Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi
Rais Samia ambaye ni Rais Mwanamke wa Kizanzibari mwenye lugha tamu laini na lafudhi ya Kizanzibari, yenye maneno na vineno, vitamu hadi raha kumsikiliza haku ukitamani asimalize kuzungumza.
Leo kwenye maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa habari, Rais Samia katamka maneno haya
"Ukinikuna Vizuri, mimi nakukuna huku nnakupapasa tena na kukupuliza ufu ufu ". Lakini "Ukinipara...Nakuparura!" - Hivi Vijineno!, Japo Vitamu Hadi Raha Kusikiliza!.
Hili ni onyo la kiana kwa vyombo vya habari, tujitahidi kumkuna Mama ili na yeye atukune, na atupapase. Tuepuke kumpara, asije kutuparura!. Ikitokea Mwandishi wa habari akampara Mama, no one knows huko kumparura, style ya Mama ya kumparura ikoje!. Kule nyuma aliwahi kutoa onyo kama hilo kuwa "ukimzengua, tutazenguana", Leo ni "ukinipara, nitakuparua!. Kwa vile no one knows uparuaji wake, unaweza kuwa mchungu kuliko Shubiri, hivyo natoa wito kwa waandishi wenzangu wa habari
1. Waandishi wanaopenda kukunwa na kupapaswa, waendelee kumkuna ili awakune na kuwapapasa.
2. Sisi waandishi wapara, tujitahidi sana kumpara kwa taratibu sana ili alone ni unamkuna, tusije mpara kwa nguvu Mama, akatupara hivyo Shubiri, tutaionja.
3. Wale waandishi ma konki ambao hawaogopi shubiri, ikitokea jambo la kumkuna, tutamkuna, lakini likitokea la kumpara, tutampara kwasababu ni waandishi wanao mpara ndio watamsaidia kuliko wanao mkuna!. Tulifanya hivyo kwa watangulizi wake, tutafanya hivyo kwake ili kumsaidia!. Kumuenzi Magufuli: Tujikumbushe 'spana' za JF zilivyomsaidia Hayati Magufuli na Taifa. Je, Samia pia tumsaidie kwa 'spana' au tumkune tu tusimpare?
Happy Press Freedom Day.
Paskali
Mabandiko mwendelezo