Rais Samia: Tuna ‘crisis’ ya umeme, tunafanya ukarabati wa mashine

Rais Samia: Tuna ‘crisis’ ya umeme, tunafanya ukarabati wa mashine

Huyu Hangaya hana kauli yoyote....anasubiri remote itoe signal ndio afungue mdomo.

👇👇....c&p
Gangsters in Suit.

KIPARA na Maharage mwezi Machi 2023, waliagiza na kuamuru maji katika bwawa la Mtera (Catchment area; 68,000 km² (26,000 sq mi)) yafunguliwe na kumwagika nje.

Hoja yao; Maji yangelijaa sana na yangelipasua bwawa la Mtera. Wahandisi na wataalam kutoka katika bwawa la Mtera wakapinga jambo hilo kitaalam.

Wataalam na wahandisi kutoka Mtera wakawaleza hifadhi ya maji (reservoirs) kwenye Rock-fill dam hutumika kwa shughuli nyingi siyo Hydropower tu.

Hifadhi ya maji (reservoirs) kwenye Rock-fill dam (kama Mtera) hutumika hata katika irrigation, human consumption, industrial use, aquaculture, na navigability.

Lakini kwa mamlaka yao, KIPARA na Maharage wakaagiza kwa lazima maji yafunguliwe katika bwawa la Mtera. Maji yakafunguliwa.

Maji hayakujaa tena katika bwawa la Mtera, kwa sababu mvua zilipotea. Sasa nchi yetu inapitia mgao mkali wa umeme kwa sababu ya wahuni.

Septemba 2023 mgao umekuwa mkali na wanaohusika na umeme wanajitetea kwamba kuna upungufu wa uzalishaji umeme kwenye mabwawa kutokana na ukame.

Kuliko kuwahamisha kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, hawa ‘wahuni’ walipaswa kupumzika utumishi wa umma. Hawatufai.

Tunataka kuamini kwamba ‘Rais ni taasisi’ na Rais anatakiwa kuwaondoa katika utumishi wa umma hawa wahuni. Haitakiwi kuwahamisha waharibifu kutoka ofisi moja kwenda nyingine.

Wakati hawa wahuni wakisubiri nje ya utumishi wa umma, Tunahitaji uchunguzi wa kamati maalum ya bunge katika jambo hili, haraka. Ingawa lenyewe ni dhaifu.

Haiwezekani wahuni wananufaika kuingiza na kuuza majenereta wakati wengine tunapata msoto wa mgao wa umeme. Wanatutia umaskini.

MMM, Mtikila.
Mkuu wangu anayepaswa kuondoka kwenye utumishi wa umma ni mkubwa wao yaani aliyewateua.

Kwani alikuwa hapati intel ya majibizano kati ya wataalam na wahuni walioteuliwa?

Kwa nini aliwaacha waendelee hadi utokee mgao?

Mnajuaje kama waliagizwa iwe hivyo na wao bila hofu wakatekeleza? Wanalindwa kwa sababu ni asset ya aliyewaweka pale
 
swala anayewinda naona kaanza kujaa kwenye kipimo chamlengaji, ngoja tuone mwisho wake
 
Ndugu zangu urais ni kazi ngumu. Ndiyo maana anko Magu aliamua kutumia maguvu tu maana katika nchi zetu hizi bila maguvu mambo aisee hayaendi. Huyu mama mpaka namwonea huruma sometimes. Hata watu wake wa karibu hawamsaidii masikini. Mungu na Amsaidie [emoji1545]
Kwani Uraisi kuna mtu analazimishwa! kama anajua hafit bora awaachie wanaoweza.
 
Akizungumia kuhusu changamoto ya kukatika kwa umeme, Rais Samia Suluhu Hassan amesema mitambo haikufanyiwa maboresho kwa muda mrefu, hivyo maboresho yanapofanyika baadhi itazimwa na ndio maana imesababisha upungufu wa umeme
Makamba alipoiingia alikuja na Wimbo huo huo mwa kutokakukarobatowa mitambo ,mpaka leo hiyo mitambo inakarabatowa tu ,huu mtawala ni wa hovyo kweli
 
Maharage tumekutoa TANESCO na nikachukulia uzoefu wako wa DSTV nikaona sekta ya TTCL ingekufaa zaidi. Sasa baadae nikagundua una biashara ndani ya TTCL na kwa sababu kampuni ile inafanya vizuri na ndio maana imemuwezesha kijana yule nae kufanya vizuri nikasema hapana, usiende mahali ambapo una biashara, itakuwa conflict of interest. Nikaona sasa nikupe u postamasta mkuu "Alisema Rais Samia".
duh
20230926_143207.jpg
 
Makamba alisema hivyo hivyo tangu ateuliwe yeye anasema Leo tena

Maharage alisema ishu ni maji Leo Samia amasema mitambo

Hamna Rais hapo ni kilemba tu

USSR
Mwanasesere wetu
 
Makamba alisema hivyo hivyo tangu ateuliwe yeye anasema Leo tena

Maharage alisema ishu ni maji Leo Samia amasema mitambo

Hamna Rais hapo ni kilemba tu

USSR
Waongo waongo waongo kabisa! Shame on you people!
 
Jamani mkumbuke wkt wa JPM hakutaka kusikia kuwa mitambo imeharibika au ina hitilafu so nadhani kwa miaka 7 haijafanyiwa ukarabati kabisa kwa kumuogopa mzee...tumpe muda madam Prezdaa
 
Hapa ndio utagundua kuna kamchezo wanatuchezea, kipara ngwidu alisema mitambo na miundombinu imechakaa ndio sababu ya umeme kukatika akapewa mabilioni kwa ajili ya ukarabati, maharage ya Mbeya na yeye akaja na stori yake ya tofauti alafu bibi yao na yeye anakuja kusema eti wanafanya ukarabati wa mashine,
sasa swali linakuja ni ukarabati gani waliufanya kipindi kile cha kipara ngwidu kwa mabilioni yote Yale, na ni ukarabati gani wanaufanya sasa 🤔🤔 na anasema eti mitambo haija karabatiwa kwa muda mrefu, swali pia umepita muda gani tangu kipara ngwidu afanye ukarabati hadi sasa 🤔🤔
Pia kipara ngwidu alisema kipindi cha bwana mjomba mitambo ilikua haifanyiwi ukarabati ndio maana alivyo pewa wizara madhara yakaanza kuonekana, swali kwa nini kipindi kile mitambo ilivyo kua haifanyiwi ukarabati umeme ulikua haukatiki lakini kipindi amefanya ukarabati umeme ukaanza kukatika bila mpangilio🤔🤔
Hivi hawa jamaa Wana ajenda gani hasa 🤔🤔 alafu mbona kwao chamba wima umeme haukatiki kama huku 🤔🤔
 
ulipomtoa dr kailemani pale wizarani ukamweka MweziWaKwanza kwa mbwembewe na mikogo mingi sana alisema hivyo hivyo, kwamba miundombinu ya umeme ni mikuukuu na nichakavu na wanaanza kuihuisha.

Sasa nauliza MweziWakwanza hakufanya huisho lolote la miundombinu hiyo upande wowote?
Kwahiyo zile zilikua mbwembwe tu na alitwambia umeme upo wa kutosha mpaka vijijini?

Mama, MweziWaKwanza anatuchukuliaje lakini?
na mbona unamkumbatia sana na wakati ni mweupe na mwepesi tu?
wizara imemshinda ataweza hapo ulipoketi wewe?
au unaona aibu kwa mzee wake lakini pia kwa mzee wa ari mpya, nguvu zaidi, na kasi zaidi?
Huyo nitegemeo kwenye wizi wa kura kimtandao
 
Back
Top Bottom