evangelical
JF-Expert Member
- Nov 21, 2011
- 5,035
- 8,218
Madeni hatujawahi kuweza kuyalipa ya ndani yametushinda ya huko nje hadi huwa tunapiga kelele wabeberu wayasamehe/wayafute
TRA kule zanzibar wanazileta bara ndio mnakula huko milo 3.,Ndugai ana point tatizo haaminiki hasa ikizitangatiwa ana mgombea wake 2025. ..Mama siyo mbaya kukopa tatizo anapeleka zenji halafu wadanganyika ndio wanalipa. ...way forward bunge liwe linajadili aina ya mkopo na namna ya kulipa ikiwemo masharti ndio tukope. ..ila sasa hakuna Bunge kwahiyo tuendelee na chukua chako mapema hadi siku wadanganyika wazinduke. ...
Samia anatufanya sisi vifaranga vya kukuHatuwezi kukamilisha miradi hii kwa pesa za ndani wala pesa za tozo, hivyo ni lazima tukope kuliko kuwakamua wananchi" aliongeza Rais SSH.[emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064] KWAHIYO TOZO ZITAFUTWA?
Anayeambiwa ni Job & co, sasa job analipa kodi gani na wapi?Kaanza Mipasho ?
Hao wapiga ramli hawalipi Kodi ?, Kama wanalipa sio wabezwe bali tujaribu kuwaelewesha na kama bado wanapinga tujiulize kwanini na tushindane nao kwa hoja...
Mapumbavu na mashetani kabisa haya majitu. Yanatufanya sisi wananchi mazuzu.
Yanakopa hayalipi halafu yanaondoka madarakani inabidi utaratibu ufanyike kila rais akimaliza madaraka asiache deni lake.
Nchi inadaiwa tirion 70 halafu bado maskini? Huu ni upumbavu
Asalam!
Rais wa JMT amefafanua kwa kina suala la mikopo ambalo limezua gumzo hasa baada ya Mh. Spika Job Ndugai kubeza suala la ukopaji.
Rais ameelezea aina ya mikopo na muda wa ulipaji vs maendeleo yanayotengenezwa. Anasema Tanzania inajipanga kivitendo kuwa kitovu cha biashara kwa ukanda wetu.
Anasema wanaodai mikopo ni tatizo inategemeana na unavotumia. Anasema tusibeze mikopo ila tuangalie faida zake.
Mh. Rais amefafanua kwa kina aina ya ukopaji wetu
Kwa mtazamo wangu amefafanua vizuri. Tumuunge mkono
======
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema zipo jitihada za kuivunja moyo Serikali kwenye Mikopo, akiongeza kuwa hakuna Nchi isiyokopa na hata Mataifa yaliyoendelea yana Mikopo mikubwa
Amesisitiza, "Tutakopa tumalize miradi ya maendeleo ili tuendelee. Ukikopa unajenga sasa kwa haraka, ukisubiri ukusanye za kwako utamaliza lini kujenga? Mradi wa Matrilioni unasubiri za kwako utaumaliza lini"
Ameongeza, "Tumekopa Mkopo wa Masharti nafuu wa miaka 20, unakudhuru nini? Maendeleo yanakuja haraka, utakusanya polepole uende ukalipe"
Taarifa ni kuwa Dodoma bado haijakamilika ujenzi.Kama anakopa na speed ya ukamilishaji miradi ionekane,kwa maana miradi ikamilike kwa wakati!! Hapo hatutakuwa na nongwa!!, kwanza huko dar wanamdanganya Sana,arudi huku ikulu ya nchi iliko Dodoma,mbona anang'ng'ana na daisalama!!??, kituo Cha kazi yake Kiko Dodoma,yeye anang'ang'ania kukaa nje ya kituo chake Cha kazi, si utovu wa nidhamu ya kazi huu!!!
yeye ni mtumishi ,sawa na watumishi wengine,mbona waalimu, ma nesi n.k wanalazimishwa kubaki kwenye vituo vyao vya kazi!!?, arudi kituo chake Cha kazi,aachane na huo mji wa daisalama!! Ebo!!