Rais Samia; Urais wa nchi ni mambo makubwa

Ume-conclude topic
 
alikuwa mkatili kwa nataifa ya nje. ila kwa nchi yake alikuwa mzalendo the same kwa hayati, aliwatimua wapiga bingo mjini ili aijenge nchi watu wake waje wafaidi.
Huna lolote ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani.
 
Equation ya hiki unachokisema hapa hakiwezi kuwa triggered na mtu mmoja bali collective efforts.

Kuna makundi mawili ambayo haya hayawezi kubadili mentality zao kwakua wamejinasibu kama injini ya mambo kusonga.

Kundi la kwanza la play makers hawa wanajulikana kama watu wa system ambao ni TISS, JUDGES NA JWTZ top ranking official.

Kundi hilo hapo juu ndio moyo wa mambo kwenda au kukwama nchi hii na hawa wanakula 30% ya keki ya Taifa na nitakuambia kitu. They deserve kwakua a single mistake we are all doomed.

Kundi la pili ni la Wanasiasa na wakurugenzi hawa hawapitishi tu maslahi ya kundi la kwanza bali wanajiweka nao hapo na kwakua kundi la kwanza maslahi yao yanalindwa na kundi hili hawana muda wa kuhoji kwakua huzibwa midomo kwa kuongezewa ambacho hawajaomba.

Tatizo la kundi hili la pili hawastahili wanachopata wakiwa madarakani na hata baada ya kuondoka. Kwakua they are just matairi ambayo hayahitaji kutizamwa baada ya kuondolewa kwenye gari.

TATIZO LINAPOANZIA:
Kundi la pili linatakiwa kuja na mikakati ya kukusanya zaidi ili waweze kupeleka kwa wananchi baada ya kutenga fungu la kundi la kwanza.

Sasa hawa Wanasiasa na Wakurugenzi wanaishia kuuza nyago tu na hawana la maana wanalofanya.

Mfano:
TRA/BANDARI/HALMASHAURI NA MANISPAA hawana weledi katika majukumu yao ambapo ndipo fedha inapopotelea...

Hivi unadhani ni kiasi gani cha fedha serikali itakusanya iwapo itatoa kwa kila mfanyabiashara mwenye eneo shilingi 364,000/_ kwa mwaka kwa biashara anayofanya ambayo ni Sawa na shilingi 1000 tu kwa siku?

Manispaa/Halmashauri zikiamua kukusanya kodi ya majengo tu Tanzania nzima kila jengi shilingi 364,000/- kwa mwaka ambayo ni Sawa na hilo 1000 kwa siku?

Hivi TPA wakiamua kutoza 100,000 kwa kila contena ya 40ft inayopita bandarini pale?

Mambo ni mengi sema kundi la pili ndio kikwazo

Wasalaam
 
Kaazi kweli kweli..
 
Nchi imefunguliwa mkuu.

Tusubirie zile semina za kufanyika Dubai zitafunguliwa pia....
 
Binafsi nilishangaa Rais wa nchi mashuka 200???!!!
 
Labda tupate serikali ya kijeshi!
 
Mkuu nakubaliana nawe kabisa juu ya matatizo yetu ya kiuchumi. Tatizo ni kwamba nani wa kufumua huo MFUMO? maana wanapaswa kuufumua ni wanufaika wa huo MFUMO.
 
Juzi mara baada ya mama kumaliza kikao nilimwambia wife, " kuanzisha shule moja ya wasichana kila mkoa ni wazo zuri lakini bado wazo hili la mheshimiwa Mama yetu lina njaa ya kutosha", akaniuliza kwa nini?

Unapoanzisha shule moja ya sayansi kwa wasichana maana yake umeangalia upande wa advance ambayo inategemea wasichana watoke huku O level waje kuilisha hii ya advance, sasa swali linakuja je vipi kuhusu usalama wa msichana anaetoka huku chini upoje?

Kumbuka shule nyingi za kata ambazo tunaziona mkombozi hazina mazingira salama. Ziko mbali sana na watoto wanatembea umbali mrefu hadi huruma. Wabunge wetu sijui michango yao juu ya suala la elimu huwa upoje, wamejikita kutoa shukrani na kupambia ngazi za juu kulingana na upepo unapobadilika yaani.
Kwa maoni yangu namshauri mama shule zote za kata ambazo wanafunzi wake hutembea umbali mrefu (hapa wataalamu wainishe ni kuanzia umbali upi) zijengewe mabweni kwa ajili ya watoto wote wa kike.
Na sheria zisimamiwe haswa na mtoto kipindi anaporipoti shule awe na sare peke tu ili kila mahali aendako awe na sare zitapunguza tatizo kwa kiasi kikubwa
 
Mleta mada pole sana! Japo una mawazo mazuri sana lakini utasubiri sana.
Kwanini... Hayo yote ni matokeo ya mfumo tulioukumbatia na kuuweka madarakani. Ifahamike kuwa ccm kwa sasa haina dira, mwelekeo na itikadi rasmi!
ccm ishajitenga mbali sana na jembe na nyundo. Hivyo ni rahisi sana kwa serikali na viongozi watokanao na ccm kujitenga mbali sana na wananchi!!
 
Magufuli ndo aliturudisha nyuma kwa kusema nchi hii ni tajiri na inaweza kuwa donor country
 
Umewahi kuona wapi Rais wa nchi kwenda kugawa mashuka 200 hospitali serious?

Mashuka 200, hiyo siyo hata level ya mkuu wa Kata. Mashuka inabidi siku zote yawepo hospitalini.

Level ya Urais at very least ni kuzungumzia madawa, vitendea kazi, Mishahara, Budget ya wizara ya Afya, kusimamia manunuzi ya vifaa, madawa, ujenzi wa hospitali kwamba hatupigwi.
 
Rais Samia jana kamwaga yai la Malkia Elizabeth kwa kujiamini.

Inaonekana lile neno maarufu entrepreneur haliwezi kumsumbua namna ya kulitamka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…