishaanza kuachana na huo ujinga maisha yaendelee kama kawaida.
 
Wameweka ndoano ya hela hatimaye kanasa!

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ukiwa masikini ni sawa na [emoji205][emoji205][emoji205][emoji205]
We kweli ni pimbi, kwani umelazimishwa? usipochanjwa wewe mumeo atachanjwa
 
Mimi nina mwezi na nusu tangu nichanje full. Naendelea kuvaa barakoa kwani najua chanjo si kinga asilimia 100. Ila ukichukua chanjo ukajumlisha barakoa, distancing , kujisanitize au kunawa unakaribia kabisa kujikinga kwa asilimia 100.

Dunia ina lengo la kuukomesha ugonjwa huu. Katika lengo hilo ndipo zinakuja hatua mbalimbali ikiwemo kutoa fedha ili kuziwezesha nchi masikini ( Afrika) . Hata Ulaya zipo nchi zimewezeshwa kifedha ili kupigana na covid 19.

Wanaoona hizi fedha ni mtego ni wivu wao tu unawasumbua. Mbona hapo awali hawakusema ni mtego au kwavile zilichukuliwa kimyakimya zikawekwa mifukoni mwa miungu yao!

Mama endelea kuupiga mwingi. Unafanya kazi inayoonekana, siyo blabla tulizokuwa tunaimbiwa na wale watesaji.
 
Back
Top Bottom