Rais Samia: Vita ya Urusi, Tanzania hatutanusurika, bidhaa zote zitapanda bei

Rais Samia: Vita ya Urusi, Tanzania hatutanusurika, bidhaa zote zitapanda bei

Rais Samia Suluhu Hassan ameelezea kupanda kwa bei ya mafuta kwa kiasi inasababishwa na mgogoro unaoendelea kati ya Urusi na Ukraine.

“Mabadiliko ya kupanda kwa bei ya mafuta kiasi kidogo yamesababishwa na vita ya Ukraine na Urusi, yanapanda bei mno. Tanzania hatutanusurika, bidhaa zote zitapanda bei, nauli zitapanda bei kila kitu kitapanda, thamani ya kila kitu itapanda juu.

“Tumesikia minong’ono kuwa maisha yanakuwa magumu, ‘kila kitu kinapanda bei, wanasema ni hao viongozi wetu tulionao hawana baraka’.

"Si baraka ya kiongozi ni hali ya ulimwengu inavyokwenda,” amesema Rais Samia katika maadhimisho ya 'Siku ya Wanawake Duniani', Zanzibar, leo Machi 8, 2022.
Sasa sisi vita hii inatuhusu nini! Huu ni upumbafu kabisa @ yaani vita ya maisha magumu tuliyonayo ni kubwa hata kuliko hiyo
 
Rais Samia Suluhu amesema vita ya Ukraine na Russia imechangia kupanda bei ya mafuta, hali inayopelekea kupanda kwa gharama za vitu vingine.

"Mafuta yanapanda bei mno...Tanzania hatutonusurika. Bidhaa zote zitapanda bei, nauli zitapanda bei, thamani ya kila kitu itapanda."

Wanasema; kauli ya raisi tayari ni sheria.
Raisi anatakiwa awe makini na kauli ipi itoke na ipi si ya muhimu kwa ustawi wa jamii. Nalaani kauli hii kwani ni kama green light kwa mafisadi kupandisha gharama za maisha kwa wananchi wa kawaida kwa makusudi kuanzia kesho kwa kisingizio hicho alichosema Chief Hangaya.
 
..Ni jukumu la serikali yake kuhakikisha Watz hatuathiriki na vita vya Ukraine na Urusi.

..Raisi na wasaidizi wake wanalipwa mapesa mengi, na kutunzwa kwa kodi zetu, kwa matarajio kwamba watakuja na mbinu na mikakati ya kuiepusha nchi na matatizo na changamoto mbalimbali.
Huwezi kukwepa athari za vita ya Russia na Ukraine bwashee.

Jiandae kunywa chai na kiporo cha ugali.
 
Huwezi kukwepa athari za vita ya Russia na Ukraine bwashee.

Jiandae kunywa chai na kiporo cha ugali.

..Maza na serikali yake wanatakiwa kuja na mbinu za kukabiliana na athari hizo na sio kuliakulia na kulalamika.

..Kauli yake ni kama vile amekata tamaa, anasubiri liwalo liwe.
 
Shida ya huyu Mama ni kwamba HAJUI ASEME NINI WAKATI GANI... sasa ngoja vitu vipande bei mpaka ashangae mwenyewe ,
 
Anakwepa uwajibikaji wafanyabiashara wamemzidi mbinu ameona adanganye vita ya Urusi
You must be ignorant on economic issues you better shut your mouth. Hii sio siasa hapa ni hali ya kiuchumi inayosababishwa na vita, wewe hata hutazami TV au Redio (CNN, BBC nk.) unashangaza sana. Rais kasema uongo wapi huna maana kabisa.
 
Mama ni BORA LIENDE: sasa ona maajabu ... umetimua wamachinga , umerudisha kodi zile za kinyonyaji , umeruhusu watu wale kwa urefu wa Kamba , alafu leo unaruhusu vitu vyote vipande bei maana yake pesa ishuke thamani ... JIUZURU HII NCHI ISHAKUSHINDA
 
kwa huyo kipindi watu tunalalamika kuhusu kupanda kwa bei toka mwaka jana wewe mheshimiwa Hangaya hukuwepo nchini?.Naona umerudi kipindi cha vita ya urusi na ukraini.Tafadhali usihamasishe wafanya biashara kupandisha bei kwa raia unaowaongoza,unatakiwa wewe ndio usimame na raia wako kwa upande wa upandaji wa bei.
 
..Maza na serikali yake wanatakiwa kuja na mbinu za kukabiliana na athari hizo na sio kuliakulia na kulalamika.

..Kauli yake ni kama vile amekata tamaa, anasubiri liwalo liwe.
Tatizo Wese huko duniani linapanda bei kila dakika.

Sioni waziri mwenye msuli wa kutunasua katika hili
 
Back
Top Bottom