Ukweli uliojificha. Jambo hili lina pande mbili: Mosi, ongezeko la watu na mifugo ni hatari kwa uhifadhi, hii nadhani inatokana na wenyeji kutokuwa waminifu na wazalendo.
Wamekaribisha mifugo ya Wakenya na wanafanya siasa hifadhini, na ndiyo unaona leo kelele zinapigwa sana Kenya. Kenya wanamuomba Mh Uhuru aje aongee na Rais Samia. Kwa lipi? Wote tujiulize.
Pili, uhifadhi wa mazingira wa Ngorongoro ni mkubwa sana, na ndiyo maana kila mfugaji tajiri awe Kenya au Tanzania atapeleka mifugo kule kwani nyasi ni nyingi sana kwa ajili ya wanyama pori na maji yapo throughout the year, na ndiyo ugomvi, wameharibu mazingira katika maeneo yao wanaingiza mifugo yao kwenye hifadhi.
Hifadhi ni km 1,500 za mraba, eneo la wamasai wamepewa km 2,500 za mraba kwa ajili yao na mifugo. Sasa wanataka zile km 1,500 za mraba na wao wawepo! Kama umefuatilia jana yupo Mkenya ametoa kauli ya serikali kuacha mara moja uwekaji wa alama za mawe kuzunguka hifadhi.
Heshima mkuu Huihui,
Haya unayoeleza hapa umeeleza upande mmoja, ingawaje mwanzo ulisema pande mbili.
Haya hapa ninakubaliana nawe, isipokuwa anayebeba lawama kubwa ni serikali yenyewe kushindwa kusimamia kazi yake ipasavyo.
Kwa nini mifugo itoke Kenya ije kulishwa Tanzania, huoni kasoro hii. Kwa hiyo makosa haya ni ya kuwalaumu wakazi wa Loliondo, na siyo serikali kushindwa kazi ya kulinda mipaka ya nchi yetu?
Uhifadhi ni muhimu, na kama kuna uharibifu ni udhaifu wa serikali hiyo hiyo. Wakazi wa eneo hilo wao wenyewe ndio wangekuwa wanahimiza uhifadhi kama wange elimishwa faida za uhifadhi huo, faida ambazo wao wenyewe ndio wangekuwa wanufaika wakubwa.
Unamlaumu mtu ambaye hata siku moja hujamuelimisha chochote, na wala kumwonyesha faida zinazotokana na yeye kuwa mwangalifu na mazingira yake asitaharibu?
Sasa una utendaji wa serikali ulivyo mbovu. Kama wamefanya tathmini na kuona kuwa uharibifu umetokea, taarifa hiyo ilifika kwa wananchi?
Wananchi wanapewa amri tu, kuhama miezi sita, na hapo hapo wanaanza kupewa vitisho wasipotii amri?
Na kama bado huelewi ninachoandika hapa, wananchi hawa hawa wanaijua historia chafu na ovu ya serikali yao, kwani walishatendewa uovu huo kupitia kwa mwekezaji aliyeletwa na kuwanyanyasa wananchi ndani ya nchi yao.
Wanachoelewa wananchi sasa hivi na serikali hii ni mwendelezo huo huo wa unyanyasaji. Mwekezaji, ambaye hata siku moja hawajawanufaisha chochote na uwekezaji wake, bali uonevu, sasa analindwa zaidi na serikali kuliko serikali kulinda maslahi ya wananchi wake..
Hatukutafuta uhuru wetu, halafu miaka michache tu tuwe tumechoka na kuwa huru na kuanza kutafuta wakoloni wengine waje kutunyanyasa ndani ya nchi yetu, kwa vipande vya rushwa wanavyopewa hawa wasaliti wa uhuru wetu.