saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 4,683
- 7,222
Mama yangu Rais Samia kwanini mkataba moja huu wa bandari utumie nishati kubwa namna hii. Huu ni mkataba moja tu je utaweza kufanya chochote km kiongozi mkuu wa nchi? Nachoogopa kwa kuwa uelewa wa watu bado ni mdogo ndio mtawachanganya zaidi. Bunge limeshapitisha, na bunge ni wawakilishi wa wananchi kuna nini usiendelee na utekelezaji. Labda kama kuna kitu kweli mnakificha, vinginevyo utaonekana rais dhaifu asiyeweza kuiendesha nchi, asiye na msimamo ktkt maamuzi yake.
Kuna kipindi ktk uongozi wa Kikwete alikuwa ameingia mikataba na makampuni ya utafutaji na uchimbaji madini kule mikoa ya Lindi na Mtwara. Ila kuna watu wakiwepo wabunge wa kule kusini walianza chokochoko kwamba gesi yetu haitoki. Rais Kikwete alisimama imara kama mkuu wa nchi, kiongozi mkuu wa serikali na amiri jeshi mkuu na jambo lile lilidhibitiwa na likapotea bila taarifa. Wale watu walitaka kuigawa nchi na kuleta ubaguzi kama wanavyofanya hawa wa sasa. Kilicho mbele yetu ni mkataba tena moja tu watu wameanza na hoja ya utanganyika. Bado unafikiri lengo ni mkataba? Sasa km mkataba moja unaleta haya yote utaweza kuingia mikataba mingapi wakati shughuli zote za uwekezaji zinahitaji mikataba.
Rais jambo hili liishe muende kwenye hatuna zinazofuata kazi ianze. Shughulikia wanaotaka kutuharibia nchi we ndio kiongozi mkuu kwa sasa.