Rais Samia usihangaike na maridhiano, hawa hawakutaki tu kwa sababu zao

Aibu yako hii, wewe jamaa jau sana.
 
Wanaotaka maridhiano ni ccm kwani waliyazungumzia kabla ya uchaguzi nq wakayataka baada ya uchaguzi tatizo hawajui waridhiane na nani maana watanganyika wengi wamemkataa.
Angekuwa anapendwa kama unavyomnadi asingejipigia kura yeye na tume.
 
Huwezi kutawala nchi Kama hao wababe hawako upande wako huwa wanaonya sana wezetu wanasomaga upepo wa raia wengi wako upande gani kwanza sometimes ukaa upande upepo unaelekea Mama amezingua big time ukila na kipofu mfano la uchaguzi!
 
Huwezi kutawala nchi Kama hao wababe hawako upande wako huwa wanaonya sana wezetu wanasomaga upepo wa raia wengi wako upande gani kwanza sometimes ukaa upande upepo unaelekea Mama amezingua big time ukila na kipofu mfano la uchaguzi!
Tatizo ni Kikwete na machawa wake.
Alafu kuna Abduli...
 
Hapo kwenye kutumia kila cent kwa wananchi hilo halikubaliki na sio utaratibu wetu
 
Hayo maridhiano sababu yake ni ipi iliyopelekea hadi mtake maridhiano?
 
Kweli jana kwenye tamasha la miaka 30 ya bongo flava walikuwa wachache sana.
Waliandama 29/10 walikuwa wachache sana.
Ndiyo maana wakati wa kampeni zake walipeleka watoto wetu wa shule za sekondari wa kidato cha tatu na cha nne kwenye mikutano yake. Lengo kupunguza nguvu ya wachache wanao mchukia.
Mnafikiri watoto wetu wajinga? Wametuambia mlivyowasomba na mabasi kisha mkawashindisha njaa. Mkawalipa wa vyuo vikuu.
 
Hizo sababu ni zipi em ziweke wazi, je ni kutosimamia vizuri watendaji wa chini yake au ni nini?
 
Alipata 98% ya kura kuliko rais yeyote nchini kama chawa wake unadhani hizo kura ni halali na kama ni halali hiyo 2% ndiyo wanamsumbua.
Hebu tuanzie hapo kwanza majibu yako ndiyo yatazalisha maswali mengine
Wewe hujui hesabu bora hata ukasoma na kunyamaza tu. Ipo tofauti ya 98% ya watanzania na 98% ya waliopiga kura. Wewe unasema ipi kati ya hizi?
 
Akili ya kitoto, unadhani ukimzomea Rais ndiyo utapata shuka mpya? Kuna nchi Rais anapigwa kiatu usoni na bado ni Rais wao wa nchi. Kumzomea Rais na hata waziri wake ni sifa ya demokrasia iliyokomaa nchini. Inampatia sifa Rais Samia kimataifa kama hamjui. Kama wanadhani wamemshuka watakuwa wamekosea sana.
 
Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete hata Magufuli hawana record ya genocide mkuu.

Ni vigumu kuliosha tope na kulipaka rangi. Tayari ni tope.
 
Hayo maridhiano sababu yake ni ipi iliyopelekea hadi mtake maridhiano?
Ni huruma za mama na 4Rs zake tu. Mbona Magufuli aliyafunga miguu, mikono na midomo kwa miaka 6 mfululizo bila kufurukuta? Mama ndiye aliyafungulia ndiyo maana hayaogopi. Hata mataifa yanajua kuwa ni Mama Samia ndiye amewafungulia mapinzani baada ya kupigwa marufuku na JPM.

Hata Samia anaweza kuyafungia tena tena na hakuna atakayefanya lolote.
 
Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete hata Magufuli hawana record ya genocide mkuu.

Ni vigumu kuliosha tope na kulipaka rangi. Tayari ni tope.
Kama hujui kaa kimya, sema kama ulikuwa bado mtoto hukujua kilichokuwa kinaendelea. Hukuwepo wakati maiti kwenye sandarusi zikiokotwa ufukweni? Kifupi, epuka kuwa kibaraka na kuwadi wa wasiotutakia mema, utakiona. Sisi tunajua Afrika hakuna demokrasia na hakuna anaekerwa na ukosefu wa haki na demokrasia kwenye familia na jamii. Ndiyo maana kuna makabila watoto wa kike wananyimwa haki ya kurithi ardhi za wazazi wao, watoto wanakeketwa, wanawake wanachapwa na wanaume zao, shuleni unatandikwa viboko, nk. Ukiona mtu yuko tayari kufa kutetea demokrasia nchini ni muongo ni kibaraka au anatafuta hela; ukimpa ananyamaza dwiiii.
 
Kulikuwa na uchaguzi?

Au maigizo?
 
Swali sababu ya hayo maridhiano ni nini na chanzo cha maridhiano hayo ni yapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…