Rais Samia usihangaike na maridhiano, hawa hawakutaki tu kwa sababu zao

Hiyo huyo mtu
Aliyeteka maelfu ya Watanganyika
Aliyepoteza watu
Aliyekuwa maelfu ya watu
Aliyehujumu uchaguzi
Aliyebambakia watu kesi
Aliyeuza Bandari
Aliyeuza Ngorongoro
Aliyejiapisha kihuni
Ufisadi wa kutosha
Anayepuuza ripoti ya CAG

Utamwelewa kweli
 
Kibaraka !!!! Sawa mkuu. Sidhani kama ni lazima kumwaga damu ili utawale, sio sifa, sio heshima, ni laana, na tangu 1961 hatujashuhudia genocide kama ya mwaka jana na hatuombei ijirudie. MUNGU aepushie mbali.

Waliokufa bila hatia bado wamepewa majina machafu, magaidi, vibaraka na matusi yote.

Mnawatukana mpaka maiti, mliowakuta wamelala mkavunja nyumba mkauwa, duuuh mnatisha.

Hongereni. Ila MUNGU hapendi.
 
Swali sababu ya hayo maridhiano ni nini na chanzo cha maridhiano hayo ni yapi?
Ni huruma tu za Rais kwa watoto ambao walidanganywa na wahuni waichome nchi yao wakauliwa. Watubambao waliwaficha mbali watoto wao na kuwadanganya watoto wa maskini kwa kuwaaminisha kuwa jeshi liko upande wao wasiogope. Waliwapa sehemu hatari za kuchoma hata zile zinazolindwa kwa mitutu ya bunduki.
 
Tangu 1961 haikutokea watu waliochoma nchi yao kama hivi. Wangekuwepo wangeuliwa pia.
 
Mbona wewe hukutekwa? Wewe hukutekwa kwakuwa sio Kibaraka wala gaidi ba wala hukwenda kuchoma ATM na TRA, vinginevyo ungeuliwa pia.
 
Aache kuandika katiba halafu ifike 2030 uone kama tume ya uchaguzi itasimamia uchaguzi, yeyote atakayethubutu kusimama uchaguzi ajiandae kuslzikwa bila katiba mpya
 
Aache kuandika katiba halafu ifike 2030 uone kama tume ya uchaguzi itasimamia uchaguzi, yeyote atakayethubutu kusimama uchaguzi ajiandae kuslzikwa bila katiba mpya
Watu wa kufanya hivyo hatunao tz, labda mkodi mungiki kutoka Kenya. hata hiyo chadema ikifika 2030 haitakuwa chadema hii.

Shida yenu hamjui kama jeshi ni sehemu ya serikali hii ya ccm.
 
Aache kuandika katiba halafu ifike 2030 uone kama tume ya uchaguzi itasimamia uchaguzi, yeyote atakayethubutu kusimama uchaguzi ajiandae kuslzikwa bila katiba mpya
Hakutakuwa na lolote. Kama mlishindwa ile Oct29 ndio basi tena itachukua muda mrefu kutokea kitu kama kile. Na kama Rais angekuwa mwanaume kutoka Tanganyika mauaji yangekuwa makubwa zaidi ya haya na viongozi wa chadema wote hali yao ingekuwa mbaya sana.
 
Walifikiri kumuua Polepole ndio itakuwa ndio solution badala yake upinzani umezidi kuongezeka ukiwa na akili ndogo always utakuwa hivyo
Hakuna serikali legelege duniani, hakuna serikali yenye mkono mfupi.

Polepole kwani alirudi nchini kutoka Cuba?
 
Wakuu napendekeza mabadiliko ya katiba yatayo mfanya mama yetu kipenzi atawale milele
Amefanya mengi sana mazuri
Unaandika kutoka moyoni au unaandika kwa shinikizo? Kila mtu ana Mama yake Acha kujipendekeza kwa Mama wa wenzako. Eti atawale Mimi 😂 aisee yaani hii is ishakuwa nchi ya Kifalme sio kidemokrasia.

Watanzania tumekuwa na akili za kijinga na kichawa chawa halafu hapo ulipo wewe ni Baba, Mume, Kaka huko kwenye familia yako.
 
Unafanya na kundi la tatu,wasiompenda Samia na CCM.
Walikosea sana kutosikiliza ushauri wa Warioba,yule mzee aliwashauri vizuri sana kabla ya uchaguzi
 
Kwamba ni sawa kuteka, kuua, kupoteza, kubambika kesi,......kisa utofauti wa mitazamo.
 
Hata Mimi binafsi sielewi hicho mnachoita maridhiano kumbuka hao ni Wanasiasa wanatafuta Dola so ni mwendo wa battle tuu.

Hakuna haja ya kubembeleza watu Kila mtu apambane kivyake.

Kwa sababu anachofanya Sasa alijaribu awamu ya Mbowe wakaishia kumdhalilisha na kuchoma vitenge alivyowapa Sasa unadhani saizi watakuwa tofauti wakati wamejaa wahafidhina?

Yaani hapa ni kama mbwai na iwe mbwai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…