Samia anayaogopa maandamano maana ameshaona hiyo ndio itakuwa njia ya mwisho kumzibua masikio yake, ili atusikie tukimwambia ule mkataba wa bandari ni mbovu unaomkandamiza mtanganyika na kuidhalilisha ardhi yetu, utu wetu, na mipaka yake, ameyataka mwenyewe kwa ukaidi wake.
Sasa ameona ayaweke maandamano kundi moja na vikundi vya kigaidi, hajui maandamano yapo kisheria, hiyo ni haki ya mtanganyika, kama anajua vilipo hivyo vikundi vya kigaidi aliagize jeshi la polisi likavikamate, asipoliagiza jeshi maana yake anafumbia macho vikundi vya kihalifu, hatufai.
Lakini asijaribu kutuchezea "mind games" ili kupunguza nguvu za kuzidai bandari zetu zote waTanganyika walizopewa waarabu, kwa huu mpango wake amefeli tayari, muhimu namshauri tu aliagize jeshi la polisi litoe ulinzi kwa waandamanaji hiyo siku ikifika, sasa ndio anavuna matunda ya ukaidi wake mwenyewe.