Rais Samia: Tutaendelea kukopa tumalizie miradi inayoendelea

busar

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2011
Posts
1,071
Reaction score
1,067
Asalam!
Rais wa JMT amefafanua kwa kina suala la mikopo ambalo limezua gumzo hasa baada ya Mh. Spika Job Ndugai kubeza suala la ukopaji.

Rais ameelezea aina ya mikopo na muda wa ulipaji vs maendeleo yanayotengenezwa. Anasema Tanzania inajipanga kivitendo kuwa kitovu cha biashara kwa ukanda wetu.

Anasema wanaodai mikopo ni tatizo inategemeana na unavotumia. Anasema tusibeze mikopo ila tuangalie faida zake.

Mh. Rais amefafanua kwa kina aina ya ukopaji wetu

Kwa mtazamo wangu amefafanua vizuri. Tumuunge mkono

======

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema zipo jitihada za kuivunja moyo Serikali kwenye Mikopo, akiongeza kuwa hakuna Nchi isiyokopa na hata Mataifa yaliyoendelea yana Mikopo mikubwa

Amesisitiza, "Tutakopa tumalize miradi ya maendeleo ili tuendelee. Ukikopa unajenga sasa kwa haraka, ukisubiri ukusanye za kwako utamaliza lini kujenga? Mradi wa Matrilioni unasubiri za kwako utaumaliza lini"

Ameongeza, "Tumekopa Mkopo wa Masharti nafuu wa miaka 20, unakudhuru nini? Maendeleo yanakuja haraka, utakusanya polepole uende ukalipe"
 
Akihutubia leo wakati wa utiaji wa saini wa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) ya Makutupora - Tabora, Rais Samia amesema mikopo sio mibaya kama itatumika vizuri.

Rais SSH akaongeza, wale wanaokosoa kuwa mikopo inaturudisha nyuma ni wale ambao hawajui maana halisi ya mikopo kwani hata nchi kubwa zinakopa na kukamilisha miradi yao.

"Hatuwezi kukamilisha miradi hii kwa pesa za ndani wala pesa za tozo, hivyo ni lazima tukope kuliko kuwakamua wananchi" aliongeza Rais SSH.

My take:
Rais kaamua kuzima maneno maneno yaliyokuwa yameanza kurushwa kutokea katikati ya nchi
 
Asalam!
Rais wa JMT amefafanua kwa kina suala la mikopo ambalo limezua gumzo hasa baada ya Mh. Spika Job Ndugai kubeza suala la ukopaji.

Rais ameelezea aina ya mikopo na muda wa ulipaji vs maendeleo yanayotengenezwa. Anasema Tanzania inajipanga kivitendo kuwa kitovu cha biashara kwa ukanda wetu.

Anasema wanaodai mikopo ni tatizo inategemeana na unavotumia. Anasema tusibeze mikopo ila tuangalie faida zake.

Mh. Rais amefafanua kwa kina aina ya ukopaji wetu

Kwa mtazamo wangu amefafanua vizuri. Tumuunge mkono
Muunge wewe na ukoo wako na siyo kutusemea wengine
 
The button is on green side - the battle is on! Time will tell....
 
"...miradi yote itaendelezwa na itamalizika kwa wakati."

"...wapo wanaoomba eti miradi hii isiishe ama kuendelezwa nasema acha wajidanganye."

"...na tutakopa popote pale ili tu tumalize miradi yote hii ya kimkakati.Bwawa kule linaendelea na pote barabara za lami zinajengwa."

Samia leo Ikulu.
 
Asalam!
Rais wa JMT amefafanua kwa kina suala la mikopo ambalo limezua gumzo hasa baada ya Mh. Spika Job Ndugai kubeza suala la ukopaji.

Rais ameelezea aina ya mikopo na muda wa ulipaji vs maendeleo yanayotengenezwa. Anasema Tanzania inajipanga kivitendo kuwa kitovu cha biashara kwa ukanda wetu.

Anasema wanaodai mikopo ni tatizo inategemeana na unavotumia. Anasema tusibeze mikopo ila tuangalie faida zake.

Mh. Rais amefafanua kwa kina aina ya ukopaji wetu

Kwa mtazamo wangu amefafanua vizuri. Tumuunge mkono
Wananchi tunamuunga mkono.
 
... mbona kila mtu anaongea lake? Spika anaongea hivi; Rais anaongea vile! Which is which? Bila Katiba ya Wananchi hatutoki; aliyepo atamaliza muda wake ataacha msala wa madeni nyuma tutaendelea kulizwa kama kawa!
 
... kilio kikubwa kimekuwa matumizi mabovu ya resources yasiyo endelevu na awamu zote hakuna ambaye aliwahi kudai anatumia mikopo vibaya which means wote walikuwa wanatumia mikopo vizuri na hata awamu ya 5 walifikia mahali wakatuhakikishia miradi yote ilikuwa kwa fedha za ndani.

Cha ajabu leo, nchi imelemewa na mzigo wa madeni (as per Speaker's statement and other sources). Ni nini kitatuhakikishia kwamba serikali yake na watendaji wake chini ya Katiba, sheria, Ilani, na chama kile kile watakuwa tofauti na watangulizi wao? Sio kwamba anaongea simply kwa sababu ana kinga ya kikatiba ya kutowajibika kesho na keshokutwa hata kama mambo yataenda ndivyo sivyo?
 
Akihutubia leo wakati wa utiaji wa saini wa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) ya Makutupora - Tabora, Rais Samia amesema mikopo sio mibaya kama itatumika vizuri.

Rais SSH akaongeza, wale wanaokosoa kuwa mikopo inaturudisha nyuma ni wale ambao hawajui maana halisi ya mikopo kwani hata nchi kubwa zinakopa na kukamilisha miradi yao.

"Hatuwezi kukamilisha miradi hii kwa pesa za ndani wala pesa za tozo, hivyo ni lazima tukope kuliko kuwakamua wananchi" aliongeza Rais SSH.

My take:
Rais kaamua kuzima maneno maneno yaliyokuwa yameanza kurushwa kutokea katikati ya nchi
Ni kweli

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
"Hatuwezi kukamilisha miradi hii kwa pesa za ndani wala pesa za tozo, hivyo ni lazima tukope kuliko kuwakamua wananchi" aliongeza Rais SSH.

Hivi kumbe deni la taifa huwa haliwahusu wananchi??
 
Akihutubia leo wakati wa utiaji wa saini wa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) ya Makutupora - Tabora, Rais Samia amesema mikopo sio mibaya kama itatumika vizuri.

Rais SSH akaongeza, wale wanaokosoa kuwa mikopo inaturudisha nyuma ni wale ambao hawajui maana halisi ya mikopo kwani hata nchi kubwa zinakopa na kukamilisha miradi yao.

"Hatuwezi kukamilisha miradi hii kwa pesa za ndani wala pesa za tozo, hivyo ni lazima tukope kuliko kuwakamua wananchi" aliongeza Rais SSH.

My take:
Rais kaamua kuzima maneno maneno yaliyokuwa yameanza kurushwa kutokea katikati ya nchi
Hatuwezi kukamilisha miradi hii kwa pesa za ndani wala pesa za tozo, hivyo ni lazima tukope kuliko kuwakamua wananchi" aliongeza Rais SSH.[emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064] KWAHIYO TOZO ZITAFUTWA?
 
Back
Top Bottom