Nilisha kueleza tokea wakati ule mlipoweka upotoshaji wa uhusika wa nchi hiyo jirani katika ujinga wenu huu, kwamba, unapotaka kumhusisha mtu unayejadili naye na mambo yanayohusiana na hiyo nchi, jaribu kwanza kuangalia msimamo wa mtu huyo na hiyo nchi.Unaona aibu tu kushikilia uwekewe vifungu vile vile kwani kipindi chako cha mtandaoni na yule mkenya kilibuma na kukugeuka.
Haukujua kuwa Tanzania imejipanga sana kwenye suala hili la uwekezaji, ujuaji umekujaa kiasi cha kudhani unajua kitu kuliko wanasheria wabobezi waliokupa shule ya bure wewe na wasaliti wengine wenye hulka kama za kwako.
Ukitaka kuniunganisha mimi na hiyo nchi jirani, siyo kazi ngumu hata kidogo kuangalia nilichowahi kuandika humu JF kuihusu nchi hiyo. Yamo mengi sana niliyokwishajadili kuihusu nchi hiyo, na hata bandari zao humu humu JF.
Sasa wewe, unapokuja hapa na kudai tu, kuwa ninashikiwa akili na huyo mtu, unajionyesha ujuha wako ulipo.
Mmetapatapa sana kutafuta njia za kuwadanganya watu juu ya jambo hili, na zote zimeshindikana, lakini hamkomi kuendelea na ujinga huo huo. Akili ya aina hii tuiite akili ya namna gani, ya kichizi?