Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Popomalism at workTuko na mama, CHADEMA tupa kule
Suala la Mbowe ni la kisheria zaidi. Rais asiingizwe kwenye mambo yanayohusu mahakama na sheria.Ukiacha suala la Mbowe, sijawahi kuwa na mashaka na Rais Samia.
Rais Samia aachane kabisa na makandokando ya awamu ya 5, japo alikuwa humo. Tunajua alikuwa humo, lakini hakuwa na mamlaka, ndiyo maana hatumhukumu kwa hilo.
Jambo la muhimu, ajitenge na yote ya kishetani ya awamu ya 5. Asirithi uovu hata akajiv 89thunia nao. Nchi inahitaji kuponyeshwa majeraha na siyo kuyapalilia.
Tunaomba Rais Samia asimame na Mungu hata pale akiwa amezungukwa na roho za uovu, atashinda. Asiyaonee haya matendo mema hata akiwa katikati ya mamilioni ya waovu.
Tunajua, ugumu uliopo kwake, yaani utende mema na ya haki, huku ukiwa umezungukwa na wanaCCM, ambao wengi wao, kwao uovu ni ujasiri. Huko wapo watu wanaoonea fahari hata kuua, kutesa, kuteka kubambikia kesi, kupora kura, kuwanga, na kila aina ya uovu alimradi kama uovu huo unawahakikisha madaraka na fedha.
Kabisa. Rais asiingilie mihimili mingine especially Mahakama.Suala la Mbowe ni la kisheria zaidi. Rais asiingizwe kwenye mambo yanayohusu mahakama na sheria.
Endapo kuna ushahidi wa kutosha na wa haki kabisa (ambao haujaonekana mpaka sasa), basi Mbowe awajibike na uhalifu kama upo.
Lakini kama hakuna, ni vyema mahakama ikamwachia na kuiamuru serikali imlipe fidia, zikiwepo zile alizoharibiwa mali zake na wale wendawazimu wa awamu ya tano.
Hakika, AminiHuyu ndiye mama wa Taifa.
Kuna mtu nime mquote mkuu sio wewe.Jinsia sio tija wala haijawahi kuwa kigezo muhimu katika Urais sikubaliani nalo. Msingi wa hoja yangu ni kama binadamu wote ni sawa basi Urais hauna jinsia. Hoja za kusema anahuruma sio sawa. Rais ametumia busara bila mihemko. Hakuna Rais mwenye kutaka kuongoza Taifa lililogawanyika Rais mwenye busara hupenda kuongoza Taifa lenye amani na utulivu. Rais kutafuta amani kwa watu wake ni wajibu wake namba moja bila kubagua mrengo wa kisiasa. Hata katiba haijaona hiki kigezo cha jinsia kama ndio kete ya kupatia urais. umeenda mbali hata kuwachagulia watanzania rais ajae awe Tulia huu ni ufutuhi.
Rais mnyenyekevu,
Rais Mpole,
Rais msikivu
Rais mpenda watu wake wote,
Rais Msikivu
Rais Mtulivu
Rais mchamungu
Rais mahiri
Rais Shupavu
Rais Jasiri
Nimeipenda sana hii attitude ya Rais Mama Samia, sana. Na huu ndio ubinadamu tunaohitaji kama taifa. Kutofautiana kisiasa siyo uadui. Kasema vizuri sana mama, nimemwelewa kuwa kwenye ubinadamu tuko pamoja, kwenye siasa tuko kazini kila mmoja aje na itikadi yake lakini undugu uendelee. Asante mama.Binafsi na kwa Umri wangu huu sijawahi kuona Rais mnyenyekevu na mpole kama huyu ( She is so simple ever )
Kwa unyenyekevu mkubwa nawaomba na kuwasihi watanzania wote wanaopenda amani, utulivu na ustawi wa mtu mmoja mmoja tumuungeni mkono Rais wetu kwani ni hakika anatupenda sana kama Taifa,
<<<Msikilize hadi Mwisho >>>
=========
Mimi ni dada tu kwa Tundu Lissu kwa hiyo kama anakuja kwangu mimi anakuja kwa dada yake, kwa hiyo kama ana shida kama ana nini atakuja kusema kwa dada yake. hakuna tension ya kisiasa kati yangu mimi na Tundu Lissu haipo kwa hiyo anakuja kumuona dada yake, Rais wake katoka Tanzania kaja kwa hiyo anakuja kumuona.
Tunapokuja kwenye swala la ubinadamu Tundu Lissu mimi ni mdogo wangu tu kwa atakuja tutazungumza, hivyo mimi siwezi kusema sijui anakuja na nini anakuja kuna hili au kuna lile siwezi kusema mpaka nimsikilize kwa hiyo anakuja kumuona dada yake, lakini anakuja kwenye jambo la kirafiki kabisa, kama unakumbuka Tundu Lissu alilazwa Nairobi na mimi nilikwenda kumuona katika hali ya kirafiki kabisa maana Tundu Lissu ni mdogo wangu.
Tunapokuja kwenye swala la kisiasa, huku sasa ni upande wa kazi, yeye atasema ya kwake na mimi nitasimama kwenye chama changu.
Leo itajulikana lazima,Mbowe si gaidi
Huyu ndie alikuwa chanzo cha kigogo na wengineo.Tuache sifa nyingi wala hazihitaji kama mnavyohisi sio sawa na yule aliepita. Huyu ndie Rias anaeitendea kazi nafasi yake kwa busara na utashi unaotakiwa ni wajibu wake kwani kila mtanzania ni wake mpinzani na wanaotoka kwenye chama chake. Huyu ndie Rais tunamtegemea. Watu kama hawa wapo ila mihemko ya kisiasa inapelekea kupata Rais mbovu na kilitesa Taifa zima. Tusirudie makosa kama yale tena. Kulikuwa kuna shida kwenye system iliyompata Rais asiejua Taifa hili watu wote ni wake bila kubagua watokapo.
Huyu ndie alikuwa chanzo cha kigogo na wengineo.
Huyu alikuwa kikulacho ki nguoni mwako!
Katiba sasaUkiacha suala la Mbowe, sijawahi kuwa na mashaka na Rais Samia.
Rais Samia aachane kabisa na makandokando ya awamu ya 5, japo alikuwa humo. Tunajua alikuwa humo, lakini hakuwa na mamlaka, ndiyo maana hatumhukumu kwa hilo.
Jambo la muhimu, ajitenge na yote ya kishetani ya awamu ya 5. Asirithi uovu hata akajiv 89thunia nao. Nchi inahitaji kuponyeshwa majeraha na siyo kuyapalilia.
Tunaomba Rais Samia asimame na Mungu hata pale akiwa amezungukwa na roho za uovu, atashinda. Asiyaonee haya matendo mema hata akiwa katikati ya mamilioni ya waovu.
Tunajua, ugumu uliopo kwake, yaani utende mema na ya haki, huku ukiwa umezungukwa na wanaCCM, ambao wengi wao, kwao uovu ni ujasiri. Huko wapo watu wanaoonea fahari hata kuua, kutesa, kuteka kubambikia kesi, kupora kura, kuwanga, na kila aina ya uovu alimradi kama uovu huo unawahakikisha madaraka na fedha.
Jina na comment yako viko kinyume kwa nyuzi 180 au "180 degrees apart"Tuko na mama, CHADEMA tupa kule
Binafsi na kwa Umri wangu huu sijawahi kuona Rais mnyenyekevu na mpole kama huyu (She is so simple ever).
Kwa unyenyekevu mkubwa nawaomba na kuwasihi watanzania wote wanaopenda amani, utulivu na ustawi wa mtu mmoja mmoja tumuungeni mkono Rais wetu kwani ni hakika anatupenda sana kama Taifa.
<<<Msikilize hadi Mwisho >>>
===
Mimi ni dada tu kwa Tundu Lissu kwa hiyo kama anakuja kwangu mimi anakuja kwa dada yake, kwa hiyo kama ana shida kama ana nini atakuja kusema kwa dada yake. hakuna tension ya kisiasa kati yangu mimi na Tundu Lissu haipo kwa hiyo anakuja kumuona dada yake, Rais wake katoka Tanzania kaja kwa hiyo anakuja kumuona.
Tunapokuja kwenye swala la ubinadamu Tundu Lissu mimi ni mdogo wangu tu kwa atakuja tutazungumza, hivyo mimi siwezi kusema sijui anakuja na nini anakuja kuna hili au kuna lile siwezi kusema mpaka nimsikilize kwa hiyo anakuja kumuona dada yake, lakini anakuja kwenye jambo la kirafiki kabisa, kama unakumbuka Tundu Lissu alilazwa Nairobi na mimi nilikwenda kumuona katika hali ya kirafiki kabisa maana Tundu Lissu ni mdogo wangu.
Tunapokuja kwenye swala la kisiasa, huku sasa ni upande wa kazi, yeye atasema ya kwake na mimi nitasimama kwenye chama changu.
Daaah, yepi hayo?Kweli kabisa yote ya kishetani ya awamu ya tano ajitenge nayo.
Hapa mama ameeleweka vizuri tatizo ni pale atakapokutana na mizimu ya CCM iliyotukosesha katiba mpya kipindi cha Kikwete aliyeonyesha utayari wa kutuletea katiba mpya katika utawala wake, mizimu ya CCM ilipotia miguu yao tu kila kitu kilisambaratika hapohapo.