Rais Samia umekosea tena; haupo kwa ajili ya kuongoza wanawake, bali kuongoza Watanzania wa jinsia zote

Rais Samia umekosea tena; haupo kwa ajili ya kuongoza wanawake, bali kuongoza Watanzania wa jinsia zote

Hivi Samia anazisoma kweli jumbe zetu hapa jf?
Naamini kama angekuwa anazisoma angebadilika japo kidogo maana hapa pndo centre ya GT.

Mama kama hufuatilii jf kutokana na majukumu nakuomba upatiwe mtu kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali hapa jf ambazo zitakusaidia katika kufanya maamuzi (baadhi).
 
Mama Samia Leo nimeona umekosea tena Jambo ambalo umekuwa ukilikosea toka mwanzo.

Ma Samia wewe ni Rais wa JMT, hivyo jinsia, ukabila, dini au rangi uliyo nayo haina uhusiano na urais wako...
Mwambie samia kuwa Joyce Banda alipoapishwa kuwa Rais baada ya kifo cha Mutharika wengi walipata matumaini, lakini alibadilika,alianza kutumia jinsia yake kupata uhalali wa kisiasa, alitesa wapinzani na 2014 akashindwa uchaguzi akakimbia nchi huku waziri wake aliyetumika kuwatesa wapinzani akijiuwa
 
Nadhani Sio SAHIHI kusema AWAMU ijayo ni zamu ya MWANAMKE kuwa RAIS.

URAIS kwa Mujibu wa KATIBA Haijabainisha hivyo kuwa URAIS uwe wa Kubadilishana kwa JINSIA.

Kama tutaanza Kumtafuta RAIS Kwa JINSIA badala ya SIFA zilizopo kwenye KATIBA kuna SIKU Tutasema Safari hii RAIS atokane na KABILA Fulani au DINI Fulani.

Tutafute RAIS kwa Sifa zilizobainishwa kwenye KATIBA na SIO JINSIA YAKE.
 
Tunakoelekea ni kigumu sana, mgawanyiko utatuandama na kuweka mambo sawa itatugharimu sana
 
Mama Samia Leo nimeona umekosea tena Jambo ambalo umekuwa ukilikosea toka mwanzo.

Ma Samia wewe ni Rais wa JMT, hivyo jinsia, ukabila, dini au rangi uliyo nayo haina uhusiano na urais wako....
Taifa lisiwe tayari kutoa nafasi kwa mtu asiye na uwezo awe rais kwa kua tu ni mwanamke. Tutakua tumekosea sana. Mwaka ule 2015 lowassa alikuja na propaganda eti ni zamu ya walutheri akapigwa chini vizuri. Hizi siasa za samia eti zamu ya kinamama zitatupotezea muda na kuruhusu waovu kurudi ulingoni.
Tutapotezwa focus kama chama na kama nchi.. Badala ya kuendeleza sera za usawa kwenye uchumi kwa kuweka kipaumbele kwenye kuinua maslahi ya umma fisadi watachipuka upya kudhibiti mambo yote huku samia akihangaika kuwapa kina mama vyeo bila kuwepo tija.
 
Watu mahiri wa kutoa hotuba kama Barack Obama wamekuwa wakiandikiwa hotuba na wanazisoma na kujiandaa na hotuba. Na hao ni wazoefu wa global stages, anajua maneno yake yanafuatiliwa dunia nzima na yanatakiwa yaakisi sera ya nje ya Marekani. Lakini wanajiandaa na wanafanya rehearsal!

Huyu Mama ni kasoro ambazo kama mkuu wa nchi anatakiwa wasaidizi wake wafanye kazi yao vizuri. Naona hapo ndio kuna pengo linaonekana kila wakati Mama akihutubia. Kila akitaka kufafanua au “kuchomekea” yasiyo kwenye hotuba anatoa controversial statements zinazozua mijadala na zaidi ku-question “uwezo” wake.

Wasaidizi wa Mama ni vizuri mkafanya kazi yenu maana Mama anaongea kama Rais sio kama Samia. Ni vizuri kujua tofauti ya hizi nafasi mbili.
 
Na ngonjera zake kila akisimimama anazungumzia wanawake

Wanawake hivi,wanawake vile !!!!!!?[emoji15]

Next time tutafikiria Sana kuwapa wanawake nafasi za juu za uongozi.

Juzi Kati hapo mwaka Jana nilikuwa ofisi moja hivi nafanya kazi zangu nimeconcentrate kweli kweli kumbe ilikuwa siku ya wanawake.

Nikashangaa ofisi wamekuja ghafla wamejaa eti wakanitimua waanze kuambia nyimbo zao[emoji1787][emoji1787][emoji1787] hopeless kabisa

Unajua nyie wanawake sometime mambo yenu bhana yanachekesha

Anyway akumbushwe yeye ni rais wa Tanzania sio wanawake
 
Na ngonjera zake kila akisimimama anazungumzia wanawake

Wanawake hivi,wanawake vile !!!!!!?[emoji15]...
Mi ni mwanamke.
Sijui kwanini sipendi vitu vya wanawake.
Sijui nini nini kwa wanawake.
Sijui kwa vile mimi mwanamke
Sijui nini waachiwe wanawake.
Sipendi Haka kamserereko KANAPUMBAZA SANA WANAWAKE KUFANHA VITU KWA MISULI ,UTASHI NA NGUVU NA KARAMA WALIZOAJAALIWA.

wanawake this wanawake that.
Sasa na Urais ni zamu ya wanawake.

Sisemi awe mwanaume.
Sisemi pia awe mwanamke.

Bali AWE MTU ANAYESTAHILI KUTUONGOZA!!.
Nitakuwa wa kwanza kumpinga,iwapo hoja mezani ni zamu ya wanawake.
 
Mama Samia Leo nimeona umekosea tena Jambo ambalo umekuwa ukilikosea toka mwanzo.

Ma Samia wewe ni Rais wa JMT, hivyo jinsia, ukabila, dini au rangi uliyo nayo haina uhusiano na urais wako...
Umenena vema kabisa. Usawa wa kijinsia ni pale ambapo hatumchagui mtu kwa jinsi yake au maumbile yake, bali kwa weledi wake. Tunapinga mfumo dume na/au mfumo jike unaobagua!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Mama Samia Leo nimeona umekosea tena Jambo ambalo umekuwa ukilikosea toka mwanzo.

Ma Samia wewe ni Rais wa JMT, hivyo jinsia, ukabila, dini au rangi uliyo nayo haina uhusiano na urais wako...
Inabidi atengue kitendawili cha Freeman Mbowe. Kwa hili ameingizwa 18. Na anayepiga penati ni mtu mzoevu. Ile mood ya uchaguzi wa 2025 unaanzia kwenye uchaguzi wa chama. Moto wake unachoma kama pasi.
 
Back
Top Bottom