Rais Samia usihangaike na maridhiano, hawa hawakutaki tu kwa sababu zao

Narudia tena na tena! Rais asipoteze hela zetu kuandika Katiba ambayo najua haitamalizika kuandikwa kabla UKAWA hawajaukwamisha tena mchakato. Labda kama umedhamiria kuuvunja muungano wewe ukiwa ndio Rais.

Huwezi kukaa kitako kuandika Katiba yenye heri pamoja na watu ambao wako tayari kuichoma nchi iwe majivu, watu wafe na nchi ifungiwe misaada ili tu wao watawale. Chama chako cha CCM unajua kuwa kinataka Muungano wa serikali 2, na unajua kuwa vyama vya upinzani vinataka muungano wa serikali 3, hivyo unafahamu kabisa kuwa mchakato utaenda kukwama tena.

Hata Marekani kama itafanya ulevi wa kuujadili Muungano wao na kusema waandike Katiba mpya Marekani haitakuwa hii waliyonayo sasa.
 
Tangu 1961 haikutokea watu waliochoma nchi yao kama hivi. Wangekuwepo wangeuliwa pia.
Mliowauwa wamelala walikuwa wanachoma nini, na wale watoto mliowapiga risasi mgongoni na mama zao walijua lolote kuhusu maandamano ?

Mmeiharibu nchi aliyoijenga Nyerere kwa upendo mkubwa.
 
Anachotaka kufanya ni sawa na simba na nguruwe pori wakae kitako wafanye maridhiano wasidhuliane huko porini. Kama Simba atakubali maridhiano hayo atadhoofika sana kwa njaa, na pengine kufa kabisa wakati nguruwepori wakistawi na kuzaana kwa wingi. Maridhiano na Katiba mpya itaondoa nguvu za CCM na hatimaye kufa kabisa. Aliyemshauri Rais kukubali maridhiano na kuandika Katiba mpya ni adui mkubwa wa CCM, anaichukia CCM na ametumwa na wasioipenda CCM na Muungano. Historia itamhukumu Rais Samia kama Rais wa mwisho wa CCM na aliyevunja Muungano. Waliomzunguuka ama wameshindwa kumshauri vizuri ama wamemdanganya.

Asidhani kuwa Marais waliomtangulia hawakukutana na shinikizo la Katiba, bali walitafakariiiiiiii sana wakaona kuwa kuandika Katiba mpya kutavunja muungano na hasara nyingi kuliko faida. Kikwete alijifanya kichwangumu kutaka kuandika Katiba mpya ili asifiwe lakini akaachana nayo katikati ya mchakato. MAGUFULI akajifunza kutokana na makosa ya Kikwete hadi akasema "siandiki katiba mpya ng'o maana haiko kwenye ilani na wala sijaahidi katiba mpya kwenye kampeni zangu". Baadaya ya kuona hivyo wahuni wakamuingizia Samia Katiba mpya kwenye Ilani na akapiga kampeni za kuandika katiba mpya, hivyo hatakwepa kama alivyokwepa Rais Magufuli. Ndio maana wamarekani hawataki Rais mwanamke hadi leo kwakuwa wanawake wana huruma sana na rahisi kushawishiwa.
 
Kitu ambacho hakiwezekani,ni Bora aelekeze Nguvu kwenye uchumi aachane na hao vibaraka wa Mabeberu wanataka Dola sio maridhiano.
 
Mliowauwa wamelala walikuwa wanachoma nini, na wale watoto mliowapiga risasi mgongoni na mama zao walijua lolote kuhusu maandamano ?

Mmeiharibu nchi aliyoijenga Nyerere kwa upendo mkubwa.
Mjadala wa waliouliwa umefungwa. Walikuwa ni watoto wa masikini waliodanganywa/tolewa kafara na waliopanga vurugu/mapinduzi/uasi ambao ulizimwa kama kibatali.

Waandaa vurugu walikuwa wanajua kuwa baadhi ya wafanya vurugu lazima watakufa na kujeruhiwa, lakini wengine watafanikisha lengo lao. Kilichowashangaza na kuwaudhi wapanga uasi ni kuona vijana wao walizuiwa wote bila kufanikisha lengo. Askofu Gwajima na Lissu walisema kabisa hadharani kuwa wachache watajeruhiwa na kufa lakini wengi wataingia Ikulu na kufanikisha kuwatoa viongozi. Au niziweke clips zao hapa msikie?

Na kwakuwa walijua kuwa vijana na waumini watajeruhiwa na kuuliwa wengi ndio maana watoto wao hawakuwemo mule kwenye vurugu. Yaani baada ya watoto wa maskini kujeruhiwa na kuuliwa watoto wao ndiyo waliandaliwa kwenda kufaidi matunda ya uasi.

Rais Samia bado hajachelewa, atumie vurugu hizi na kukosa fedha za wahisani kuachana na kuandika Katiba mpya. Aache Rais ajae ambae ni mtanganyika na mwanaume aiandike hiyo katiba badala ya kujiongezea joto lingine.

Nadhani hata yeye analifahamu hili, ndiyo maana bajeti haina fungu la kuandika Katiba mpya. Huwezi kuzuia nchi ikose misaada halafu unataka nchi iandike Katiba, upuuzi wa kijinga. Itaandika na nini?

Unadai ulipwe ruzuku ya chama huku unashangilia nchi kusitishiwa misaada, utalipwaje sasa, yaani unashangilia unaemdai hela zako kunyimwa mkopo.
 
Kwahiyo umejibu nilivyokuuliza?

Anaehitaji maridhiano na anaetaka yafanyike ni chamagni nani?
 
Jumuiya ya madola ndio nani kwetu? Kama wanaweza siwamalize vita yao ya Ukraine na Urusi? Wamalize vita ya Sudani, DRC na Iran watu wasife?
Tanzania ni member wa commonwealth. Tulijiunga kwa hiari. Tukitaka tujiondoe wasitusumbue.
Ukraine na Urusi sio members wa Commonwealth.
 

Ukweli ni kwamba alikosa hekima. Kama angekuwa na hekima, asingethubutu kugombea.

Kama asingegombea, wengi wangekosa sababu ya kumsema vibaya:
1. Hakuna ambaye angethubutu kusema kuwa Mtangukizi wake aliuawa ili yeye awe Rais. Ambaye angesema hivyo, angekosa hoja: Watu wangehoji, kama alishiriki mauaji ya mtangulizi wake, mbona hana tamaa ya kuendelea?

Kung'ang'anua madaraka wakati watu hawakupendi, kuamua kuua watu maelfu ili uendelee kubakia madarakani, kunaipa uzito tuhuma.

Mtu wake wa karibu, tena ndugu yake, Umm alimshauri asigombee, yeye akamwona adui, akamwondoa kwenye uwaziri, akaamuru akatwe hata kwenye ubunge. Sasa baada ya maji kumfika shingoni, amejipeleka karibu naye, na kumteua eti mshauri wake! Atamshauri nini, wakati alipomshauri mara ya kwanza, ukamwona adui?

Laiti kama angekuwa na hata chembe ndogo sana ya hekima, angeachia ngazi. Haoni viongozi wengine wanavyofanya? Waziri mkuu wa UK, tena bila ya uovu wowote unaokaribia wa kwake, baada ya kugundua idadi kubwa hawaridhishwi na uongozi wake, amajiuzulu, na maisha yanaendelea. Sasa huyu kwa kung'ang'ania kubakia kwenye madaraka kwa gharama za damu za wanadamu wenzake, atapata nini zaidi ya laana? Wanaomtumia ndio wanaofaidika, ila yeye atavuna matokeo ambayo hakuwahi kuyafikiria, kuna siku ataona aheri angekuwa mvuna tende kuliko kuwa rais. Waovu walimbadili na kumwingiza kwenye uovu ili wamtumie, lakini gharama atailipa yeye na kizazi chake.
 
Kwahiyo umejibu nilivyokuuliza?

Anaehitaji maridhiano na anaetaka yafanyike ni chamagni nani?
Serikali inalo jukumu na wajibu. Wahuni hawana atakaewatathimini. Ndio maana wanaweza kuchoma kila kitu chetu
 
Wewe unajua maana ya kuwa Rais wewe au unahemka tu. Kuwa Rais sio mchezo hata kidogo. Rais Maguli alikuwa haamini kama ni kweli yeye ni Rais hadi amekufa. Yaani nisigombee Urais eti kwasababu wahuni 7 hawataki. Ni mjinga tu anawaza kama unavyowaza wewe. Hata Tump kuna wamerekani hawamtaki mpaka walitaka kumuua asigombee lakini aliendelea kugombea, na hata sasa anasakamwa sana lakini yupo tu. Unajua maana ya survival of the fittest wewe?

Huna ujualo, soma comments za wengine
 
Tanzania iko Afrika kutoa mifano ya UK ni kuonyesha hujui mambo mengi. UK kuna chama kinaweza kuchoma vituo vyao ya polisi, reli, TRA, mahakama, ATM na hospitali?

Kama wapinzani wanaifananisha tz na UK basi ujue tz imevuka viwango vya Afrika kwa ustaarabu.
 
Tanzania ni member wa commonwealth. Tulijiunga kwa hiari. Tukitaka tujiondoe wasitusumbue.
Ukraine na Urusi sio members wa Commonwealth.
Una uhakika sudani haiko Jumuiya ya madola? Una uhakika chadema itakupatia maisha bora kuliko uliyonayo sasa, how?
 
Serikali inalo jukumu na wajibu. Wahuni hawana atakaewatathimini. Ndio maana wanaweza kuchoma kila kitu chetu
Sasa anaehitaji na kulazimisha maridhiano ni nani?

Mbona kabla ya uchaguzi hamkutaka maridhiano mnayataka sasahivi?
 
Kwahiyo apoteze kodi(pesa) zetu kwenye mambo ya anasa na kuzifisadi kuliko kuandika katiba mpya yenye misingi imara ya uongozi.Nyie vilaza tu mmepata hayo madaraka kwa bahati lakini hamna uwezo wa kuongoza hii nchi.
 
"Katiba mpya haileti malisho kwa wafugaji, tena inatumia pesa nyingi ambazo hatuna"
What a shame bado kuna kenge anawaza huu ujinga,hatuna pesa ya katiba Ila tuna pesa ya kulipa PR company imsafishe samia ulaya! Na kununua magari mapya kila siku!
Katiba ndio inaamua nchi igawanywe vipi,wabunge wawe wangapi? Rais anaamua kuipa idara ya ujasusi kinga ya kuua bila kushitakiwa, katiba ndio mkataba kati ya mtawala na mtawaliwa, katiba inaamua mtu akqmatwe kwanza harafu uchunguzi baadae,katiba Bora Leo tungejua pole pole yupo wapi, nani alimpiga risasi lisu,katiba ingezuia Maghu kutumia mabilioni ya pesa kujenga uwanja wa ndege chato, ambao Leo, watu wanaanikia mahindi! Katiba ingezuia kuwaamisha wa Masai kutoka eneo Lao.
America ina katiba safi,Kenya IPO pale kutokana na katiba mpya, hakuna detention without trial, zilikiwepo kipondo cha Kenyatta na Moi, 80s, 90s, Sisi, tunaishi maisha, Kenya waliyaishi miaka,30+iliyopita,
Fikiria aliyekuwa PM Warioba kutishiwa, kuongea na kenge wa CCM,
Je wewe utafanywaje? Si watakuti.... Dole la, k..... ti harsfu useme! Asante........
 
Ni bora mungeuwa walioko barabarani wakiandamana, kuliko kupita mtaa kwa mtaa majumbani mnauwa watu ovyo kama wakusanya Kodi. Mlijipanga kuuwa ama kwa visasi au kwa maagizo.

Nakubaliana dola kukabiliana na uhalifu lakini kisayansi sio kivita.. Tatizo ni maandalizi ya vikosi vyenu waliojipanga kuuwa watu makusudi na kusingizia maandamano.

Damu ya mtu sio maji. Mmelaaniwa.

Hiyo ya ruzuku nikuulize wewe mwanasiasa, mie hainihusu wapewe au wanyimwe mtajuana na vyama vyenu.

Mikopo na misaada ya nje inayonunua risasi za kuuwa watu wako mwenyewe badala ya kujenga madaraja haisaidii maendeleo yoyote.
 
Sisi tunachojua umeme unasambazwa kwenye vitongoji, barabara zinajengwa kila kona. Vyote hivyo ni pesa zetu sio mik*undus yenus. Pale Dar nimekuta mji mzima unatimka vumbi ujenzi wa barabara. Unaposema pesa zinaliwa itakulazimu ukapimwe mkojo.

Bahati nzuri Rais ameusoma uzi huu na amesema..

View: https://youtu.be/GLCZogISSag?si=uA_HiNAVGKy1AoLC
 
Hata aliyemuua John F Kennedy Rais wa Marekani hawamjui hadi leo sembuse sisi ambao ujanja wetu ni mdogo kuliko wao. Upinzani wamepoteza sifa ya kukaa meza moja na CCM na serikali yake. Huwezi kitako na mtu anaedai anataka kuwaletea wananchi maisha bora halafu anachoma hata hicho kidogo walichokidunduliza kwa miaka 65 ya uhuru na kuzunguuka huku na huko ili nchi isipate misaada wala wawekezaji. Hata Nabii Suleiman aliwakataa watu wa aina hiyo.

Bro unapoikatia misaada nchi maskini maana yake unataka kuua watoto wa nchi hiyo wanaotegemea chanjo za misaada kuzuia magonjwa ya kuambukiza. Unataka serikali ikate fedha za mikopo ya wanafunzi ili kufidia pengo litakaloachwa na misaada ya wahisani. Yaani watu wa aina hiyo ni makosa kuwaacha watembee huru mitaani. Wataliangamiza taifa maana watawatisha hatavwatalii wasije kwetu, ni janga kama ukichekea vitendo vyao.
 
Wewe mbona uko hai, uliponaje kama walikuwa wanapita mtaa kwa mtaa kuua watu?. Acheni undezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…