Rais Samia: Ulaya na Marekani hawafanyi vizuri kiuchumi kama sisi

Watu wenyewe wanaohutubiwa huo mkutano wanaelewa chochote kuhusu siasa za kidunia ukiachilia mbali siasa za kikanda. Zaidi ya mechi za Simba na Yanga na kubet watapiga makofi .... 😳
 
Uchumi unakua na mambo yanazidi kuwa magumu, yanamwelemea na hataki kuachia kamna. Deni la taifa limefika trillioni 107. Siku huyu mama atakapotoka madarakani mwaka 2030 deni litakuwa Trillioni 200
Kiongozi wa hovyo kuwahi kutokea
Deni Hupimwa Kwa Gdp, debt to Gdp ratio.

Uchumi wetu unakua kuliko deni hicho ndio cha muhimu, mwaka huu debt to Gdp ratio itashuka toka 48.3% mpaka 47% na inakadiriwa hadi 2030 itashuka hadi 40%


Mfano rahisi ambao layman anaweza kuelewa.

Wewe una milioni 5, ukaenda ukakopa milioni 3 ukazungusha ukawa na milioni 10, ukakopa tena milioni 3 deni likawa milioni 6 ila ukazungusha ukawa na milioni 15 etc so deni linaongezeka ila pato lako limeongezeka zaidi.
 
Samia azuiwe kutumia pombe kabla ya kutoa hotuba au tamko lolote kuhusiana na mustakabali wa nchi, mental health is real.
Anatembelea biti za Msukuma huko usukumani.... Kenya hawatuzidi kwa lolote!.😎
 
Mama amesema kweli kabisa.
Atufungulie Busisi hapo tupite sie kwa kuteleza.
Mambo mengi muda mfupi..
 
Hivi jambo la kujitegemea ni controversy kwamba liwe ni la Samia ama la nchi? Si ni jambo kila mwananchi anatakiwa ku strive? Kesho na keshokutwa mkipewa misaada msupport ushoga mtaanza kulalamika.

Issue ya kukopa nimeelezea comment ya juu

2001 Gdp to debt ratio ilikua zaidi ya 50% hapo ndio tulikua na Deni kubwa kupata kutokea nchi yetu kutokana na uwezo wetu wa kulipa.
 
Kukopa ni harusi, kulipa ni matanga!. Hata kama tunakopesheka, utaratibu wa kulipa uko vipi? Au ni kuusukuma mzigo huo wa deni kwa watoto wetu na rasilimali za taifa kama rehani?😳
 
Wawe wamesema ama hawakusema will that change data? Mbona mnataka kila kitu kukifanya siasa?
Context ilikua kwa Sasa, as if huko zamani hatukua na ukuaji kama huu kuliko marekani kulingana na muktadha wenu.
Ilipaswa basi aseme kwa miaka mingi uchumi wetu umekua vizuri kuliko marekani, maana hakuna mwaka marekani wametupa toka enzi ya kikwete
 
How? Inter trade Africa Mashariki tumezipita nchi zote, Makusanyo yetu sasa hivi ni makubwa to the point tunakaribia kubalance Trade na kutomtegemea mtu, kilimo, dhahabu, Utalii vyote vimeongezeka maradufu etc.
Acha uongo deni mwaka wa fedha limekua almost Trillion 10+
Yaani uwe na mapato mazuri alafu uwe kinara wa kukopa science ya wapi kwa sababu kama una makusanyo mazuri kwanini ukope
 
Kukopa ni harusi, kulipa ni matanga!. Hata kama tunakopesheka, utaratibu wa kulipa uko vipi? Au ni kuusukuma mzigo huo wa deni kwa watoto wetu na rasilimali za taifa kama rehani?😳
Kama umekopa milioni 3 ikarudisha milioni 5 hilo sio janga kwa vizazi vya baadae sababu umeingiza kingi kuliko ulichokopa, na jinsi unavyoingiza kingi na kukusanya mapato ndio jinsi unavyokua na mapato makubwa na ndio jinsi deni linalipika. Mfano mwaka huu bajeti ya kulipa deni ni Trilioni 14, mwaka jana Ilikua ni Trilioni 13 etc
 
Acha uongo deni mwaka wa fedha limekua almost Trillion 10+
Yaani uwe na mapato mazuri alafu uwe kinara wa kukopa science ya wapi kwa sababu kama una makusanyo mazuri kwanini ukope
Weka data zako hapa na ulipozitoa kama vile ambavyo mimi nimeweka data zangu.
 
Context ilikua kwa Sasa, as if huko zamani hatukua na ukuaji kama huu kuliko marekani kulingana na muktadha wenu.
Ilipaswa basi aseme kwa miaka mingi uchumi wetu umekua vizuri kuliko marekani, maana hakuna mwaka marekani wametupa toka enzi ya kikwete
Si Kweli, miaka mingine Usa anatupita, 2021 tu hapo ukuaji wao USA ulikua ni 6% na sisi 4%
 
Hicho kingi kinachoingia kupitia mikopo kinatumikaje hata kama tunapanga kulipa Trillion 14 mwaka huu? Vipi huu ukuaji wa deni, unaenda sambamba na ongezeko la watanzania ? Hizi nadharia za kutoana wasi wasi zinatofauti gani na zile porojo za kuepuka dhambi ili uishi maisha mazuri baada ya kifo?
 
Sawa tukopeshe nchi zingine basi.
Ukiwa maskn ukapata kiwekeza milion 1 na ikazaaa 500k utasema uchumi umekua kwa asilimia 50 haya ina maana mwenye bilioni uchumi wake ukakua kwa 2% mtakuwa sawa kweli. ? Huyu nyama anakulaga gambe au cha chuga wazee
 
Sa
sawa
 
Hivi jambo la kujitegemea ni controversy kwamba liwe ni la Samia ama la nchi? Si ni jambo kila mwananchi anatakiwa ku strive? Kesho na keshokutwa mkipewa misaada msupport ushoga mtaanza kulalamika.
Chawa..🚮🚮
 
Huyo baba Mwajuma atakuwa ni Kafulila maana ndio mshauri wake mkuu kwenye mambo ya uchumi wa IFM na WB ... 🤔 Aibu tupu!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…