Rais Samia: Waliopokea ongezeko la gharama za ununuzi wa ndege ya mizigo waachie nafasi zao watupishe

Rais Samia: Waliopokea ongezeko la gharama za ununuzi wa ndege ya mizigo waachie nafasi zao watupishe

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687

Kuna watu wameongeza 110% kwenye gharama za Ununuzi wa Ndege ya Mizigo. Nadhani Sasa Mh. Rais ameanza kuwafahamu Watanzania. Hawa watu msiishie kuwafuta kazi waende mahakamani.

Hii Nchi watu Kuiba ni sehemu ya maisha Yao so kuwasimamia Kwa kuwabembeleza watakutafuna Hadi ukome. Watanzania wanatakiwa kuendeshwa kama punda ndio wanaleta.

Mwisho waboresheeni maslahi Yao pia vinginevyo Kuna syndicate kubwa sana ya wizi.

==============

Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha kuchukizwa na kitendo cha ongezeko la fedha za manunuzi ya Ndege mpya ya mizigo kinyume na fedha ambazo zilikuwepo kwenye mkataba wa awali huku akiwataka Watumishi wa Serikali waliokubali ongezeko hilo bila kuhoji waachie nafasi zao kwakuwa hawana uchungu na fedha za Watanzania.

“Kuna mradi hapa tumetengeneza Ndege ya mizigo ambayo tunakaribia kuipokea, last Installments ilikuwa tulipe dola milioni 37, invoice imekuja dola milioni 86….. unauliza mkataba ulisemaje? hii imetokana na wapi?, ooh vifaa vimepanda bei, vipi? mkataba wetu ulisemaje”

“Na bado aliyepokea anakuletea Serikalini hii ilipwe ndio invoice tumepokea….. stupid, ulipopokea umechukua hatua gani? umeuliza nini? umefanya nini? ukilitazama kwa undani hili ongezeko limeanzia huku ndani kuna Watu wameongea huko”

“Hatuwezi kwenda hivyo na nadhani hawa wanaopokea hizo invoice wakazileta kwa raha zao kabisa Serikalini watupishe, hawafai kuwa kwenye hizo nafasi, kama wanafaa angepokea huko akalihoji”

“Baada ya kuhoji akasema nilipokea hivi, nimeambiwa hivi lakini bado nimeoka tufanye hivi, huyu unamuelewa lakini Mtu anapokea kwa raha zake tu analeta Serikali ‘Kuna hiyo invoice imekuja, vifaa vimeongezeka baada ya covid, pumbavu haiwezekani. Mawaziri tusaidieni over-invoicing zipo nyingi sana” ——— Rais Samia.

mizigo.jpg
==​
 
Kuna watu wameongezeka 10% kwenye gharama za Ununuzi wa Ndege ya Mizigo.

Nadhani Sasa mh.Rais ameanza kuwafahamu Watanzania.

Hawa watu msiishie kuwafuta kazi waende mahakamani.

Hii Nchi watu Kuiba ni sehemu ya maisha Yao so kuwasimamia Kwa kuwabembeleza watakutafuna Hadi ukome..

Watanzania wanatakiwa kuendeshwa kama punda ndio wanaleta..

Mwisho waboresheeni maslahi Yao pia vinginevyo Kuna syndicate kubwa sana ya wizi.

----
Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha kuchukizwa na kitendo cha ongezeko la fedha za manunuzi ya Ndege mpya ya mizigo kinyume na fedha ambazo zilikuwepo kwenye mkataba wa awali huku akiwataka Watumishi wa Serikali waliokubali ongezeko hilo bila kuhoji waachie nafasi zao kwakuwa hawana uchungu na fedha za Watanzania.

“Kuna mradi hapa tumetengeneza Ndege ya mizigo ambayo tunakaribia kuipokea, last Installments ilikuwa tulipe dola milioni 37, invoice imekuja dola milioni 86….. unauliza mkataba ulisemaje? hii imetokana na wapi?, ooh vifaa vimepanda bei, vipi? mkataba wetu ulisemaje”

“Na bado aliyepokea anakuletea Serikalini hii ilipwe ndio invoice tumepokea….. stupid, ulipopokea umechukua hatua gani? umeuliza nini? umefanya nini? ukilitazama kwa undani hili ongezeko limeanzia huku ndani kuna Watu wameongea huko”

“Hatuwezi kwenda hivyo na nadhani hawa wanaopokea hizo invoice wakazileta kwa raha zao kabisa Serikalini watupishe, hawafai kuwa kwenye hizo nafasi, kama wanafaa angepokea huko akalihoji”

“Baada ya kuhoji akasema nilipokea hivi, nimeambiwa hivi lakini bado nimeoka tufanye hivi, huyu unamuelewa lakini Mtu anapokea kwa raha zake tu analeta Serikali ‘Kuna hiyo invoice imekuja, vifaa vimeongezeka baada ya covid, pumbavu haiwezekani….. Mawaziri tusaidieni over-invoicing zipo nyingi sana” ——— Rais Samia.

Naomba kuuliza hivi TAKUKURU na watu wa intelligence hawawezi zuia haya mambo Hadi waache wizi umefanyika?
 
Usd ml37 hadi usdml86!!!
Hapana Mh Rais umezidi kuwachekea ni Tsh bilion ngapi hizo zanaingia mifukoni mwa watu?

Ndio maana kuna wapuuzi wanatuambia humu Mama kafungua Nchi kumbe ni kwa style hii?
Kweli hakuna gharama za hivyo hata kama ni covid 19,Hawa watu Fukuza na wapande Kizimbani..

Watanzania sio watu wa kuchekea Mimi nawafahamu vizuri..

Mwendazake aliwajua isipokuwa alikosea kwenye uchumi na siasa.
 
Back
Top Bottom