ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Your browser is not able to display this video.
Kuna watu wameongeza 110% kwenye gharama za Ununuzi wa Ndege ya Mizigo. Nadhani Sasa Mh. Rais ameanza kuwafahamu Watanzania. Hawa watu msiishie kuwafuta kazi waende mahakamani.
Hii Nchi watu Kuiba ni sehemu ya maisha Yao so kuwasimamia Kwa kuwabembeleza watakutafuna Hadi ukome. Watanzania wanatakiwa kuendeshwa kama punda ndio wanaleta.
Mwisho waboresheeni maslahi Yao pia vinginevyo Kuna syndicate kubwa sana ya wizi.
==============
Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha kuchukizwa na kitendo cha ongezeko la fedha za manunuzi ya Ndege mpya ya mizigo kinyume na fedha ambazo zilikuwepo kwenye mkataba wa awali huku akiwataka Watumishi wa Serikali waliokubali ongezeko hilo bila kuhoji waachie nafasi zao kwakuwa hawana uchungu na fedha za Watanzania.
βKuna mradi hapa tumetengeneza Ndege ya mizigo ambayo tunakaribia kuipokea, last Installments ilikuwa tulipe dola milioni 37, invoice imekuja dola milioni 86β¦.. unauliza mkataba ulisemaje? hii imetokana na wapi?, ooh vifaa vimepanda bei, vipi? mkataba wetu ulisemajeβ
βNa bado aliyepokea anakuletea Serikalini hii ilipwe ndio invoice tumepokeaβ¦.. stupid, ulipopokea umechukua hatua gani? umeuliza nini? umefanya nini? ukilitazama kwa undani hili ongezeko limeanzia huku ndani kuna Watu wameongea hukoβ
βHatuwezi kwenda hivyo na nadhani hawa wanaopokea hizo invoice wakazileta kwa raha zao kabisa Serikalini watupishe, hawafai kuwa kwenye hizo nafasi, kama wanafaa angepokea huko akalihojiβ
βBaada ya kuhoji akasema nilipokea hivi, nimeambiwa hivi lakini bado nimeoka tufanye hivi, huyu unamuelewa lakini Mtu anapokea kwa raha zake tu analeta Serikali βKuna hiyo invoice imekuja, vifaa vimeongezeka baada ya covid, pumbavu haiwezekani. Mawaziri tusaidieni over-invoicing zipo nyingi sanaβ βββ Rais Samia.