KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Ninaijua vizuri sana, na usidhani nilipoandika hivyo sikuitambua hali hiyo; lakini husikii lugha anayotumia Samia ikitumiwa na Waziri Mkuu wa India. Huwezi hata mara moja akizungumza namna hiyo.Unajua hali ya kimaisha ya raia wa kawaida wa India na Pakistan? Hao jamaa wakipata hata nafasi ya kuja hapo TZ hawakubali tena kurudi kwao! Korea Kaskazini wana kila aina ya bomu, wanajenga na Nyuklia pia lakini asilimia kubwa ya wananchi wake wanashindia mlo mmoja! BTW hakuna nchi isiyokopa au kusaidiwa kwa namna moja ama nyingine! Kutawala ingekuwa ni majaribio natamani nyie watu mngepewa miaka 5 muongoze hii nchi tuone hizo "akili kubwa" zenu
Hata hivyo, usisahau kuwa India imo kati ya nchi za G20, au hujui maana yake ni nini?
Unasubiri India wakakope kujenga vituo vya mabasi? Hivi unaelewa unachokiandika hapa wewe? Ni wapi nilipoandika kwamba nchi "hazikopi", lakini kukopa kwenda kujenga mashimo ya choo?
Wewe nilishakueleza toka mwanzo, hilo jina ulilojipajchika haliendani kamwe na akili yako.