Rais Samia: Uchumi wetu unakua lakini tunachokusanya kingi kinaingia mifukoni kwa Watu

Rais Samia: Uchumi wetu unakua lakini tunachokusanya kingi kinaingia mifukoni kwa Watu

Soma thread yangu iliyopita nimeanisha jana/juzi PM alikuwa anahoji watumishi kulipana posho/honoraria pesa kedekede
Posho tuu? Mbona vihela vidogo hivyo? Kwa vimishahara vya Watumishi posho ni sawa wakilipana
 
Hili amelijua lini na amechukua hatua gani Kama kiongozi na amiri Jeshi mkuu ?
 
Akisema hivyo inatusaidia nini kama taifa? Yeye ndio namba moja afanye kwa vitendo tumechoka porojo!
 
Hio mikono ya watu ni kina nani na anafanya nini ili kuepukana na hilo ? (Hivi hizi Control Number zinafanya nini) unless hio mikono ya watu ni huko juu alipo yeye...

Na sisi tunaokamuliwa hatuoni value for money kitaa..., By the way nilitegemea suluhisho kutoka kwake na sio malalamiko (ila what would you expect from a politician)
 
Rais Samia Suluhu akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi, amesema kuwa kodi tunayokusanya hailingani na idadi ya watu.

“Uchumi wetu unakua sana, lakini haulingani na tunachokikusanya. Tunakusanya kidogo sana, kingi kinaingia mifukoni kwa watu bure bure tu. Shughuli za kiuchumi zinazoendelea nchini na idadi ya watu hailingani na mapato tunayoyapata.”

My Take: Naunga mkono hoja, na huu ndio ukweli. Ukiangalia utajiri wa Watu na miradi wanayofanya na kile tunapata ni vitu 2 tofauti.

Serikali inawaonea Watumishi tuu ambao hawawezi kukwepa Mapato lakini huko Mitaani wafanyabiashara wanalipa robo ya wanachostahili au wanakwepa kabisa.👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DAsmS5qq-x9/?igsh=aG50bzc5ajJ2dGZm


Pamoja na Kulalamikia kwamba watu ni wengi ila hawalipi Kodi ni lazima ujue kati ya hao watu mil.65 ,,ukiondoa under 18 na maskini,wanafunzi,wazee Je Nguvu kazi halisi ni kiasi gani?

View: https://www.instagram.com/p/DAsoqL_KoP5/?igsh=aHlmaGJlMWlmMXE0

Soma hapa: LIVE - Rais Samia akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi Ikulu - Dar, Oktoba 4, 2024


Kauli kama hii angesema mtu wa upinzani
Mngekuja speed kutetea na kuona wanapinga kazi mzuri ya Rais

Haya sasa Leo kasema mwenyewe, wale wazee wa mama anatosha mitano tena mnasemaje? 😂
 
Alisharuhusu watu watafune kwa urefu wa kamba zao
 
Akisema hivyo inatusaidia nini kama taifa? Yeye ndio namba moja afanye kwa vitendo tumechoka porojo!
 
Mambo mengine ni ujinga unapouliza..hivi kampuni za telecoms kwa nini haziko kwenye walipa kodi watatu bora kitaifa?? kampuni ina customer base millioni 16 ina wafanyakazi hawazidi 300 lakini hawamo kwenye tatu bora! halafu serikali wakiongea wanajifanya hamnazo kabisa wakati ukweli uko wazi mtu yeyote mwenye uelewa atauona..au kuna kutradeoff kwamba tukupe kodi kdg halafu tutakuwa tunakupa taarifa za wateja wakati wowote unapotaka! kwa nini vodacom si mlipa kodi bora??? hata pale mwenzake safaricom alikuwa mlipa kodi bora mfululizo huko anakofanyia biashara tena akiwa na customer base watu million 6 tu..halafu anakuja mtu anauliza kinachokusanywa hakiendani na uhalisia, ts peculiar..!
 
Juzi nilimsikia pm akihoji makatibu kuchota posho ya 44 m kwa siku moja ka honoraria nikataka kuzimia nikadhani pm kakosea lakini ukweli kodi za wananchi zinatumka vibaya na viongozi
Ndio maana hatutaki kulipa!
 
Rais mwenyewe halipi kodi pamoja nakua na mshahara mkubwa stili bado halipi kodi si hatari hiyo
 
Back
Top Bottom