Rais Samia: Uchumi wetu unakua lakini tunachokusanya kingi kinaingia mifukoni kwa Watu

Halmashauri nyingi hazikusanyi mapato ipasavyo.Makadirio/maoteo yao yapo chini ya nusu.Waache wizi.
 
Kwahiyo!!!??? Yaani inakera sanavkuona wezi wa kuku huku mitaani wanashughulikiwa ipasavyo na vyombo vya dola. Lakini unajiuliza wezi kama hawa kwanini hawachukuliwi hatua? Mh Rais hadi akatamka maana yake ushahidi anao kulingana na taarifa zinazotolewa na wasaidizi wake. Tutegemee kuona anawachukulia hatu stahiki.
 
Ningelitamani walipa Kofi ndiyo wangalipewa haki ya kuchagua Raid na wabunge maana ndio wenye uchungu na nchi yao
 
Mwigulu analiwa kichwa vere soon.

Pole mkuu
 
I
Punguzeni mishahara, posho na marupurupu ya wanasiasa (wabunge) na baneni matumizi kwa kupunguza safari zisizo na ulazima na kuondoa makongamano yasiyoisha kila uchao
Hili likitekelezwa ndilo tiba. Ila sasa ni Nani ataagiza hivyo !
 
"Kuleni kila mtu kulingana ulefu wa kamba Yako."
 
Ndio vinaongeza Kodi vikipungua? Kinachotakiwa Kila mtu alipe.kodi stahiki
Havitaongeza lakini itapunguza sana fungu la matumizi ya kawaida ambalo hutumika kulipa mishahara, posho na mengineyo tofauti na mafungu ya mfano maendeleo. Huku tukitafakari namna ya kupanua wigo wa walipa kodi nafikiri watunga sera/sheria hawana budi kuja na mikakati kabambe kama vile kupunguza viwango vya kodi (VAT, Kodi ya makampuni-Corporate tax nk) ili kila mtu aweze kumudu kingine nafikiri ni kutafuta namna ya kuwajumuisha wafanyabiashara wadogo (machinga) hata kama watalina kidogo lakini kwa idadi Yao wataongeza mapato kuliko kutolipa kabisa hapa inabidi watafutiwe utaratibu wa kulipia kila tuseme miezi 6 au kwa mwaka.
 
Juzi nilimsikia pm akihoji makatibu kuchota posho ya 44 m kwa siku moja ka honoraria nikataka kuzimia nikadhani pm kakosea lakini ukweli kodi za wananchi zinatumka vibaya na viongozi
Hakika zinachotwa kweli sio kipolepole sasa kamą nidhamu hakuna kwenye matumizi ya serikali lazima fuko liishiwe tu
 
Matumizi mabaya ni kama yapi?
 
Hadithi za kuvuka malengo huwa ni kisiasa zaidi ili kupambisha lakini ukweli wa mambo unajulikana pesa haipo wazabuni/wakandarasi hasa wa ndani wengi wao wamekopwa hawajalipwa mpaka hivi leo na haijulikani watalipwa lini unajiuliza wanaendeshaje makampuni yao na kodi watalipa vipi ikiwa hawalipwi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…