Rais Samia: Vita ya Urusi, Tanzania hatutanusurika, bidhaa zote zitapanda bei

Sasa sisi vita hii inatuhusu nini! Huu ni upumbafu kabisa @ yaani vita ya maisha magumu tuliyonayo ni kubwa hata kuliko hiyo
 
Rais Samia Suluhu amesema vita ya Ukraine na Russia imechangia kupanda bei ya mafuta, hali inayopelekea kupanda kwa gharama za vitu vingine.

"Mafuta yanapanda bei mno...Tanzania hatutonusurika. Bidhaa zote zitapanda bei, nauli zitapanda bei, thamani ya kila kitu itapanda."

Wanasema; kauli ya raisi tayari ni sheria.
Raisi anatakiwa awe makini na kauli ipi itoke na ipi si ya muhimu kwa ustawi wa jamii. Nalaani kauli hii kwani ni kama green light kwa mafisadi kupandisha gharama za maisha kwa wananchi wa kawaida kwa makusudi kuanzia kesho kwa kisingizio hicho alichosema Chief Hangaya.
 
Rais hakupaswa kusema hiyo statement kabisa...wafanyabiashara huwa wanatumia mwanya huo kupandisha Bei vitu na huduma. Pili Rais anatakiwa atumie mechanism zingine kupunguza makali badala ya kuhalalisha kuwa lazima vitu vipande...

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Huwezi kukwepa athari za vita ya Russia na Ukraine bwashee.

Jiandae kunywa chai na kiporo cha ugali.
 
Huwezi kukwepa athari za vita ya Russia na Ukraine bwashee.

Jiandae kunywa chai na kiporo cha ugali.

..Maza na serikali yake wanatakiwa kuja na mbinu za kukabiliana na athari hizo na sio kuliakulia na kulalamika.

..Kauli yake ni kama vile amekata tamaa, anasubiri liwalo liwe.
 
Shida ya huyu Mama ni kwamba HAJUI ASEME NINI WAKATI GANI... sasa ngoja vitu vipande bei mpaka ashangae mwenyewe ,
 
Anakwepa uwajibikaji wafanyabiashara wamemzidi mbinu ameona adanganye vita ya Urusi
You must be ignorant on economic issues you better shut your mouth. Hii sio siasa hapa ni hali ya kiuchumi inayosababishwa na vita, wewe hata hutazami TV au Redio (CNN, BBC nk.) unashangaza sana. Rais kasema uongo wapi huna maana kabisa.
 
Mama ni BORA LIENDE: sasa ona maajabu ... umetimua wamachinga , umerudisha kodi zile za kinyonyaji , umeruhusu watu wale kwa urefu wa Kamba , alafu leo unaruhusu vitu vyote vipande bei maana yake pesa ishuke thamani ... JIUZURU HII NCHI ISHAKUSHINDA
 
kwa huyo kipindi watu tunalalamika kuhusu kupanda kwa bei toka mwaka jana wewe mheshimiwa Hangaya hukuwepo nchini?.Naona umerudi kipindi cha vita ya urusi na ukraini.Tafadhali usihamasishe wafanya biashara kupandisha bei kwa raia unaowaongoza,unatakiwa wewe ndio usimame na raia wako kwa upande wa upandaji wa bei.
 
..Maza na serikali yake wanatakiwa kuja na mbinu za kukabiliana na athari hizo na sio kuliakulia na kulalamika.

..Kauli yake ni kama vile amekata tamaa, anasubiri liwalo liwe.
Tatizo Wese huko duniani linapanda bei kila dakika.

Sioni waziri mwenye msuli wa kutunasua katika hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…