Huyu Hangaya hana kauli yoyote....anasubiri remote itoe signal ndio afungue mdomo.
[emoji116][emoji116]....c&p
Gangsters in Suit.
KIPARA na Maharage mwezi Machi 2023, waliagiza na kuamuru maji katika bwawa la Mtera (Catchment area; 68,000 km² (26,000 sq mi)) yafunguliwe na kumwagika nje.
Hoja yao; Maji yangelijaa sana na yangelipasua bwawa la Mtera. Wahandisi na wataalam kutoka katika bwawa la Mtera wakapinga jambo hilo kitaalam.
Wataalam na wahandisi kutoka Mtera wakawaleza hifadhi ya maji (reservoirs) kwenye Rock-fill dam hutumika kwa shughuli nyingi siyo Hydropower tu.
Hifadhi ya maji (reservoirs) kwenye Rock-fill dam (kama Mtera) hutumika hata katika irrigation, human consumption, industrial use, aquaculture, na navigability.
Lakini kwa mamlaka yao, KIPARA na Maharage wakaagiza kwa lazima maji yafunguliwe katika bwawa la Mtera. Maji yakafunguliwa.
Maji hayakujaa tena katika bwawa la Mtera, kwa sababu mvua zilipotea. Sasa nchi yetu inapitia mgao mkali wa umeme kwa sababu ya wahuni.
Septemba 2023 mgao umekuwa mkali na wanaohusika na umeme wanajitetea kwamba kuna upungufu wa uzalishaji umeme kwenye mabwawa kutokana na ukame.
Kuliko kuwahamisha kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, hawa ‘wahuni’ walipaswa kupumzika utumishi wa umma. Hawatufai.
Tunataka kuamini kwamba ‘Rais ni taasisi’ na Rais anatakiwa kuwaondoa katika utumishi wa umma hawa wahuni. Haitakiwi kuwahamisha waharibifu kutoka ofisi moja kwenda nyingine.
Wakati hawa wahuni wakisubiri nje ya utumishi wa umma, Tunahitaji uchunguzi wa kamati maalum ya bunge katika jambo hili, haraka. Ingawa lenyewe ni dhaifu.
Haiwezekani wahuni wananufaika kuingiza na kuuza majenereta wakati wengine tunapata msoto wa mgao wa umeme. Wanatutia umaskini.
MMM, Mtikila.