Rais Samia: Tuna ‘crisis’ ya umeme, tunafanya ukarabati wa mashine

Huu upuuzi sasa. Huyo waziri makamba muda wote huu aliokuwa madarakani alikuwa anakarabati nini? Makamba akamatwe mara moja. Mama samia unaanza kuniudhi unajibu majibu mepesi kwenye maswali mazito.
Cha kushangaza huyo January amezawadiwa nafasi nyingine
Wakati ilitakiwa awekwe ndani.

Na amezawadiwa na Rais..
Huyu Rais utasemaje ni mzalendo wakati anawazawadia vyeo majizi?
Yeye tumuoneje kama amewakumbatia matapeli wa nchi,?

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Januari na maharage wanatakiwa kiwa ndani muda huu
 
Bora Tanganyika ingekuwa nchi ya Kiislamu.
Wamama wote wangeishia tu kupika jikoni.
Na ni mwiko kwenda Mbugani.

Sisi tunatulia huku mmama anaongea.
Hii haikubaliki hata kidogo.

Shehe Mazinge unalinaje hili?
Na Mujahidina FaizaFoxy,
Vipi biblia inasemaje?

Uislam hakuna mahala umesema mwanamke ni mtu wa jikoni. Uislam unafundisha mwanamke kulishwa, kuvishwa, kuheshimiwa.

Nafahamu unaleta kejeli lakini tatizo lako kubwa huuelewi Uislam kuwa ndiyo mfumo wa maisha yako. Laiti ungeuelewa usingefanya kejeli.

Nakushauri usome Uislam kwa faida yako, ya familia yako na jamii kwa ujumla.
 
Akizungumia kuhusu changamoto ya kukatika kwa umeme, Rais Samia Suluhu Hassan amesema mitambo haikufanyiwa maboresho kwa muda mrefu, hivyo maboresho yanapofanyika baadhi itazimwa na ndio maana imesababisha upungufu wa umeme

Kuna tatizo kwenye muhimili wa bunge ambao kazi yake ni kuishauri na kuisimamia serikali naamini hata kwenye hili la umeme wana nafasi kubwa ya kusaidia lakini wamemwacha Suluhu anapambana mwenyewe wao wambaki kama watazamaji na wazomeaji mpaka namkumbuka spika wa viwango mzee Sitta(Mungu ampe pumziko)maana kama ingekuwa lile bunge lake kuna watu wangewajibika
 
mpaka hapo , tuzoee tu Jambo la umeme limeshindikana. Tatizo kubwa sijui ni Nini . kusema marekebisho hapana!!!!
 
Hii stori tu.
Sio kuamini kila unachosikia..
 
Miezi 6 tumepewa yakununua majenereta, hiyo ni live live.
 
Akizungumia kuhusu changamoto ya kukatika kwa umeme, Rais Samia Suluhu Hassan amesema mitambo haikufanyiwa maboresho kwa muda mrefu, hivyo maboresho yanapofanyika baadhi itazimwa na ndio maana imesababisha upungufu wa umeme
Uongo na wanasiasa ni mapacha, tuliambiwa tatizo ni upungufu wa maji leo bitozo anasema ni ukarabati wa mitambo!
 
Akizungumia kuhusu changamoto ya kukatika kwa umeme, Rais Samia Suluhu Hassan amesema mitambo haikufanyiwa maboresho kwa muda mrefu, hivyo maboresho yanapofanyika baadhi itazimwa na ndio maana imesababisha upungufu wa umeme
Shida ni ukarabati wa mitambo au shida ni uzalishaji wa umeme.
Kama ni ukarabati si angewaacha waliokuwepo maana wao ndio walioanzisha hiyo miradi , baada ya watangulizi kushindwa kuliona Hilo.
Na hiyo miradi ya ukarabati wa mitambo ulianza lini 2017 au ndio unaanza sasa 2023 kuelekea hiyo miezi SITA ijayo
 
Unamshauri ajifunze primitivity?
 
Akizungumia kuhusu changamoto ya kukatika kwa umeme, Rais Samia Suluhu Hassan amesema mitambo haikufanyiwa maboresho kwa muda mrefu, hivyo maboresho yanapofanyika baadhi itazimwa na ndio maana imesababisha upungufu wa umeme
Samia amekuwa msemaji wa Tanesco tu hana lolote, mitambo inakarabatiwa pindi umeme unapokuwa hautoshi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…