Rais Samia: Tutaendelea kukopa tumalizie miradi inayoendelea

Rais Samia: Tutaendelea kukopa tumalizie miradi inayoendelea

Ndugai ana point tatizo haaminiki hasa ikizitangatiwa ana mgombea wake 2025. ..Mama siyo mbaya kukopa tatizo anapeleka zenji halafu wadanganyika ndio wanalipa. ...way forward bunge liwe linajadili aina ya mkopo na namna ya kulipa ikiwemo masharti ndio tukope. ..ila sasa hakuna Bunge kwahiyo tuendelee na chukua chako mapema hadi siku wadanganyika wazinduke. ...
 
Asalam!
Rais wa JMT amefafanua kwa kina suala la mikopo ambalo limezua gumzo hasa baada ya Mh. Spika Job Ndugai kubeza suala la ukopaji.

Rais ameelezea aina ya mikopo na muda wa ulipaji vs maendeleo yanayotengenezwa. Anasema Tanzania inajipanga kivitendo kuwa kitovu cha biashara kwa ukanda wetu.

Anasema wanaodai mikopo ni tatizo inategemeana na unavotumia. Anasema tusibeze mikopo ila tuangalie faida zake.

Mh. Rais amefafanua kwa kina aina ya ukopaji wetu

Kwa mtazamo wangu amefafanua vizuri. Tumuunge mkono
Ukiona mtu hamuungi mkono ajuwe sio mtanzania.Bila kukopa hakuna maendeleo.Makabila mengi ukienda kuchumbia, utaulizwa una madeni? ukisema huna madeni,huthaminiwi. Wanasema huyu, atakuja mlaza na njaa mtoto wetu, akiwa hajui kukopa.
Hakuna tajiri, wala mfanyabiashara mkubwa asiye kopa. Hakuna maskini wala mfanyabiashara mdogo, asiyekopa, binadamu anayejitambua lazima akope.
 
Asalam!
Rais wa JMT amefafanua kwa kina suala la mikopo ambalo limezua gumzo hasa baada ya Mh. Spika Job Ndugai kubeza suala la ukopaji.

Rais ameelezea aina ya mikopo na muda wa ulipaji vs maendeleo yanayotengenezwa. Anasema Tanzania inajipanga kivitendo kuwa kitovu cha biashara kwa ukanda wetu.

Anasema wanaodai mikopo ni tatizo inategemeana na unavotumia. Anasema tusibeze mikopo ila tuangalie faida zake.

Mh. Rais amefafanua kwa kina aina ya ukopaji wetu

Kwa mtazamo wangu amefafanua vizuri. Tumuunge mkono

Tokea maviongozi ya ccm yameanza kukopa hizo pesa tumefaidika na nini zaidi ya kupata sifa ya highly indebted poor country.
Mara elfu 200 tungeendelea kutambulika kama poor country isiyodaiwa.

Yaani ma CCM bwana yameshindwa kuongoza nchi bado maskini sana ila yameiongezea na madeni
 
yeye ni 'mkojani' hivyo hata akiuza Tanganyika yoote hana hasara……….
 
Akihutubia leo wakati wa utiaji wa saini wa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) ya Makutupora - Tabora, Rais Samia amesema mikopo sio mibaya kama itatumika vizuri.

Rais SSH akaongeza, wale wanaokosoa kuwa mikopo inaturudisha nyuma ni wale ambao hawajui maana halisi ya mikopo kwani hata nchi kubwa zinakopa na kukamilisha miradi yao.

"Hatuwezi kukamilisha miradi hii kwa pesa za ndani wala pesa za tozo, hivyo ni lazima tukope kuliko kuwakamua wananchi" aliongeza Rais SSH.

My take:
Rais kaamua kuzima maneno maneno yaliyokuwa yameanza kurushwa kutokea katikati ya nchi
Wananchi tunamuunga mkono Rais wetu.
 
Wanaparurana wao kwa wao. Acha mvua iendelee kunyesha tupajue panapovuja..
 
Divide and rule, akishikwa anakimbilia kwa legacy ya Magu (RIP) kusema anamaliza miradi huku Serikali yake inazima umeme, Magu akisifiwa anakuja kuchonganisha Magu aonekane mbaya na kwamba matatizo yakitokea siyo Awamu yake.

Pitting people against each other, …
 
Ndugai akimfatilia mama MDA huu[emoji4]
IMG_20210917_183745.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"...miradi yote itaendelezwa na itamalizika kwa wakati."

"...wapo wanaoomba eti miradi hii isiishe ama kuendelezwa nasema acha wajidanganye."

"...na tutakopa popote pale ili tu tumalize miradi yote hii ya kimkakati.Bwawa kule linaendelea na pote barabara za lami zinajengwa."

Samia leo Ikulu.
Reli ya umeme itakamilima 2050. Hadi leo kipande cha Dar to Pugu hakijakamilika
 
"...miradi yote itaendelezwa na itamalizika kwa wakati."

"...wapo wanaoomba eti miradi hii isiishe ama kuendelezwa nasema acha wajidanganye."

"...na tutakopa popote pale ili tu tumalize miradi yote hii ya kimkakati.Bwawa kule linaendelea na pote barabara za lami zinajengwa."

Samia leo Ikulu.
Nimepita mbagala naona watu wamepiga usingizi maana hakuna kinacho endelea
 
Back
Top Bottom