Rais Samia: Tumeleta umeme Kigoma ili kuvutia Uwekezaji

Rais Samia: Tumeleta umeme Kigoma ili kuvutia Uwekezaji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan Mkoani Kigoma, leo Jumatatu Oktoba 17, 2022

Akizindua Umeme wa Gridi ya Taifa na Uzimaji wa Jenereta katika Mkoa wa Kigoma - Kasulu Mjini.
Rais Samia amesema lengo la kuleta umeme kigoma ni kuanza kuvutia wawekezaji kwenye mkoa huo ulio pembenzoni mwa nchi.

Amewataka wananchi wa Kigoma kutunza majenereta yaliyokuwa yanatumika zamani pamoja na miundombinu mipya ya kusafirisha umeme iliyojengwa ili nishati hiyo ichochee maendeleo ya watu.
 
Nani alipiga pasi nguo ya Rais!!!

1665996459045.png
 
Wale wa kulalamikia bei ya petrol wapo kimyaaa siku hizi. Hili ni suala la maana sana limefanyika huko Kigoma leo hii.
 
Wrong approach.

Inatakiwa umeme umsaidie mzawa kujikwamua kiuchumi na sio kumwezesha mgeni kuja kushika vyanzo vya uchumi vya Taifa hili.

Kuendelea kufikiria kuwa wageni ndio wataleta maendeleo yetu badala ya sisi wenyewe ni makosa yanayojirudia kila mara katika awamu hii.
 
Waha na Wamanyema sijui watatoa zawadi gani ngoja tuone?

Migebuka?! Mama kachoshwa na Vibua.
Mtazamo huu ni wa kipuuzi.Tumpe zawadi kwa nini?Anatekeleza wajibu wake kama sisi tunavyotekeleza wajibu wa kulipa kodi.
 
Mtazamo huu ni wa kipuuzi.Tumpe zawadi kwa nini?Anatekeleza wajibu wake kama sisi tunavyotekeleza wajibu wa kulipa kodi.
Tamaduni za KiChifu hizo,yeye kama Chifu Hangaya Machifu wa Kiha na Kimanyema sijui watampa zawadi gani.
 
Wrong approach.

Inatakiwa umeme umsaidie mzawa kujikwamua kiuchumi na sio kumwezesha mgeni kuja kushika vyanzo vya uchumi vya Taifa hili.

Kuendelea kufikiria kuwa wageni ndio wataleta maendeleo yetu badala ya sisi wenyewe ni makosa yanayojirudia kila mara katika awamu hii.
Huyo mwenyeji wa nchi amekatazwa kwenda Kigoma na kutumia fursa za maendeleo katika uwekezaji?.

Dunia ya sasa ni kama kijiji, hauwezi ukamkwepa mwekezaji, anayo maarifa makubwa anao uzoefu wa sekta husika.

Wawekezaji ndio wameinua Dubai tunayoiona leo hii, ndio wameinua Marekani ya miaka na miaka, huwezi kuwakwepa cha muhimu ni kuwaelewa na kuishi nao kuliko kuendekeza zile falsafa za kichoyo na kibaguzi eti kwamba kibali cha kazi kikimalizika mgeni arudi kwao!!.

Anarudi kwao huku akiacha kazi aliyoifanya nusu ikiendelea kuwa na matokeo mabovu kwa sababu ya ukosefu wa taaluma na maarifa aliyowekeza kipindi anafanya kazi nchini.
 
Wananchi wa Kigoma tuna imani na Rais wetu Mama Samia.
Rais wetu ni mtu mwadilifu na mtendaji anaye wajibika kikamilifu kwa watanzania wote.
 
Back
Top Bottom