Rais Samia: Tundu Lissu ni mdogo wangu tu, mimi ni Rais na ni dada yake

Rais Samia: Tundu Lissu ni mdogo wangu tu, mimi ni Rais na ni dada yake

Binafsi na kwa Umri wangu huu sijawahi kuona Rais mnyenyekevu na mpole kama huyu (She is so simple ever).

Kwa unyenyekevu mkubwa nawaomba na kuwasihi watanzania wote wanaopenda amani, utulivu na ustawi wa mtu mmoja mmoja tumuungeni mkono Rais wetu kwani ni hakika anatupenda sana kama Taifa.




===
Mimi ni dada tu kwa Tundu Lissu kwa hiyo kama anakuja kwangu mimi anakuja kwa dada yake, kwa hiyo kama ana shida kama ana nini atakuja kusema kwa dada yake. hakuna tension ya kisiasa kati yangu mimi na Tundu Lissu haipo kwa hiyo anakuja kumuona dada yake, Rais wake katoka Tanzania kaja kwa hiyo anakuja kumuona.

Tunapokuja kwenye swala la ubinadamu Tundu Lissu mimi ni mdogo wangu tu kwa atakuja tutazungumza, hivyo mimi siwezi kusema sijui anakuja na nini anakuja kuna hili au kuna lile siwezi kusema mpaka nimsikilize kwa hiyo anakuja kumuona dada yake, lakini anakuja kwenye jambo la kirafiki kabisa, kama unakumbuka Tundu Lissu alilazwa Nairobi na mimi nilikwenda kumuona katika hali ya kirafiki kabisa maana Tundu Lissu ni mdogo wangu.

Tunapokuja kwenye swala la kisiasa, huku sasa ni upande wa kazi, yeye atasema ya kwake na mimi nitasimama kwenye chama changu.
Maneno mazuri kabisa.Mungu akupe uzima,afya,mama yetu,Rais wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu ni Rais asiyemcha Mungu anategemea nguvu za wazungu na fedha zao
 
Sasa mtu kama mie nisie mwanasiasa au kuwa na hadhi yeyote ile naweza vp kupata nafasi kama aliyopata Lissu na kueleza malalamiko yangu? Au nikiwa na kesi kama ya Mbowe unafikiri ni nani ataenda kuniombea kwa rais ili niachiwe huru?
Ndio hapo utajua kama nchi sio ya mwananchi kama wewe
 
Rais mnyenyekevu,
Rais Mpole,
Rais msikivu
Rais mpenda watu wake wote,
Rais Msikivu
Rais Mtulivu
Rais mchamungu
Rais mahiri
Rais Shupavu
Rais Jasiri
Ongeza na hili: Raisi aliyeondoa kero zote za muungano kimya kimya na Zenji yote meno nje!!!! Hadi 2025 Zenji itakuwa Dubai ya Afrika mashariki!!
 
Kazi nzuri Mama, tupo na wewe mpaka mwisho.
 
Back
Top Bottom