Rais Samia unatupa wakati mgumu wanachama wa CCM

Rais Samia unatupa wakati mgumu wanachama wa CCM

Pole sana kwa maoni yako

Ninachojua mimi ambacho ndio ukweli ni kwamba majukumu ya kiutawala hayafanywi na kiungo cha uzazi (ke/me) ila yanafajikishwa na akili, hekima, uweza, uzoefu, elimu na ujuzi wa mtu awe mwanamke au mwanaume.

Halafu nikukumhushe tuu kwenye siasa mimi Sijawahi Unga mkono popote tukashindwa.

Rejea mijadala historia ya harakati za siasa ndani na nje ya nchi walau kwa miaka 15 utanielewa sana.

Na sasa nakuambia October tuna uhakika wa kushinda kwa kishindo toka kwa Rais mwenye jinsia ya kike
Umeanza tena ,mama D kamdomo huponza sana
 
Mimi nina kadi ya muda mrefu.

Marekani nchi iliyoendelea kuliko zote duniani, nchi ambayo mwanaume anaweza kubadili jinsia, akakimbia mke na watoto na jamii ikamkubali.

Nchi hii kwa mara ya pili mfululizo imekataa kuwa na rais mwanamke. Wameona bora shetani kuliko mwanamke mara zote mbili. Sio kwamba Trump anapendwa sana, alishindwa na Biden mwaka 2020 tena akiwa rais.

Tanzania sisi wa mwisho kila kitu na chama changu ccm tunataka kuwaaminisha watanzania kwamba mjita wa mkoani Mara atampigia kura rais mwanamke tena anaevaa ushungi?

Wasukuma jirani zangu wazee wa wanawake weupe kweli watampigia kura mwanamke?

Wazee wangu wayao wa Songea, watu wa kuoa wake hadi wa 4 kweli wataenda kumpigia kura mwanamke awaongoze?

Imetosha CCM, tumeweka historia tayari.
Miaka mitano ni mingi mno, damage itakua kubwa mno.

Si twezi utu wala sibezi uwezo wa Dr Samia, ila tuwe wakweli.

Tanzania bado sana.

Kidumu chama cha mapinduzi.
Mimi kwangu jinsia sio hoja. Hoja ni itikadi. Samia sio mjamaa na ni mtu mpenda mali na mbinafsi. Karibu auze bandari zetu zote kwa dubai. Hiyo DP sijaamini kuna tija bali naona itakwaza maendeleo yetu kujitegemea na watatuibia kushirikiana na wahuni. Pia sera za PPP watakuja wahindi wezi tu. Hata huko marekani wameshitukiwa.
 
Vipi Marekani?
Mgombea alisukumizwa bila kuniandaa, Marekani sio wajinga kwamba mtu ateuliwe ndani ya miezi 3 awe Rais tena ashindane na Rais wa zamani ambae alijiandaa kuwa Rais Toka siku ya kwanza.

Wataendelea kusimamisha wagombea na Kuna siku watashinda,maana sio kweli kwamba Democrats wao ni wajinga kuliko nyie.
 
Samia ana kismati hata kama Ni mwanamke. Wewe ungejua Baada ya COVID nchi nyingi zilipatwa msukosuko wa uchumi watu wakapatwa na changamoto za akili, maandamano, nchi za ulaya zikaondoa viongozi, ila Rais Samia Kwa kismati Chake ndio akawa kama kaingia wakati wa neema so, ngoja uchumi wa Dunia ukae vzr utaona itakuwa mara kumi ya sasa.
 
1.Samia anajenga hactarws 500k za umwagiliaji Nchi nzima,na Bajeti ya 1.2 wengine wamewahi fanya?

Nionyeshe nataka twende kimoja baada ya kingine.Na nataka ushahidi Mimi ninazo nitakupa hapa.
Mradi wa SGR wenyewe umejifia waturuki wameondoka site kumebaki maghofu tu .
 
Samia ana kismati hata kama Ni mwanamke. Wewe ungejua Baada ya COVID nchi nyingi zilipatwa msukosuko wa uchumi watu wakapatwa na changamoto za akili, maandamano, nchi za ulaya zikaondoa viongozi, ila Rais Samia Kwa kismati Chake ndio akawa kama kaingia wakati wa neema so, ngoja uchumi wa Dunia ukae vzr utaona itakuwa mara kumi ya sasa.
Ndugu yangu, sisi hatujawahi kuwa vizur kiuchumi.
 
Mengine yapi? Mfano mwingine ni Rais gani aliyenunua CT scans Hospital za Mikoa yote Tanzania,MRI Hospital zote za Kanda Tanzania Toka ipate uhuru tofauti na Samia?

Namba za Samia hazilingani na takataka mwingine yeyote.
Kuna rais mmoja ambae alikuja na practical approach, JPM. No offence kwa pres samia, but jpm alianzisha mwngine yalikuwa on motion. Leo hii yanaitwa ya rais fulani
 
Kuna rais mmoja ambae alikuja na practical approach, JPM. No offence kwa pres samia, but jpm alianzisha mwngine yalikuwa on motion. Leo hii yanaitwa ya rais fulani
Aliyofanya huyo JPM wako hayakuwa kwenye motion?

Magufuli aliyeshindwa Hadi Ajira atapata wapi hela ikiwa wafanyabiashara walikimbia?

Hakuna Rais wa kumfikia Samia Kwa lolote na Kwa sekta yeyote.

View: https://x.com/TaruraTz/status/1875562845984997476?t=0O2fmqNhyEvCr7x_vS3L9Q&s=19

Samia atakuwa anaonesha kazi hapeleki maneno matupu.
 
Back
Top Bottom