Rais Samia: Tuna ‘crisis’ ya umeme, tunafanya ukarabati wa mashine

Rais Samia: Tuna ‘crisis’ ya umeme, tunafanya ukarabati wa mashine

Makamba alisema hivyo hivyo tangu ateuliwe yeye anasema Leo tena

Maharage alisema ishu ni maji Leo Samia amasema mitambo

Hamna Rais hapo ni kilemba tu

USSR
Tulieni jamani Mama anarekebisha mitambo kidogo!
Tanzania imepatikana safari hii!!🤣🤣🤣🤣
 
Bado anaimba chorus ya Bwana mdogo wakati wenzie wamerukia kwenye uhaba wa maji!

Yaani kila akijitutumua,anatoa Boko!

Ndiyo unaelewa kwa nini washauri wa kufikirika wamekuwa wakilalamikiwa kila wakati.
 
«crisis» gani kila mwaka ikifika miezi fulani umeme unasuasua? Same ol’ shit year in, year out tokea awe rais. Enzi zs Magufuli hakukuwepo hii adha. Mara mitambo inatengenezwa mara hali ya hewa??!! Kwanini hakuna mipango madhubuti ya kutumia nishati mbadala kama gesi na ikiiwezekana hata mafuta kuzalisha umeme?
 
This is insulting our intelligence kwahio mpaka kesho hatuna plan B na tutaendelea kuwa na mapungufu kila pale ambapo so called maintenance zinafanyika ?

Huenda mimi sio mwelewa lakini this shows lack of planning (hata kama anachosema ni kweli); Sababu walijua since day one kwamba maintenance zitafanyika na walijitayarisha vipi wakati wanazifanya ? Ni pesa ngani tumeshatumia katika Maintenance alizosema Makamba kwamba zikiisha na Mgao utaisha ? Ule usukaji mpya wa Makamba aliosema uliochukua mapesa ya kutosha umeishia wapi ?
Kwanini na wewe ni msahaulifu kiasi hicho? Mwaka jana walisema Magufuli hakuwahi kufanyia maintenance hivyo wanazima ili wafanye jambo hilo
 
Kwanini na wewe ni msahaulifu kiasi hicho? Mwaka jana walisema Magufuli hakuwahi kufanyia maintenance hivyo wanazima ili wafanye jambo hilo
Rudia kusoma nilichosema....... Nimesema and I Qoute...
Ni pesa ngani tumeshatumia katika Maintenance alizosema Makamba kwamba zikiisha na Mgao utaisha ?
 
Huyu Hangaya hana kauli yoyote....anasubiri remote itoe signal ndio afungue mdomo.

👇👇....c&p
Gangsters in Suit.

KIPARA na Maharage mwezi Machi 2023, waliagiza na kuamuru maji katika bwawa la Mtera (Catchment area; 68,000 km² (26,000 sq mi)) yafunguliwe na kumwagika nje.

Hoja yao; Maji yangelijaa sana na yangelipasua bwawa la Mtera. Wahandisi na wataalam kutoka katika bwawa la Mtera wakapinga jambo hilo kitaalam.

Wataalam na wahandisi kutoka Mtera wakawaleza hifadhi ya maji (reservoirs) kwenye Rock-fill dam hutumika kwa shughuli nyingi siyo Hydropower tu.

Hifadhi ya maji (reservoirs) kwenye Rock-fill dam (kama Mtera) hutumika hata katika irrigation, human consumption, industrial use, aquaculture, na navigability.

Lakini kwa mamlaka yao, KIPARA na Maharage wakaagiza kwa lazima maji yafunguliwe katika bwawa la Mtera. Maji yakafunguliwa.

Maji hayakujaa tena katika bwawa la Mtera, kwa sababu mvua zilipotea. Sasa nchi yetu inapitia mgao mkali wa umeme kwa sababu ya wahuni.

Septemba 2023 mgao umekuwa mkali na wanaohusika na umeme wanajitetea kwamba kuna upungufu wa uzalishaji umeme kwenye mabwawa kutokana na ukame.

Kuliko kuwahamisha kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, hawa ‘wahuni’ walipaswa kupumzika utumishi wa umma. Hawatufai.

Tunataka kuamini kwamba ‘Rais ni taasisi’ na Rais anatakiwa kuwaondoa katika utumishi wa umma hawa wahuni. Haitakiwi kuwahamisha waharibifu kutoka ofisi moja kwenda nyingine.

Wakati hawa wahuni wakisubiri nje ya utumishi wa umma, Tunahitaji uchunguzi wa kamati maalum ya bunge katika jambo hili, haraka. Ingawa lenyewe ni dhaifu.

Haiwezekani wahuni wananufaika kuingiza na kuuza majenereta wakati wengine tunapata msoto wa mgao wa umeme. Wanatutia umaskini.

MMM, Mtikila.
Haya yote yanafanyika kwasababu hatuna chama cha upinzani.

Lisdu anawlemewa wengine qote wapo kusaka tonge ndio maana wanatafuta mwafaka na ccm
 
Tuliambiwa muda mrefu Sana kuna ukarabati wa mashine je makamba na maharage walikuwa wanafanya nini muda wote huo kama bado ukarabati upo?

samia kapuyanga hapo habari za kusema mitambo haikufanyiwa service muda mrefu tumesikia tangu mwaka 2021 leo unarudia yale yale je hao vijana wako walikuwa wanaamka na kwenda kunywa chai ofisini kwa miaka miwili na nusu yote????????

Halafu leo unakuja kumtwika mzigo mhandisi wa watu na kumpa miezi 6

Ukiambiwa ukweli unasema unaziba masikio
 
Back
Top Bottom