Rais Samia: Vijana wanatutukana tu huko "Twitter Republic" na tunastahili

Rais Samia: Vijana wanatutukana tu huko "Twitter Republic" na tunastahili

L
"Vijana wetu hawa wako wamemaliza shule, wako wanazubaa tu huko, wengi wao wamekwenda JKT lakini wakitoka hamna kazi, wapo tu.

Lakini ni nguvu kazi nzuri, wamefunzwa maadili JKT ni vijana wazuri kwa Taifa wamefunzwa uzalendo, hawana cha kufanya.

Kazi ni kuhamia "Twitter Republic" watutukane kule na tunastahiki kwa sababu tumewasomesha hawana kazi za kufanya.

Leo hili mlilolifanya, vijana wanatoka JKT mnawadaka mnawafundisha, tunawawapatia nyenzo wanakwenda kujitegemea ni jambo kubwa sana. " - Rais Samia Suluhu Hassan

Ila Mama saa zingine unatusema vibaya sijapenda. Unatuchukulia poa sana, plz plz sio vizuri. Mie nimehitimu chuo sina ajira, well and good sio lazima wote tuajiriwe. Mwishoni mwa mwaka jana nilibeti nikapata ka kitu flani kanono kiasi chake, nikanunua pori kwa laki5 kama ekari 10 hivi nikafyeka kwa laki5, watu wa mazingira wakaja wakanitisha nami nikawavimbia na elimu yangu wakaniogopa wakaniacha. Ni Ekari 10 tu lakini zilinitoa jasho hadia aibu, shamba ninalo nalima na nini sina hata senti moja? Kwa trecta mwaka huu ekari 1 ilikua elfu50 kwa huku kwetu. Mbolea na mbegu naziona kwa watu tu, na sikua na cha kufanya. Nilikata tamaa kulima mwaka huu japo shamba nilikua nalo tayari.

Nilikuja kumpiga muhindi kwenye beting mwishoni mwa January2023 nikapata sent kidogo nikalima na trekta huku nikipanda mbegu kwa kurushia mbegu za kienyeji huku nafukuza treka. Nikapata tabu sana wakati wa kupalilia na tena nilipalilia mara moja tu badala ya mara2, Majani yalirefuka sambamba na mahindi na alizeti. Mazao yalipokomaa wezi wakanipitia kidogo kwa kujivunia mahindi na alizeti sehemu yaliposhamiri zaidi, na kwakweli nimevuna kwa tabu sana kwasababu nguvukazi ya kunisaidia sikua na uwezo wa kuwalipa. Kupukucha mahindi kila gunia sh.1100 nikalazimika baada ya kupukucha nikauza kunia moja chapchap tsh.85,000 nikalipa mpukucha mahindi chap nikalipa mifuko ya kuhifadhia mahindi ile ya bei rahisi sh.700 na mwishowe nimeambulia gunia 9 za mahindi na gunia 8 alizeti. Nikiwa narudi town bahati mbaya nilipata ajali ya boda nikalazimika kuuza gunia jingine kwahiyo store saivi nina gunia 7 mahindi na 8 alizeti, nasubiri bei ipande kidogo niuze kupata walau pesa ya kulimia mwakani. Lakini pia nataka nifyeke ekari 10 nyingine .

Jambo kubwa hapa ni MTAJI. Hata uwe na vifaa au elimu ya kilimo vizuri kiasi gani ikiwa huna mataji, huna nguvu kazi itakayokusaidia ni ngumu sana kuvutiwa na kilimo. Kuwaita vijana wazururaji si sawa. Ni ngumu mno kijana kuvutika kwenye kilimo bila kua na mtaji. Halafu kinachoudhi zaid ni bei za hovyo za serikali wakati wakenya wanakuja kununua mahindi bei nzuri mno mnawazuia mnalazimisha bei za hasara sana za serikali ukilinganisha na gharama halisi mkulima alizotumia hadi mavuno.

Kwahiyo mama acha izo bana. Twiter republic ni mahala pa kupumzikia na kujifariji baada ya kupigwa na Muhindi.
Lakini pia kwa hali hiyo apo juu , kama kijana ana moyo mwepesi hawezi rudia kulima tena.

Mtaji, Bei na Soko la mazao lisiloingiliwa na kudhibitiwa na serikali ndio pekee inaweza wavutia vijana kwenye kilimo.
 
"Vijana wetu hawa wako wamemaliza shule, wako wanazubaa tu huko, wengi wao wamekwenda JKT lakini wakitoka hamna kazi, wapo tu.

Lakini ni nguvu kazi nzuri, wamefunzwa maadili JKT ni vijana wazuri kwa Taifa wamefunzwa uzalendo, hawana cha kufanya.

Kazi ni kuhamia "Twitter Republic" watutukane kule na tunastahiki kwa sababu tumewasomesha hawana kazi za kufanya.

Leo hili mlilolifanya, vijana wanatoka JKT mnawadaka mnawafundisha, tunawawapatia nyenzo wanakwenda kujitegemea ni jambo kubwa sana. " - Rais Samia Suluhu Hassan

Watoa ajir
 
Riisiramu rinatufanya wajinga.
Mkuu habari za miaka mingi? Kwakweli ulipotea sana kwenye jukwaa, nahisi awamu ya kwanza ya awamu ya tano yote ya utawala sikuona maoni yako jukwaani.
Nimekumbuka ile mpambano wako na Mh. Zito Kabwe ndani ya jukwaa hili....ilionekana unaweza kujibu hoja kwa kuandika kwa speed ya mwanga.
Karibu sana usipotee sana, niliisi kama Corona ilikuathiri wewe na Bruce Lee.
 
"Vijana wetu hawa wako wamemaliza shule, wako wanazubaa tu huko, wengi wao wamekwenda JKT lakini wakitoka hamna kazi, wapo tu.

Lakini ni nguvu kazi nzuri, wamefunzwa maadili JKT ni vijana wazuri kwa Taifa wamefunzwa uzalendo, hawana cha kufanya.

Kazi ni kuhamia "Twitter Republic" watutukane kule na tunastahiki kwa sababu tumewasomesha hawana kazi za kufanya.

Leo hili mlilolifanya, vijana wanatoka JKT mnawadaka mnawafundisha, tunawawapatia nyenzo wanakwenda kujitegemea ni jambo kubwa sana. " - Rais Samia Suluhu Hassan

Yeye uzalendo wake upo wapi kama anauza kil kitu
 
Kutambua kuwa kuna tatizo fulani ni mwanzo mzuri wa kupata suluhisho au utatuzi wa tatizo.
Kongole kwa hili Mh. Rais SSH.
Ni hivi: ukiwa kiongozi ni jukumu lako kujua strength na weakness za wananchi wako. Tumia strength zao kuendesha nchi na weakness zao, fanya namna ya kuzi-rectify. Hii ndiyo maana ya uongozi na unachaguliwa ili ufanye haya mambo na siyo kulaumu-laumu au kulia-lia.
 
Ahsante mama Kwa kuliona hili,serikali itoe ajira Kwa wire kupunguza kutukanwa
 
Mafisadi wasisiem wanaogopa kuwekeza kwenye nchi yao mana sera za nchi zipo kwa ajili ya kuwatia umsikini wananchi wao.
Ni wajinga sana, halafu wanajiita wazalendo
Kwa unafiki waswahili hawajambo kwa kweli

Anaona bora afe aziache zioze au zichukuliwe na foreigners kuliko ziliwe na ndugu zake
Ila nao wanakufa vibaya tu
 
"Vijana wetu hawa wako wamemaliza shule, wako wanazubaa tu huko, wengi wao wamekwenda JKT lakini wakitoka hamna kazi, wapo tu.

Lakini ni nguvu kazi nzuri, wamefunzwa maadili JKT ni vijana wazuri kwa Taifa wamefunzwa uzalendo, hawana cha kufanya.

Kazi ni kuhamia "Twitter Republic" watutukane kule na tunastahiki kwa sababu tumewasomesha hawana kazi za kufanya.

Leo hili mlilolifanya, vijana wanatoka JKT mnawadaka mnawafundisha, tunawawapatia nyenzo wanakwenda kujitegemea ni jambo kubwa sana. " - Rais Samia Suluhu Hassan

Hotuba hizi,.... Zinasisimua sana.
 
Back
Top Bottom